Hivi Rais Magufuli alifanya maamuzi ya busara kwa kuwaita Wakuu wa Vyombo vya Usalama kuongelea COVID19, badala ya kuwaita Wataalamu wa Afya?

Hivi Rais Magufuli alifanya maamuzi ya busara kwa kuwaita Wakuu wa Vyombo vya Usalama kuongelea COVID19, badala ya kuwaita Wataalamu wa Afya?

Naona michango yao tu humu!Ni analysis ya maoni tu,au niweke poll hapa uone itakavyokuwa?

Poll kamili ya kwamba Rais JPM na CCM anakubalika au hapana tunaisubiri Oktoba 2020 na siyo hii yako ya Kijinga uitakayo.
 
Poll kamili ya kwamba Rais JPM na CCM anakubalika au hapana tunaisubiri Oktoba 2020 na siyo hii yako ya Kijinga uitakayo.
Niweke poll hapa tuone wangapi wanamuunga mkono kwa hatua alizochukua dhidi ya Corona? Wewe naona uko kwenye mambo ya uchaguzi mimi niko kwenye Corona,hatuwezi kuelewana!Endelea kulamba viatu vya wakubwa wako hapo lumumba!
 
uoga

nguvu ya hoja vs hoja ya nguvu

na akishatumiaga hao jamaa hakuna anayebisha tena;

hata wale waliotaka lockdown wamenywea,japo kwa muda
 
Lihakanga, Achà kuwa mjinga. Itokeapo mambo ya usalama kitaifa hawezi kuitisha kikao mbele ya kamera na kuzungumza. Mbona mnajilisha upepo namna hii?

Anaita wakuu wa ulinzi na usalama kisha unawahutubia habari za kujifukiza na kula vitunguu swaumu?

Sidhani kama CDF aliyepita mambo kama hayo angekubali. Au kina Gen Mboma, Kyaro nk. Au hata IGP Mahita na Mwema wangekaa kimya bila kuhoji!
Kizazi hiki kimekumbwa na nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna watu huwa hawana amani na watu waliowapigia kura na kuapa kuwaongoza. Huwa hawalali mpaka IGP, Mkuu wa Majeshi na Mkurugenzi wa Usalama wawapigie simu kuwa wameshaamka na hali ni salama.
Sky Eclat
Ukiona hivyo ujue Mkuu wa aina hiyo, hajapata kihalali ushindi wake

Bali umetokana na "goli la mkono" walilosaidia kulifunga hivyo vyombo vya dola!
 
Ukitazama kwa mapana yake basi utaona umuhimu wa kufanya hivyo, ila kama utalichukulia hilo jambo katika mrengo wa afya pekee utaita madaktari peke yao bila manesi na wauguzi.
 
Poll kamili ya kwamba Rais JPM na CCM anakubalika au hapana tunaisubiri Oktoba 2020 na siyo hii yako ya Kijinga uitakayo.
Mzukulu
Kwa kutegenea vyombo vya dola, kama akivyokiri Katibu Mkuu wako wa CCM, Dkt Bashiru Ally, hakika mtaupata ushindi wa 100%

Mbona mnakataa kuundwa kwa Tume huru ya uchaguzi, kama mnajua kuwa kweli mbakubalika nchi nzima??
 
Kinachonishangaza hatujui nia ya huyu jamaa ktk nchi yetu anaonekana kbsa hayuko fit kua president alaf watu kama TISS wanaangalia tu,kweli unaeza mpa uraisi hata kingwendu na Tiss wakaufyata tu.
Mkuu kama hujui kitu bora unyamaze aisee..

Kama ndiyo mnawaza huu ujinga mtakufa sana aisee, yanayoendelea nyuma ya pazia yanasikitisha sana mzee, kama vyombo vya ulinzi na usalama havita shirikishwa mtakufa wote
 
Niweke poll hapa tuone wangapi wanamuunga mkono kwa hatua alizochukua dhidi ya Corona?Wewe naona uko kwenye mambo ya uchaguzi mimi niko kwenye Corona,hatuwezi kuelewana!Endelea kulamba viatu vya wakubwa wako hapo lumumba!
Tigershark
Mimi naendesha polls humu JF

Hadi sasa wapinzani wanaongoza kwa kura asilimia 95 na Jiwe na CCM yake wana asilimia 5 pekee!
 
Hivi unajua kuwa ndani ya Janga fulani usipokuwa makini na Usalama wako kama Nchi unaweza kutoa mwanya kwa Maadui?
Acha kuhalalisha ujinga! Kwa sasa, adui atusumbuae ni huu ugonjwa. Kwa maoni yako, Rais wetu kitisho chake yeye ni kupokonywa huo URAIS wake tu? Hajali hata Watanzania wengi wakiteketea?
 
Lihakanga, Mambo ya usalama wa nchi yanazungumzwa hadharani mbele ya macamera vile? Duuh kazi tunayo

Ukweli mchungu kwa mashabiki wa jiwe, jamaa yenu hatoshi kukalia kiti namba moja, hata uwaziri mkuu pia hafai, yaani alipaswa abakie wizarani nyampara wa barabara tu.

Paliponishangaza alivyopingana na data za task force aliyoiteua ikiongozwa na pm, yeye anasema wagonjwa waliopona zaidi ya 100 wakati pm/ummy walio front line wanatueleza tofauti

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo ni moja tu. Jiwe aliamini kuwa "ka-corona" ni kaugonjwa kanakowahusu mabeberu tu na kwa maana hakutarajia nchi "ingepigwa" na huu ugonjwa.

Maambukizi yalipoongezeka kwenye nchi yake kwa zaidi ya asilimia 500 ndani ya wiki moja akili yake ikampa kwamba "si bure, bali kuna mkono wa mtu" ambao ni wakala wa mabeberu unafanya hujuma kwa kusambaza corona kupitia fumigation, barakoa za msaada na hata vifaa vya kupimia ugonjwa wenyewe (Covid-19 test kits).

Kwa mtazamo wake huu corona ni tatizo la kiafya linalotokana na "mambo ya kiusalama" kutoka kwa maadui na kwa maana hiyo vyombo vya ulinzi na usalama vinatakiwa vifanye kazi yake kama ifuatavvyo.
1. Wachunguze ni nani alitoa amri ya kufanya fumigation Mwanza na Dar,
2. Wachunguze kubaini endapo "fumigants" zilizotumika hazikuwa na virusi vya corona kwa kuwa mlipuko uliongezeka mara dufu mara baada ya zoezi la fumigation.
3. Vyombo vya ulinzi na usalama viingie maabara kuu ya taifa ya afya (NHL-QATC) na kuchunguza ubora na usalama PCR kits zinazotoa majibu chanya mengi kwa sampuli zinazopimwa. Lakinini pia wabaini hizo kits zilitoka wapi na ziliingia kwa utaratibu gani.
4. Jeshi la polisi kwa kushirikiana na TCRA wachunguze na kupambana na watu wanaoandika taarifa "mbaya" kuhusu corona hapa nchini.
5. Wizara ya afya ichunguzwe kwani huenda inatekeleza maelekezo ya mabeberu kutoa taarifa zinanazoelemea idadi ya maambukizi mapya peke yake bila kutaja idadi ya wagonjwa ambao wamepona kama mh. Rais ali yodokezwa na "watu wake" kuwa ni zaidi 100 ndo wamepona.

Kiufupi ni kwamba Mh Rais hana imani na mabeberu. Anahisi wamesambaza ugonjwa huu ili nchi zipigike kiuchumi na ziendelee kuwa tegemezi kwa misaada na mikopo toka kwao.

Kwa Magufuli "offer" ya mkopo iliyotolewa na Benki ya Dunia katikati ya janga la corona maana yake ndo hiyo. Ndiyo maana ameijibu ofa hiyo kwa "challenge" kwamba kama kweli mabeberu wana nia njema kwa nchi zilizoathirika kiuchumi kutokana na corona, basi hiyo "offer" isiwe mikopo badala yake watoe nafuu kwa kusamehe "asilimia fulani" katika madeni yao wanayodaiwa sasa.
 
Tigershark
Mimi naendesha polls humu JF

Hadi sasa wapinzani wanaongoza kwa kura asilimia 95 na Jiwe na CCM yake wana asilimia 5 pekee!
Poll yangu ni juu ya maoni ya wananchi juu ya hatua zilizochukuliwa na JPM kama zinajitosheleza au la!
 
X-bar,
X-bar
Umetoa tathmini ya uhakika kabisa Mkuu

Ubaya huyu jamaa hajiamini na anawachukia mno mabeberu

Hivi bebebu gani alete hizo barakoa zilizopandikizwa ugonjwa wa corona?

Hiyo inaitwa ni pure inferiority complex
 
Back
Top Bottom