Hivi redio hizi za Kimataifa BBC, DW, VOA na RFI zinanufaika na nini?

nyumbamungu

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2017
Posts
1,033
Reaction score
895
Wadau naomba kuuliza hivi redio za Kimataifa kama vile BBC, DW, VOA na RFI zinanufaika na nini kwakurusha matangazo hasa kwa hizi nchi za Maziwa makuu, (Kiswahili) kwani hazirushi matangazo ya biashara kama zilivyo redio zetu. Mfano BBC imefungua Studio kubwa naya kisasa nchini Kenya,
 
Mabeberu wanazipa ruzuku kusambaza mazuri ya wazungu, na usidhani ni kiswahili tuu wanaidhaa Mpaka za kiausa na kiigbo. Unaposikia hii ni radio DW idhaha ya kiswahili ni sawa na kusema idara ya kiswahili, utakuta wana idhaha hata hamsini za lugha MBALIMBALI duniani mpaka Afghanistan huko kwa warabu
 
Sio propaganda bali ni kutoa taarifa kwa watu wao wa kazi pia kutokana na mapungufu ya radio zenu zinazoishia Chalinze

Lakini mkuu ukiwa kwao hatuoni hizo taarifa,mara nyingi vyombo vyao vya habari hutangaza yanayowahusu tu
 
Kwenye idhaa hizo huwezi kusikia wanaitaja kwa wema Iran, Russia, Korea Kaskazini na nchi nyinginezo hasimu.
Maana yake lengo ni kuzipamba nchi zao na kutengeneza mentality ya negativity kwa mahasimu wao.

Na hii imefanikiwa sana kuipa Afrika mentality ya kumuona mzungu ndio kila kitu
 
Hiv Iran au Korea ile ya "Subwoofer" utaipamba kwa lipi?
 
Wadau naomba kuuliza hivi redio za Kimataifa kama vile BBC, DW, VOA na RFI zinanufaika na nini kwakurusha matangazo hasa kwa hizi nchi za Maziwa makuu, (Kiswahili) kwani hazirushi matangazo ya biashara kama zilivyo redio zetu. Mfano BBC imefungua Studio kubwa naya kisasa nchini Kenya,
Hili ni suala muhimu. Natamani itokee redio toka Afrika ifungue vituo US na EU halafu iwe inatangaza mabaya ya huko na mazuri ya Afrika na hata waarabu halafu niskie kama haitafungiwa ....refer to Al Jazeera ilivyofungiwa US .
 
Pia kuna channel ya African News hii nayenyewe inajaribu kutembea kwenye nyendo za akina aljazeer ila sijajua iko kwenye mikono ya akina nani, taarifa zake ni kwa lugha ya Kifaransa na kiingereza, inatangaza taarifa za afrika mara nyingi..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wadau naomba kuuliza hivi redio za Kimataifa kama vile BBC, DW, VOA na RFI zinanufaika na nini kwakurusha matangazo hasa kwa hizi nchi za Maziwa makuu, (Kiswahili) kwani hazirushi matangazo ya biashara kama zilivyo redio zetu. Mfano BBC imefungua Studio kubwa naya kisasa nchini Kenya,
Vyombo hutumika kufanyia uchunguzi mbalimbali wa kiuasalama kwy nchi zinazoendelea hasa za afrika, waandishi wengi wa habari wa afrika hutumika sana kutoa habari za kiuchunguzi pasipo kujua kuwa wanatoa habari za nchi zao kwa manufaa ya wazungu. Wazungu huwalipa kiasi furani cha pesa na trip za kwenda ulaya. watangazaji wengi kwy hizo radio ni vibaraka. Mzungu huwa hafanyi kazi isiyo na faida
 
Kwenye idhaa hizo huwezi kusikia wanaitaja kwa wema Iran, Russia, Korea Kaskazini na nchi nyinginezo hasimu.
Maana yake lengo ni kuzipamba nchi zao na kutengeneza mentality ya negativity kwa mahasimu wao.

Na hii imefanikiwa sana kuipa Afrika mentality ya kumuona mzungu ndio kila kitu
Mbona sisi tuna TBC?? Kwa nini tusishindane nao?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanahubiri Propaganda za mataifa yao kwetu.
 
Back
Top Bottom