Yaani ukiwa yanga kweli akili zinaruka kiufupi kwenye CAF champion's league au UEFA kule kwa wazungu kila mtu anatumia uwanja wake wa nyumbani ndio kawaida ya mashindano hayo liverpool alikufa 3 pale kwa Barcelona ila Anfield alikufa 4 mtungi psg alipigwa 6 na Barcelona,
wakati watu wanaamini game ilishaisha na juzi hapa Madrid kampiga psg bernabeu hyo ni mifano tu kwa wazungu tukija africa hapa niletee takwimu za team iliyoshinda ugenini mechi zake zote au mechi mbili kwenye CAF champion's league halafu kuhusu Madrid sikusema ilikuwa mbovu ila wakati Madrid anachukua UEFA Barcelona ndo alikuwa bingwa wa league tena mara 7 mfululizo huku Madrid anachukua UEFA,
mara tatu mfululizo bila kuwa bingwa wa league point yangu ni kwamba league na mashindano ya kimataifa zinakuwa na aproach tofauti ila kabla hatujaendelea niletee team zilizo shinda ugenini mechi zote au angalau mechi mbili kwenye CAF champion's league ya africa nakusubira mkuu ili twende sawa.
Kwa ulaya hakuna timu inakuwa na Guarantee ya kuwa lazima ya kupata matokeo nyumbani kwake maana hakuna kingine zaidi ya kucheza mpira, hivyo yeyote aliyejipanga vyema anaweza kupata matokeo.
Liverpool alitolewa kwa kufungwa goli tatu pale pale Anfield dhidi ya Atletico Madrid
Atalanta kafumulushiwa huko huko kwao dhidi ya vilareal
Chelsea kafungwa na Madrid hapo hapo darajani kwao
Benfica kafungiwa huko huko kwao
Juventus katolewa na kufungwa huko huko kwao
Ajax katolewa kwa kufungwa huko huko kwao
Man U kapigiawa huko huko kwao
Liverpool vs Inter walibadilishana tu uwanja, kila mmoja akishindia ugenini kwa mwenzie.
Lile kafungwa kwao dhidi ya chelsea.
Hizo ni baadhi ya mechi za hivi karibuni ulaya, kama hakuna kingine zaidi ya mpira kuchezeka uwanjani, timu yoyote inaweza kupata ushindi popote pale.
Kwa upande wa mashindano ya Caf
1) Orlando pirates kashinda mechi mbili away
2) Soura, Al Ittihad, pyramid, Al Ahl Tripol wameshinda away na kutoa sare
3) Mamelody hakupoteza hata mechi moja away
4) Raja Casablanca, Es Tunis na Wydad Casablanca washinda mechi mbili away
Zipo timu zilizopata ushindi wa mechi moja moja away kama vile Petro de Luanda, Amazulu, Es Setif, Belouizdad