Hivi sisi wenye Samsung galaxy 6, na iPhones tunachanganya post zetu Humu na wenye tecno na itel?

XDA verified member, androidpt verified member, crackberry partner member,
 
Tecno hizo sio Samsung eeeeh [emoji120]
Kwa wanaojua simu kwa sasa Tecno na Samsung zote fungu moja tu, labda zinazidiana daraja katika fungu la simu mbovu.

Nami nimetumia Samsung kwa kama miaka 10 iliyopita mpaka nimeacha mwaka jana. Nimeanzia kwenye flip phone mpaka Note 2 all the way to 6. Kila ikitoka Note mpya nilikuwa nachukua.Tena Samsung bora hata simu za zamani kuliko hizi mpya.Kwa hiyo nazijua.
 
Basi sawa [emoji122][emoji122][emoji122]
 
Unauliza nini mkuu ? Kwani unapotumia hicho ki Iphone chako na mwingine Itel hizo keyboards zake zinatofauti kwamba ukiandika embe kwenye Iphone basi Itel itaandika magimbi ?
Tofauti zipo, button za itel, tecno, huaiwei zinaumiza vidole, i mean ngumu
 
Sasa na sisi tunaotumia nokia tochi sijui tuseme nini sasa [emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
 
Wewe ni mtu wa ajabu sana.Yaani unaona kuwa na Galaxy au iPhone inakufanya uwe bora zaidi kuliko mwenye Tecno.Hapana ndugu yangu,hayo ni mambo tu ya kupita,wala hayakufanyi uwe a better person than others.Change your mindset.
Tofauti ipo kubwa tu, simu ya laki 2 huwez compare na simu ya 1.5m
 
Watu mnakaa na visimu vya kuhongwa mnavimba kama mimba za mbilikimo bora itel na tecno ya jasho kuliko iphone na galaxy za kushikishwa ukuta.

Tena shukuru sana leo sipo kwenye mood ya kutukana.
 
Tofauti ipo kubwa tu, simu ya laki 2 huwez compare na simu ya 1.5m
Utakuta simu ya laki 2 ina Android 5.1 na ya milioni 1.5 ina Android 4.4
[emoji125][emoji125][emoji125][emoji125]
 
Ukute una hiyo IPhone 6 halafu daily unakimbilia mlimani ukajiunge bando la chuo [emoji23] [emoji12]
 
Watu mnakaa na visimu vya kuhongwa mnavimba kama mimba za mbilikimo bora itel na tecno ya jasho kuliko iphone na galaxy za kushikishwa ukuta.

Tena shukuru sana leo sipo kwenye mood ya kutukana.
Mkuu kwani Si una Toleo jipya la tecno wewe? Why povuz
 
Unauliza nini mkuu ? Kwani unapotumia hicho ki Iphone chako na mwingine Itel hizo keyboards zake zinatofauti kwamba ukiandika embe kwenye Iphone basi Itel itaandika magimbi ?
Au akiandika Sharif Hamad kwenye Iphone basi Itel itaandika Prof Lipumba .
 
Aisee upo vizuri yaani kila ikitoka mpya ulikuwa unachukua, inaelekea mambo muhimu yote Mzee umeshayamaliza. Big up kwako me hata kiwanja bado siwezi shindana na simu.
 
🙄 una Iphone/Galaxy 4.4 yeye ana Tecno/itel 5.1 nakuendelea nan mjanja???? wewe Una iPhone/Galaxy unaunga bundle la 500 ikizidi ni 1000 yule ana Tecno/Itel anaunga Bundle la 50000 nakuendelea na hawazi hata kidogo nan Mjanja???? Teh teh teh teh(Vijana Bhana!!) j
 
Mkuu kwani Si una Toleo jipya la tecno wewe? Why povuz
Siku zote wanasema kimbiza mwizi kimya kimya hakuna anaejua mwenzake humu anatumia simu ya aina gani kila mtu anaona tu comment tu wengine tupo kwenye dekstop ila ujanja mwingi kama vile tuna iphone 8
 
Aisee upo vizuri yaani kila ikitoka mpya ulikuwa unachukua, inaelekea mambo muhimu yote Mzee umeshayamaliza. Big up kwako me hata kiwanja bado siwezi shindana na simu.
Ni mipango tu ya maisha.

Wengine teknolojia hizi ndizo kazi zetu, kwa hiyo hutakiwi kuwa nyuma katika fani yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…