Kila kona ukipita wamejaa mateja wa kamari wenye msongo mkali wa mawazo baada ya kuliwa dau walizoweka, hasa sports betting, muda wote wanaomba hela tu, full vizinga, ili wakabet, na kazi hawataki kufanya wakiamini ipo siku watakuwa mamilionea.
Sasa sielewi,serikali inafurahia hili wimbi la mataahira wanaozalishwa mitaani au? Nini kifanyike?
Tunapoteza nguvu kazi ya taifa kwa kisingizio cha kodi, hii haikubaliki, kamari zichezwe kwenye makasino tu ili kuepusha vishawishi kwa watoto na vijana...
============================
Kwa wale ambao mmeshawahi kusikia namna 'punda' wa 'sembe ya mwakyembe' wanavyo 'packiwa' mizigo ya kusafirisha mtakubaliana na mimi kwamba biashara hii 'takatifu' ina faida kubwa iliyotukuka. Ni ukweli unaosikitisha kwamba 'pipi' za 'sembe' hushindiliwa kupitia njia ya nyuma mpaka tumbo lijae...
www.jamiiforums.com