Kwa wenye kufahamu utararatibu wanaotumia kufanikisha kurusha matangazo yao kutoka hapa Nchini. Nauliza swali hilo kwasababu mwishoni mwa mwaka jana Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) iliagiza kutolewa kwenye orodha chaneli za ndani isipokuwa TBC, katika kampuni zinazotoa huduma za kurusha matangazo ya televisheni.
Mamlaka ilitoa sababu kuwa walipoenda kwenye mamlaka hiyo kuomba leseni ya kurusha matangazo walijisajili watakuwa wanarusha chaneli za nje, hivyo hawakupaswa kurusha chaneli za ndani. Iliendelea sababu endapo wataruhusiwa kurusha chaneli za nje hapo inaweza kutokea hujuma. Kwamba tukio limetokea hapa nyumbani, habari ikatangenezwa hapa nyumbani, halafu itoke hapa iendekwanza nje ya nchi kisha irudi hapo lolote linaweza kutokea.
Hapo ndio naomba tofauti ya huo mtiririko na wanavyorusha hizo redio za kimataifa, tukio linatokea hapa nyumbani, habari wanaitengeneza hapa nyumbani, kwanini wao waruhusiwe kurusha kwenda nje halafu ndio tuipokee tena hapa nyumbani? je inatofauti gani waliokataza kwa hizo kampuni???
#tcra, #PaschalMayalla, #Nyangombali, #Domsel, #gigabyte, #Wissman, #Joshua_ok, #Mpekuzi Tanzania, #shaka-zulu, #Polonium, #mfianchi, #Wile, #Pandagichiza, #Billionea Asigwa, #thinkanyarwele, #Smart911,