Hivi Simba SC tutawahi tena kuja kuwa na Kikosi imara na cha kukumbukwa kama hiki?

Na hawakumpa heshima yake mzee wa watuu!.wabongo jaman duu!.

Sent from my TECNO-N8 using JamiiForums mobile app
 
Kikosi bora cha simba cha kukumbukwa miaka yote ni
1- Omary mahadhi
2-Daud salum "Bruce Lee'
3- Mohammed kajole " machela'
4- Aloo Mwitu
5- Mohammed Bakar 'Tall'
6- Nico Njohole
7- Abdallah Mwinyimkuu
8- Ezekiel Greyson "juju men'
9- Jumanne Hassan Masimenti
10- Adam Sabu
11-Thuwen Ally
Sub
Moses Mkandawire
Martin kikwa
Dan Mwalusamba
 
pamoja na uimara wa kikosi hchi, walikuwa wakifika kwa tim iliyoitwa Ushirika ya moshi, walikuwa wanaacha point zote pale!.

Sent from my TECNO-N8 using JamiiForums mobile app
Mkuu umenkumbusha timu ya zamani, kuna hizi tena:

-Mecco
-CDA
-Ndovu Arusha
-Pilsner
-Pan Africa
-Sigara
-Nyota Nyekundu
 
Hapo waongeze Mark Sirengo,Yusuph Macho,Noely Joely na kuna jamaa alikuwa ni beki kutoka Zambia jina limenitoka,umenikumbusha mbali sana kpind hicho nikiwa nasoma drs la nne

Sent from my TECNO-N8 using JamiiForums mobile app
 
Dah wakat mwingne unakuwa na akili
 
Icho kikosi kilinufaisha vipi taifa letu?

Kiliwafanya Dada zako wengi wapate ' Ujauzito ' jambo ambalo lilisaidia Wao kutuzalia Watoto ambao leo hii ndiyo wapiga Kura wetu wa ' Kutukuka ' hapa nchini Tanzania na pia wameweza kuisaidia nchi kwa kulipa Kodi katika kila huduma ambayo wamekuwa wakiipata hivyo kupelekea maendeleo ya haraka na Kiuchumi ya Tanzania.

Swali lingine Mkuu kama lipo niulize tafadhali.
 
hapo kwenye 5. Victor Costa (Patrick Betwel ni season ya nyuma yake), pia Kureshi Ufunguo kabla ya Waso? Christopher Alex na Ulimboka kwenye 4 na 11. , season iliyofuata, (walitoka reli ya morogoro) No. 11. Mark Sirengo. Afu kwa ndani sometime pia alikuwa Madaraka na Nteze John. Tusker Cup yanga chini ya Tarimba ilipigwa 4-1, la tano Shekhan Rashid aliwaonea huruma akaurudishia ndani dana dana mpira ukaisha. Goli la tatu yanga walianza kurusha chpa za maji n.k.!
 

Hiko ni ' Kikosi ' changu hivyo tafadhali sana ' usinilazimishe ' nikubaliane na cha Kwako. Narudia tena kusema na kusisitiza kuwa ilikuwa ni ngumu sana kuwa na Kikosi ' imara ' kipindi hiko bila ya kuwepo na huyo Mchezaji aliyekuwa na ' Kipaji ' cha aina yake hasa katika nafasi ya Kiungo au Beki wa mwisho ' Kitasa / Libero ' kama Patrick Betwel Buba ' Mmasai '. Mtafute Mtu yoyote wa Simba SC anayejua hasa mpira mwambie akupe kidogo ' Wasifu ' wa Betwel hasa Kiuchezaji. Marehemu Siang'a nakumbuka kila ambapo alikuwa akimuona Betwel akifanya vitu vyake ' mazoezini ' muda wote utamwona Baba wa Watu anatabasamu tu kwani alikuwa ' anaburudishwa ' nae mno. Betwel alikuwa ana ' control ' ya ajabu utadhani alizaliwa na mpira wake huko ' Umasaini '.
 
Omar mahadh
Kajole
Shaban baraza
Daud salim
Aluu Alli
Umar Gumbo
Khaidar
Athuman Mambosasa
King Kibaden
Ezekiel G Jujuman
Abbas Dilunga
Malota soma
Abdallah Mwinyimkuu
hebu endeleza

Omar Mahadhi hakucheza na Shaaban Baraza, Gumbo, Haidari, Abbas Dilunga, Malota Soma hizo ni awamu tangu 1972 hadi 1992 miaka 20!

1972: John Semainda, Shaaban Baraza, Mohamed Kajole, Arthur Mambeta, Juma Mzee, Khalid Abeid, Willy Mwaijibe,....., Adam Sabu, Athuman Abdallah Kibaden, Emanuel/ Choteka. mechi ya 1 vs Yanga 1-1, marudiano Yanga 1-0. Mpira ulivurugika kwa fujo zilizoanzia kwa wapenzi wa YANGA, baada ya Simba kucheza mwingi si kawaida, Yanga ikiwa inaongoza moja(Chitete) mpira ulimalizwa kabla...Yanga ikawa bingwa

1973: Athuman Mambosasa, Baraza,Kajole, Mambeta,Chogo,Khalid,Willy Mwaijibe, Michael Sentala?Sabu?, Haidari Abeid, Kibaden, Abbas Dilunga. Simba 1-0 Yanga, dakika ya 17, Haidari alifunga kwa kichwa, cross ya Willy(Mokili) baada ya kumwabia Sentala "Miss the Ball", Sentala akampoteza Kapera kwa kuinama. Simba ilichukua ubingwa baada ya miaka 5 mfululizo ya Yanga. Ubingwa Africa, 2-1 dhidi ya Lesotho, 3-2 dhidi ya mufulira wanderers. Walipitia Iringa kumchukua Sadi Ally wa African Wanderers ya Iringa. Wakaingia robo fainali na Accra Hearts of Oak. Mambosasa alikuwa amefichwa na Yanga Jangwani akarudi simba. Ikaitoa Oak mabingwa watetezi mwaka ule, ikaingia semi-final na Mehala El Kubra ya Misri. Saad Ally alifunga dakika ya 90 Dar. Kule Egypt nao wakafunga moja, kukatokea fujo nyingi, Simba ilitolewa kwa penati. Final ilikuwa Mehala na mabingwa wa Congo Brazaville. Raisi Ngouabi wa congo alipeleka timu na makomandoo, mehala ilitolewa, ubingwa ukaenda kongo. Timu mpya simba ilikuwa: Mambosasa, Baraza, Kajole, Athuman Juma, Aloo Mwitu( hawa wawili walitoka Lake Star Kigoma na kudumu Simba kwa mafanikio makubwa. Kwa kumbukumbu zangu walicheza Simba mpaka wanastaafu hawakuwahi kufungwa na Yanga> Sawa na Matola, Costa, Pawasa, Machupa, n.k ), wengine ni kina Chogo,Khalid, Gumbo, Mwaijibe, Haidari, Sabu, Sadi Ali, Kibadeni na Abass Dilunga. Baada ya kukosa klabu bingwa ndiyo ikaja fainali ya 1974 Nyamagana. Simba ilipoteza ubingwa kwa 2-1, afu na ubingwa wa Africa Mashariki kule Zanzibar kwa 2-0. Yanga ikashiriki klabu bingwa Africa, wakatolewa na Enugu Rangers, wakafukuzwa wote first eleven na mabeki wakahamia Nyota Africa Morogoro, baadaye wakaunda Pan African. Kuanzia 1976, Simba ilichukua ubingwa kwa miaka karibu 7 mfululizo mpaka yanga ilivyokombolewa na akina Juma Mkambi?...etc.kwenye early 80s. Hiyo simba ya kuanzia 1977 ni moja ya Peaks za performance yake, kwani ilikomba karibu timu yote ya taifa:
Mahadhi/Mambosasa, Daudi Salum, Kajole, Athuman Juma/Alloo Mwitu, Mohamed Bakari(Tall), Nico Njohole, Willy Mwaijibe/George Kulagwa(Best), Aluu Ally/Ezekiel Greyson, Sabu,Jumanne Hassan (Masimenti yaani Nascimento ya pele), Kibadeni, Martin Kikwa...pia akina Abdallah Hussein, Ismail Mwarabu na Abdallah Mwnyimkuu. Hii sehemu kubwa ndiyo iliifunga yanga 6-0. Inaaminika hii timu ingeifunga timu yeyote duniani. Bahati mbaya karibu wote walienda Arabuni baada ya kutolewa kwenye mojawapo ya makombe ya klabu bingwa, simba ikaanza tena na vijana, mkongwe pekee akiwa Kajole na Daud Salum. Hawa vijana ndiyo walifanya muujiza wa 4-0 kugeuza to 5-0 Kwa Mufulira wanderers 1979.

Simba kali zilikuwepo na zitakuwepo hata Taifa Stars, tatizo ni vilabu kidogo, uyanga na usimba kidogo na zaidi BMT na FAT, sasa TFF. Bado matumaini yapo.
Mnisamehe kwa hadithi ndefu nilitaka niweke histroria kidogo wazi kwa faida ya vijana wapya.
 
Umemsahau
YaHaya akili mali victor coster nurdin bakar haruna mosh noban
IlikuwA noma sana those day football were used to be football sio cku hiz wachzaji ni Jerry muro na kaka haji manara

Sent from my TECNO-C5 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu umenkumbusha timu ya zamani, kuna hizi tena:

-Mecco
-CDA
-Ndovu Arusha
-Pilsner
-Pan Africa
-Sigara
-Nyota Nyekundu
mkuu kweli bana pindi hiyo ndiyo palikuwa na wasukuma goz kweli siyo hawa wa ss hv wanacheza huko bukta iko kwenye kata k!..tim ulizozitaja hapo zilikuwa c mchezo,Kuna hzi pia Pamba ya kina george masatu,wazir mkuu ya dodoma,milambo ya tbr,Tukuyu stars,yakule mbeya,kuna Reli ya moro iliitwa kiboko ya vigogo,majimaji ya songea ya akina kicho chilemba,nk.ila hapo kwenye nyota nyekundu kuna wachezaji wawili walikuwa wakinifurahisha kwwli.rosta nduguru(mzee wa rafu) na itutu kigi acha kabisa muzee!.sijui hawa watu wapo wapi ss hv

Sent from my TECNO-N8 using JamiiForums mobile app
 
Zimbaaaaa mnyamaaaaaa! Waarabu wanaita Zimbaaaaaaaa!
Waliochuchumaa kutoka kushoto;
Athumani China, Dua Said, ........
Waliosimama kutoka kulia;
George Masatu, Mustaga Hoza, Hussein Masha, Mohamed Mwameja, George lucas(sima uhakika), madaraka suleimani(mzee wa kiminyio)....
 
Mkuu umenkumbusha timu ya zamani, kuna hizi tena:

-Mecco
-CDA
-Ndovu Arusha
-Pilsner
-Pan Africa
-Sigara
-Nyota Nyekundu
Alafu Zenji kuna;
-Small Simba,
-Malindi,
-Mlandege.

Ukirudi bara;
-biashara shinyanga
-rtc kagera kina mkama ntare
-ushirika ya moshi
-ujenzi hii sikumbuki ilikuwa ya wapi, sijui Rukwa???
 
Nakumbuka niko mkoani saa mbili kasorobo usiku tuko redioni rtd kusubiri matokeo ya mechi zingine kipindi cha michezo.
 
Hiko kikosi kilichukua kombe la klabu bingwa afrika?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…