Hivi Rais wetu ameshindwa kabisa kuchukua hatua dhidi ya janga la kamari? Tunaelekea shimoni, nini kifanyike?

Hivi Rais wetu ameshindwa kabisa kuchukua hatua dhidi ya janga la kamari? Tunaelekea shimoni, nini kifanyike?

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
40,956
Reaction score
47,046
Kila kona ukipita wamejaa mateja wa kamari wenye msongo mkali wa mawazo baada ya kuliwa dau walizoweka, hasa sports betting, muda wote wanaomba hela tu, full vizinga, ili wakabet, na kazi hawataki kufanya wakiamini ipo siku watakuwa mamilionea.

Sasa sielewi,serikali inafurahia hili wimbi la mataahira wanaozalishwa mitaani au? Nini kifanyike?
Tunapoteza nguvu kazi ya taifa kwa kisingizio cha kodi, hii haikubaliki, kamari zichezwe kwenye makasino tu ili kuepusha vishawishi kwa watoto na vijana...
============================
 
Kuna vijana nawaona hapa wako sooo demoralised baada ya barcelona sijui kuwachania mkeka..., wanatia huruma, wako so depressed..., unaweza hisi wanataka kujiua....
 
Ndiyo ajira pekee iliyobaki,kuna mtu namjua anajenga kwa kubet
 
Kodi inayopatikana ni kubwa.
Ajira zinazopatikana pia ni nyingi hasa kwa mawakala pamoja na wanaobeti. Shukuru Mungu wewe unayo kazi kuna watu hawana kazi kabisa kwa hiyo kamari ndio kazi yao. Inawezekana usingekuwa na kazi ungekuwa unasuka mkeka.
 
Ila kuna njia mbadala za kukusanya kodi endapo hawa vijana watatafutiwa ajira za kueleweka, wakulaumiwa ni TBS na uhamiaji
Ishu ya ajira hapa Tanzania sio rahisi kama unavyofikiri. Mfumo wa kijamaa wa kumuona tajiri ni mnyonyaji na mwizi ni mfumo wa ovyo sana na ndio umetufikisha hapa.
 
mbona mimi nabet kama hobby tu! kama wewe unavyokunywa pombe!!
Kuna kijana namsikia hapa analalamika baada ya kuliwa na anatamani JPM aufungie huu uwendawazimu wa kubet, maana yeye kama yeye hawezi kujizuia
 
Ishu ya ajira hapa Tanzania sio rahisi kama unavyofikiri. Mfumo wa kijamaa wa kumuona tajiri ni mnyonyaji na mwizi ni mfumo wa ovyo sana na ndio umetufikisha hapa.
TBS wanaua viwanda vya ndani na kupoteza ajira kwa kuruhusu bidhaa feki na substandard zinazouzwa bei ya kutupa. Pia uhamiaji wanatoa vibali vya kufanya kazi kwa wageni hadi kwa kazi za kufagia choo, unategemea nini?
 
Kama ilivyo kwa vilevi kama pombe na sigara, kuna ONYO pamoja umri wa kucheza hizi kamari.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kamari ipigwe marafuku, tumefika pabaya, zunguka uone mataahira ya kamari yalivyojazana mitaani.
 
TBS wanaua viwanda vya ndani na kupoteza ajira kwa kuruhusu bidhaa feki na substandard zinazouzwa bei ya kutupa. Pia uhamiaji wanatoa vibali vya kufanya kazi kwa wageni hadi kwa kazi za kufagia choo, unategemea nini?
Kusema ule ukweli kabisa sisi Watanzania tuna lack seriousness. Mfano: Linganisha chooo cha kulipia kinachosimamiwa na mwajiriwa was serikali, choo cha kulipia kinachosimamiwa na mwekezaji Mtanzania, na choo cha kulipia kinachosimamiwa na foreigner, halafu rudisha mrejesho.
 
Wanatumia pesa yako kubet, au kuna jamaa kapiga pesa unajisikia kiwivu wivu fulani.
 
Back
Top Bottom