Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Tumemsikia mara kwa mara Rais Magufuli wakati akihutubia akisema kuwa maendeleo hayana vyama, akimaanisha kuwa serikali yake haina upendelo linapokuja suala la maendeleo ya nchi, kuwa kila mwananchi anayo haki sawa
Lakini, maneno hayo yana tofauti kubwa katika utendaji wake katika uteuzi wake wa nafasi za utumishi wa Umma katika nafasi kama vile maRC's maDC's, maRAS, maDAS, wakurugenzi wa wilaya, pamoja na nafasi zote za uteuzi katika nafasi kubwa za utumishi katika mashirika yote ya Umma, ambapo "qualification no 1" kwake Rais Magufuli, ni lazima uwe kada kindaki ndaki wa CCM.
Hivi Rais Magufuli haoni kuwa anafanya ubaguzi wa waiwazi kabisa, wakati Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya mwaka 1977, inasema kuwa nchi yetu ina mfumo wa vyama vingi?
Katika Katiba ya nchi inayoainisha hivyo, kwa Rais Magufuli kufanya ubaguzi wa waziwazi kabisa, haoni kuwa kwa kuangalia wale anaowateua katika nafasi hizo, kwa kuangalia uanachama wao wa kindaki ndaki kwa CCM, haoni kuwa anaivunja Katiba hiyo ya nchi?
Nawakaribisha wasomaji tuidadavue mada hii, kwa maslahi mapana ya Taifa hili.