Ngoja niwasaidie Kamati ya Usajiri ya Simba.
Kuna wachezaji wa Kigeni wa kuwaondoa dilisha kubwa lijalo.
Ni afadhari tuangalie wachezaji wa ndani.
Freddy. huyu haiwezi kabisa ligi ya bongo hata mkimbakisha mtakuja kumwondoa tu. kiwango chake ni kidogo sana.
Luiz Miquesson. huyu mpira umeisha kabisa. Miguu yake ishalegea na haiwezi kukaa sawa tena, sijui nini kilimpata.
Barbarca. huyu uwezo wake ni kawaida sana. anapenda kupumzika uwanjani, hafaiti kama Mzamilu. mipira mingi anarudisha nyuma. kwa kiwango chake hatoshi Msimbazi.
Ntibayonkiza. Naye aangaliwe anapoteza sana mipira shauri ya papara. Aangaliwe hadi mwisho wa msimu. Nadhani akili yake inataka mwili unakataa shauri ya Umri.
.............................................................
Per Omar Jobe kibongobongo yuko vizuri, kwa kiwango chetu cha pesa anatosha.
Onana amesha iweza ligi, aache tu ubishoo.