Sijui ni Mimi mwenyewe naona au hata nyie watanzania wenzangu.naona hii michezo ya wanawake hasa mabinti wadogo wadogo kucheza Ngoma za Uchi maarufu kama Baikoko mitaani hasa kwa Jiji la daresalam ikizidi kukuwa kwa kasi .
Mkuu wa mkoa yupo , Wakuu wa wilaya wapo na viongozi wote wa serikali wapo wanaangalia.
Hivi ni maadili gani tunaifunza jamii yetu? Naomba serikali kudhibiti hii michezo huu ni upunguwani kabisa kama siyo ufirauni unataka kuzoeleka katika jamii yetu. Inanikera sana hii tabia. Mh waziri muhusika naomba ushughulikie hili suala ASAP