Huyo alikuwa ' anasubiri ' kwa Mchezaji ' Kipenzi ' changu ambaye mpaka leo bado sijaona ' Mchezaji ' yoyote anayemfikia na huyu si mwingine bali ni Patrick Betwel Buba ' Mmasai '. Makocha wengi wa Kigeni wa Simba SC kipindi kile kila walipokuwa wakimwona walikuwa wanamuuliza alikuwa anafanya nini hapa Tanzania? Kwa kukusaidia tu hata ' uchezaji ' wake ' Marehemu ' Christopher Alex alikuwa akimuiga sana ' Mtaalam ' Patrick Betwel Buba ' Mmasai '. Betwel alikuwa na kila kitu ambacho ungetaka kukiona kwa ' Mchezaji ' wa mpira hasa wa nafasi ya Kiungo wa Ukabaji au ' Kitasa '.