Nina masikitiko sana kuhusu kupanda hovyo kwa bei ya bidhaa mbalimbali hapa nchini. Nitoe tu mifano michache niliyoyaona.
Kwa siku za karibuni nilikuwa nanunua gesi ya kupikia kilo 15 kwa Tshs.51,000 leo gesi ilipoisha nikaenda kununua na nikaambiwa bei ya gesi ya kilo 15 ni Tshs.59,000.
Sasa ukija kwenye bidhaa za ujenzi ndiyo ngoma nzito. Juzi nimenunua gypsum powder kwa Tshs.28,000 leo nilipoenda kununua kwa mara ya pili nikakutabei yake ni Tshs.32,000. Bei ya nondo, mabati, saruji na bidhaa zingine za ujenzi ndo usiseme.
Hivi Serikali inajua yote haya?. Mzunguko wa fedha haupo kabisa, kila kukicha wananchi wanazidi kuwa masikini. Hivi tukimbilie wapi?.
Na hali hii haina muda mrefu ni kama imeanza miezi miwili iliyopita. Ni wajibu wa Serikali kusaidia wananchi wake.