Omar mahadh
Kajole
Shaban baraza
Daud salim
Aluu Alli
Umar Gumbo
Khaidar
Athuman Mambosasa
King Kibaden
Ezekiel G Jujuman
Abbas Dilunga
Malota soma
Abdallah Mwinyimkuu
hebu endeleza
Omar Mahadhi hakucheza na Shaaban Baraza, Gumbo, Haidari, Abbas Dilunga, Malota Soma hizo ni awamu tangu 1972 hadi 1992 miaka 20!
1972: John Semainda, Shaaban Baraza, Mohamed Kajole, Arthur Mambeta, Juma Mzee, Khalid Abeid, Willy Mwaijibe,....., Adam Sabu, Athuman Abdallah Kibaden, Emanuel/ Choteka. mechi ya 1 vs Yanga 1-1, marudiano Yanga 1-0. Mpira ulivurugika kwa fujo zilizoanzia kwa wapenzi wa YANGA, baada ya Simba kucheza mwingi si kawaida, Yanga ikiwa inaongoza moja(Chitete) mpira ulimalizwa kabla...Yanga ikawa bingwa
1973: Athuman Mambosasa, Baraza,Kajole, Mambeta,Chogo,Khalid,Willy Mwaijibe, Michael Sentala?Sabu?, Haidari Abeid, Kibaden, Abbas Dilunga. Simba 1-0 Yanga, dakika ya 17, Haidari alifunga kwa kichwa, cross ya Willy(Mokili) baada ya kumwabia Sentala "Miss the Ball", Sentala akampoteza Kapera kwa kuinama. Simba ilichukua ubingwa baada ya miaka 5 mfululizo ya Yanga. Ubingwa Africa, 2-1 dhidi ya Lesotho, 3-2 dhidi ya mufulira wanderers. Walipitia Iringa kumchukua Sadi Ally wa African Wanderers ya Iringa. Wakaingia robo fainali na Accra Hearts of Oak. Mambosasa alikuwa amefichwa na Yanga Jangwani akarudi simba. Ikaitoa Oak mabingwa watetezi mwaka ule, ikaingia semi-final na Mehala El Kubra ya Misri. Saad Ally alifunga dakika ya 90 Dar. Kule Egypt nao wakafunga moja, kukatokea fujo nyingi, Simba ilitolewa kwa penati. Final ilikuwa Mehala na mabingwa wa Congo Brazaville. Raisi Ngouabi wa congo alipeleka timu na makomandoo, mehala ilitolewa, ubingwa ukaenda kongo. Timu mpya simba ilikuwa: Mambosasa, Baraza, Kajole, Athuman Juma, Aloo Mwitu( hawa wawili walitoka Lake Star Kigoma na kudumu Simba kwa mafanikio makubwa. Kwa kumbukumbu zangu walicheza Simba mpaka wanastaafu hawakuwahi kufungwa na Yanga> Sawa na Matola, Costa, Pawasa, Machupa, n.k ), wengine ni kina Chogo,Khalid, Gumbo, Mwaijibe, Haidari, Sabu, Sadi Ali, Kibadeni na Abass Dilunga. Baada ya kukosa klabu bingwa ndiyo ikaja fainali ya 1974 Nyamagana. Simba ilipoteza ubingwa kwa 2-1, afu na ubingwa wa Africa Mashariki kule Zanzibar kwa 2-0. Yanga ikashiriki klabu bingwa Africa, wakatolewa na Enugu Rangers, wakafukuzwa wote first eleven na mabeki wakahamia Nyota Africa Morogoro, baadaye wakaunda Pan African. Kuanzia 1976, Simba ilichukua ubingwa kwa miaka karibu 7 mfululizo mpaka yanga ilivyokombolewa na akina Juma Mkambi?...etc.kwenye early 80s. Hiyo simba ya kuanzia 1977 ni moja ya Peaks za performance yake, kwani ilikomba karibu timu yote ya taifa:
Mahadhi/Mambosasa, Daudi Salum, Kajole, Athuman Juma/Alloo Mwitu, Mohamed Bakari(Tall), Nico Njohole, Willy Mwaijibe/George Kulagwa(Best), Aluu Ally/Ezekiel Greyson, Sabu,Jumanne Hassan (Masimenti yaani Nascimento ya pele), Kibadeni, Martin Kikwa...pia akina Abdallah Hussein, Ismail Mwarabu na Abdallah Mwnyimkuu. Hii sehemu kubwa ndiyo iliifunga yanga 6-0. Inaaminika hii timu ingeifunga timu yeyote duniani. Bahati mbaya karibu wote walienda Arabuni baada ya kutolewa kwenye mojawapo ya makombe ya klabu bingwa, simba ikaanza tena na vijana, mkongwe pekee akiwa Kajole na Daud Salum. Hawa vijana ndiyo walifanya muujiza wa 4-0 kugeuza to 5-0 Kwa Mufulira wanderers 1979.
Simba kali zilikuwepo na zitakuwepo hata Taifa Stars, tatizo ni vilabu kidogo, uyanga na usimba kidogo na zaidi BMT na FAT, sasa TFF. Bado matumaini yapo.
Mnisamehe kwa hadithi ndefu nilitaka niweke histroria kidogo wazi kwa faida ya vijana wapya.