Hivi sifa kubwa ya kuteuliwa na Rais kwenye nafasi za utumishi wa Umma ni kuwa kada kindaki ndaki wa CCM?

Hivi sifa kubwa ya kuteuliwa na Rais kwenye nafasi za utumishi wa Umma ni kuwa kada kindaki ndaki wa CCM?

Ni kweli kabisa.

Inashangaza kuona wale ambao ni mabingwa wa kuwatukana wapinzani, ndiyo wanaopewa "priority" ya uteuzi!
Hivi rais alipowateua wakina kitila mkumbo au mama mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro walikuwa makada wa CCM mbona marais wote waliopita hawakuwahi kuwachagua wapinzani na hamkusema?
 
Tumemsikia mara kwa mara Rais Magufuli wakati akihutubia akisema kuwa maendeleo hayana vyama, akimaanisha kuwa serikali yake haina upendelo linapokuja suala la maendeleo ya nchi, kuwa kila mwananchi anayo haki sawa

Lakini, maneno hayo yana tofauti kubwa katika utendaji wake katika uteuzi wake wa nafasi za utumishi wa Umma katika nafasi kama vile maRC's maDC's, maRAS, maDAS, wakurugenzi wa wilaya, pamoja na nafasi zote za uteuzi katika nafasi kubwa za utumishi katika mashirika yote ya Umma, ambapo "qualification no 1" kwake Rais Magufuli, ni lazima uwe kada kindaki ndaki wa CCM.

Hivi Rais Magufuli haoni kuwa anafanya ubaguzi wa waiwazi kabisa, wakati Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya mwaka 1977, inasema kuwa nchi yetu ina mfumo wa vyama vingi?

Katika Katiba ya nchi inayoainisha hivyo, kwa Rais Magufuli kufanya ubaguzi wa waziwazi kabisa, haoni kuwa kwa kuangalia wale anaowateua katika nafasi hizo, kwa kuangalia uanachama wao wa kindaki ndaki kwa CCM, haoni kuwa anaivunja Katiba hiyo ya nchi?

Nawakaribisha wasomaji tuidadavue mada hii, kwa maslahi mapana ya Taifa hili.
Mbona alimteua Anna Mngwira wa ACT kua RC? Pia alimteua Prof Kitila wa ACT kua Katibu Mkuu wa wizara. So Mhe Rais hana ubaguzi wa kichama
 
Ni kweli kabisa.

Inashangaza kuona wale ambao ni mabingwa wa kuwatukana wapinzani, ndiyo wanaopewa "priority" ya uteuzi!
sasa hivi kuelekea uchaguzi kapunguza speed kidogo ili kuwaadaa watu kwa kumtoa chizi mmoja mkuu wa Arusha na kutuma ujumbe kwa wengine kuwa watulie kwanza. ila uchaguzi ukipita huyu atapata kazi sehemu akayaendeleze.
 
Kabisa........

Ukisikia mpinzani kateuliwa kwenye nafasi za uteuzi za Mheshimiwa Rais, aidha mpinzani huyo yupo njiani kuekekea CCM, au mpinzani huyo ni kiwiliwili tu chake kipo upinzani lakini moyo wake upo CCM!
ila imetumika nguvu kubwa sana kuiangamiza CHADEMA, Mpaka Nasali kasalimu amri kajisalimisha ccm ili tu apae uhakika wa kupata ubunge! Yaelekea ubunge ni biashara inayolipa!
 
Back
Top Bottom