Hivi serikali inasubiri watu wapigane visu kwa ajili ya Simba ndio waingilie kati?

Hivi serikali inasubiri watu wapigane visu kwa ajili ya Simba ndio waingilie kati?

Cashman

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2018
Posts
3,333
Reaction score
5,845
Siyo siri naangalia mechi hapa na Kagera naona Simba wanacheza hovyo sana,hawana morali,wanacheza kama wapo mazoezini.

Hii timu kwa sasa inakatisha tamaa
 
Kuna kosa kubwa sana wananchama wa Simba walilifanya uchaguzi uliopita. Na hili litawatafuna mpaka siku akili ziwakae vizuri vinginevyo Simba ni kaburini moja kwa moja. Hii kitu aliyoanzisha huyo mheshimiwa pale Simba eti influencer (mimi nawaita influenza) hao ndio msumari wa mwisho kwenye jeneza la Simba. Hao mainfluenza ni madalali tu hata wakijaribu kutumia neno la kiingereza.

Na siku zote dalali ni dalali tu hachelewi kuuza nyumba ya familia ilimradi kaona pesa mbele yake atauza tu halafu atakwenda kununua kiwanja hata bondeni aanze kujenga. Leo huyu anamsifia Mo kesho akipewa hela anamponda Mo yule leo anamsifia Mwenyekiti wa wanachama kesho akipewa hela anamponda Mwenyekiti wa wanachama. Na mbaya zaidi inasemekana wamepewa kadi kipindi ambacho Simba ilisimamisha kutoa kadi za uanachama.

Simba inapitia kipindi kigumu sana kuliko watu wengi wanavyofikiri. Na niiombe serikali ikamalize huo ujinga unaoendelea pale Simba kwani hayo mambo yanayoendelea hayana afya kwa Simba na mpira wa Tanzania kwa ujumla. Serikali iingilie sasa hivi na isisubiri mpaka damu imwagike. Na seriakli ikiamua hata leo hii inaweza kuondoa ule ujinga unaondelea kukua kila siku pale Simba. Ni suala tu wizara ya sheria na katiba ikishirikiana na wizara ya michezo kwenda pale Simba na kumaliza utata wa katiba ya Simba kuhusiana na uwekezaji 'full stop"

Ni mtizamo tu.
 
Serikali kupitia msajili ilitakiwa kuchukua hatua mapema kuhusu katiba ya Simba kuchezewa.
Kazi ya msajili sio kupitisha katiba tu bali kuhakikisha inatekelezwa.
Kitendo cha Mangungu kutumia busara na upande wa mo kuendelea kukaa madarakani wakati katiba haiwatambui ni uvunjaji wa katiba.
Mpira ni mchezo wa hisia siku washabiki watatoka na kumshambulia yule anayehisi anawahujumu hapo serikali ndio itaona uzembe wake.
 
Simba inachekesha kama wewe siyo shabiki wao, kwa kweli hata derby ya kariakoo inakosa mvuto hivi sasa Iko one sided mno
 
Siyo siri naangalia mechi hapa na Kagera naona Simba wanacheza hovyo sana,hawana morali,wanacheza kama wapo mazoezini.

Hii timu kwa sasa inakatisha tamaa
Serikali ifanye, iifute? iipe ubingwa bila kucheza? iue wachezaji? ilazimishe timu nyingine zisikabe wachezaji wa simba? au ifanye kitu gani roho yako iridhike,
Hivi Simba au timu nyingine yoyote zinafaida kwa mustakabali wa Tanganyika yetu? Hivi walionyeshwa hata kujali pale wananchi wenzao walivyomiminiwa risasi na kuuawa kama wadudu wasio na thamani yoyte?
 
Wataalam wanasema mpira wa tz unatumika kisiasa
Ww unaweza kuona ni tatizo ila kwa serikal inaona hii ni fulsa maana watu wanakaa kujadiri mgogoro wa Simba wanasahau kujadiri mambo ya maana kwa nchi

Yan kwa akili ndogo tu inaonesha serikal ina nufaika moja kwa moja na ishu ya simba
Asante
 
Siyo siri naangalia mechi hapa na Kagera naona Simba wanacheza hovyo sana,hawana morali,wanacheza kama wapo mazoezini.

Hii timu kwa sasa inakatisha tamaa
Mimi ni shabiki wa Simba
Kama viongozi wanahujumu timu, wacha visu vitembee😀
 
Siyo siri naangalia mechi hapa na Kagera naona Simba wanacheza hovyo sana,hawana morali,wanacheza kama wapo mazoezini.

Hii timu kwa sasa inakatisha tamaa
Pambania katiba mpya
 
Siyo siri naangalia mechi hapa na Kagera naona Simba wanacheza hovyo sana,hawana morali,wanacheza kama wapo mazoezini.

Hii timu kwa sasa inakatisha tamaa
Tatizo tajiri wenu hakuchangia bilioni kumi kama yule wa nyuma mwiko.
 
Back
Top Bottom