Hivi serikali inapata kodi kwa manunuzi ya nje ya nchi yanayofanywa na Watanzania?

Hivi serikali inapata kodi kwa manunuzi ya nje ya nchi yanayofanywa na Watanzania?

Nimetoka kulijadili hili na mtu hapa,
Kwa mfano, nikilipia kitu google play store au nikifanya in-app purchase yoyote, serikali yangu inapata chochote mle?

Na kama jibu ni hapana, serikali hawaoni kuwa wanakosa kodi kubwa sana huko? Kipi kifanyike?
Kwa uelewa wangu hawakati kodi. Makampuni haya ya kimarekani kukiwa na Kodi mteja ndio unalipa sio wao hivyo bei ingeongezeka. Sasa hivi ukinunua kitu cha dola 50 playstore unakatwa 115,000 kamili. Hapo hakuna Vat.
 
KIla chenye kustahili kodi kinalipiwa. kije kwa posta, DHL
Mleta mada mtu yeyote yule anaeagiza vitu online vikiwa chini ya $20 hicho kitu hakilipiwi kodi ila kikiwa zaidi ya $20 i.e $21 na kuendelea hicho kitu kiñapaswa kulipiwa kodi hicho kitu kiforodha kinaitwa diminìmus Uganda wao diminimus ni $50 hio nimeiona kwa bitu vidogo vidogo kama.vi parcel etc
ukinunua kitu online kikija hapa utalipia exercise duty, import duty, dumping fee, etc. ukinunua service online ina maana utatumia mb za bando lako ambalo linalipiwa kodi, hakuna utakachokwepa we tumia tu.
Boss kodi inalipwa pindi unapoingiza huo mzigo husika nchini. Mfano hai ni sisi waagizaji wa Magari kwamba, hakuna gari itapita iwe kwa ndege au kwa meli bila kulipiwa kodi na wanaangalia thamani halisi ya mzigo na kuufanyia makadirio.
Mkuu Kodi inalipwa kwa namna nyingi. Agiza kitu halafu uone kama hutolipa kitu. Usije ukawa ume post hii kwa chuki tu baada ya kuona fulani ananunua vitu nje na ukahisi halipii kodi. Agiza na wewe uone kama hutalipia.
Mtoa mada anazungumzia in app purchase, na malipo mengine ya online ya kununua Huduma. Na sio kununua bidhaa zinazoingia kwa ndege ama meli.

Mfano nanunua game online kwa laki na nusu na kulidownload kwenye computer, serikali wanapewa kodi yao?
 
Weng hatujakuelewa kwa ,kwa mujibu wa swali lako jibu Ni hapana hatlipi kwa sababu ,bado hatujafikia huko naamin,,na mnaotoa majibu ya kuagiza magar ,saa n.k.kumbuken mwenzetu hajauliza hicho mnachomjibu
mkuu tumemwelewa, nikuwa hakuna dirrect tax kwa hiyo huduma ya online services, ila zipo indirrect tax, mfano unapolipia bando linakatwa kodi ila upuuzi au maarifa utakayopata huko haulipi kodi
 
Weng hatujakuelewa kwa ,kwa mujibu wa swali lako jibu Ni hapana hatlipi kwa sababu ,bado hatujafikia huko naamin,,na mnaotoa majibu ya kuagiza magar ,saa n.k.kumbuken mwenzetu hajauliza hicho mnachomjibu
mkuu nijuavyo kodi lazima utalipa tu kama ni physical item. Itakapofika hapa nchini utalipa tu kodi zote I we kwa dhl ems,au posts utakutana na dawati LA tra utalipa kodi
 
Nimetoka kulijadili hili na mtu hapa,
Kwa mfano, nikilipia kitu google play store au nikifanya in-app purchase yoyote, serikali yangu inapata chochote mle?

Na kama jibu ni hapana, serikali hawaoni kuwa wanakosa kodi kubwa sana huko? Kipi kifanyike?
Kwa malipo ya mtandaoni kwa uzoefu wangu naona unachajiwa pesa ya kubadilisha TZS kwenda pesa za kigeni, usipofuatilia malipo unayoyafanya huwezi kujua kama kuna hela unakatwa unaponunua kitu kwa njia ya mtandao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hiyo ame edit. Alizungumzia pia Ebay, Amazon ambazo si purchase za apps.
C5CC7386-9071-4C96-A84C-B33599851C62.jpeg


Mtoa mada anazungumzia in app purchase, na malipo mengine ya online ya kununua Huduma. Na sio kununua bidhaa zinazoingia kwa ndege ama meli.

Mfano nanunua game online kwa laki na nusu na kulidownload kwenye computer, serikali wanapewa kodi yao?
 
Mtoa mada anazungumzia in app purchase, na malipo mengine ya online ya kununua Huduma. Na sio kununua bidhaa zinazoingia kwa ndege ama meli.

Mfano nanunua game online kwa laki na nusu na kulidownload kwenye computer, serikali wanapewa kodi yao?
Hapo nadhani serikali inabenefir indirectly kwenye exchange rate ya bank husika pale na yale makato makato ila kubenefit direct ni ngumu kwa mtazamo wangu..
 
ukinunua kitu online kikija hapa utalipia exercise duty, import duty, dumping fee, etc. ukinunua service online ina maana utatumia mb za bando lako ambalo linalipiwa kodi, hakuna utakachokwepa we tumia tu.
Simkodi zote unalipishwa wewe service provider .Unalambwa pesa za Kodi kuanzia exchange rate na pia Unalambwa Kodi kwenye service fee ya kutuma hizo pesa kupitia mtandao unaoutumia.Mpaka hell iondoke ushalambwa
 
TRA bado hajaweka mfumo wa kucapture online purchases za software au application kwa watu ambao hawatayarishi financial statement. Nadhani this thing is on the pipeline. Ukiwa unatayarisha financial statement definitely utaonyesha hayo manunuzi yako. Lakini TRA wakipata taarifa kuwa umefanya hivyo (purchase an app online) watakutoza Kodi
 
Hapo nadhani serikali inabenefir indirectly kwenye exchange rate ya bank husika pale na yale makato makato ila kubenefit direct ni ngumu kwa mtazamo wangu..
Mifumo bado haijawekwa, ila ikiwekwa sio suala gumu,
 
Ni jukumu la serikali kuyabana hayo makampuni ya nje japo kuna ugumu, kwasababu hayajasajiliwa huku TZ, yanapotuuzia huduma yanapaswa kulipa kodi, kwa nchi za ulaya mfano Uingereza, ukienda ebay kwa mfano kuna gharama zinawekwa kabisa ambazo ni kodi za serikali na mteja atazilipa moja kwa moja, haijalishi ni huduma au bidhaa gharama zinajikokotoa zenyewe.
Na pia ebay kama kampuni linalipa kodi UK za uendeshaji wa shuhuli zake, imesajiliwa huko na inaendesha shuhuli zake huko.
 
Kuna mifumo bado hatujaanza kunufaika nayo. Mfano Paypal mpaka sasa huwezi pokea pesa ukiwa Tanzania.
 
Kuna mifumo bado hatujaanza kunufaika nayo. Mfano Paypal mpaka sasa huwezi pokea pesa ukiwa Tanzania.
Ingekuwa PayPal inatumika Serikali Kama ilivyo kutumia tigo pesa ,mpesa,aitel money nk wangekuwa wakifaidi kwa miamala inayofanyika
 
Back
Top Bottom