Hivi Simba SC mbona kama hawapo serious na usajili?

Kuna shida Simba hasa upande wa Management. Hapa ndipo palipotulaza na Viatu Msimu huu.

Ubahili na kutokuchukua mahamuzi ya haraka hasa panapotokea nafasi ya kupata mchezaji Mzuri pamekua na Ubahili wa kupindukia kunakopelekea kukosa Mchezaji.

Hatuwezi kusema tuna malengo ya kucheza nusu fainali ya caf kwa wachezaji wa ml 100 hizo ni ndoto za Asubui.

Timu kama Petro Atletico ya Angola wamefika nusu fainal ya Klabu bingwa mwaka huu baneti yao ni zaidi ya dola Million 20 wamewekeza wamepata matokeo.

Hatuwezi kusema tuna weka Million 800 kutafuta wachezaji Ambao watatufikisha Mbali kwenye mashindano ya kimataifa.

Nimalizie kwa kusema
Kama uongozi wa simba utafanya ujinga kama ulioufanya msimu uliopita na kutusababishia mashabiki kuzodolewa na utopolo basi ujiandae kuondoka.
 
Tulia sindano ikuingie vizuri
 
Mashabiki wengi ni watoto wadogo ambao asilimia kubwa wanaishi kwa betting.

Timu wameanza kuishabikia ikiwa na mafanikio tu hivyo hawajui kuwa football kuna kupanda na kushuka.

Simba walipata generation nzuri yenye alphamale footballers wengi wakaipa mafanikio lakin wengi wao umri umekwenda hivyo lazima kuwa na kuporomoka kidogo.


Msimu uliopita usajili ulikuwa wa vijana zaidi lengo likiwa nikuanza kutengeneza generation nyingine bahati mbaya walikuta timu ikiwa kwenye kuporomoka kwa viwango kwa wachezaji karibu wote, kutokana na uchanga wao pressure ya matokeo ikawaathiri.

Simba kushindwa kumsajili Aziz Ki siyo tatizo kwanza anakuja kucheza nafasi ya nani wakati Chama yupo na eneo la Bwalya wanataka mchezaji bora zaidi ?


Tuache pressure za kitoto.
 
Wapo kwenye mazungumzo na George Mpole. Msijali next season mtatisha sana akisimama Mpole pale mbele. Sisi Yanga wajinga sana, eti tunapambana kuwasajili kina Aziz Ki, Lazarous Kambole n.k ambao hawajui kitu waje wacheze na Mayele.wakati Mayele mwenyewe hajui chochote!
 
Yaani pamoja na kumuongezea Wawa mkataba unaona hawako serious!?
 
Mashabiki wa simba bhana! Sasa mnalalamikia usajili kutoeleweka, na wakati kocha mkuu wa timu bado haja ajiliwa!

Nadhani mngewapigia kelele viongozi wenu kuajiri kocha mpya mapema iwezekanavyo, ili afanye mchakato wa kutengeneza kikosi chake cha msimu ujao.
 
Uliaza vzr huko juu nimesomaaaa umekuja kuzingua na ushabiki maandazi wako mwisho eti ataenda kucheza namba ya nani? Nitajie wewe mchezaji wa kumuweka benchi Ki Aziz ple kwa timu ipi? Chama ana maajabu gani siku hz? Bwalya ndio haaaaaahaaaaa hovyo kabisa mna timu mbovu sana na mkileta jeuri msipokubali huu ukweli na kufanya marekebisho basi msimu ujao kazi mnayo tena
 
HII COMMENT YAKO IMEFUNGA RASMI HUU UZI[emoji3] Nimeandika kwa herufi kubwa sababu sioni vizuri[emoji1][emoji1][emoji1]
 
LK mwenye 46 apps na goli mbili,?
 
Muogope Mungu ndugu miaka mingapi? Ni miaka 4 sio 5 na ndani ya hyo miaka kuna mwaka mlitolewa mapemaaa na ud songo na juzi hp mkapopolewa na galaxy msijisahaulishe

ewaaa, ilikua mara moja jiulize kabla ya hapo mwendo wa timu ulikuaje, michuano ya kimataifa mlikua mnaishia wap, na cha muhimu zaidi ulichangia kiasi gan kabla gachori kuja, cha ajabu zaidi nani zaidi mpaka sasa imefika mil 100, wakati gachori anatafuta bil 5 za simba kila mwaka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…