Hivi Spika Ndugai ameokoka siku hizi?

DATAZ

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2012
Posts
3,799
Reaction score
10,196
Mheshimiwa Job Ndugai, umekuwa ukihaha sana kwa siku za hivi karibuni kikosoa serikali kwa Mambo menngi. Kimsingi serikali sio Mungu na huwa inakosea sana. Japo pia makosa mengi ya serikali zetu yalitokana na udhaifu na Unafiki wa Bunge ambalo wewe umekuwa sehemu ya uongozi wake kwa muda mrefu.

Ndio maana uliwahi hata kujishangaa mwenyewe ulipong'aka na kuhoji Bungeni kuwa "HIVI KWELI SHERIA HII TULIIPITISHA SISI HUMU BUNGENI"?

Lakini usisahau kuwa wale waliokuwa mstari wa mbele kuikosoa na kuikumbusha serikali wajibu wake walichukiwa na kupigwa vita na cha ajabu na wewe Ndg Ndugai ukaungana kuwapiga vita kwa namna namna.

Leo unahitahidi kuwa Kiongozi wa mhimili na Kiongozi wa Upinzani Bungeni kwa dhambi uliyoiunga mkono na kuishiriki kwa gharama zote na rasilimali za Bunge.

Wewe sio mwana CCM kuliko Hayati Mwalimu Nyerere, Lakini Mwalimu Nyerere aliona wazi bila Upinzani Nchi hii ingeenda kusiko, akasimama kidete kuunga mfumo wa vyama vyingi Nchini.

Kila serikali huja na maono yake pamojana kubeba mizigo na madudu ya watangulizi wake. Muache Mheshimiwa Samia atekeleze aliyokusudia na wakati ndio utamhukumu sio Bunge dhaifu.
 
Unafki na chuki binafsi ndivyo vinamuongoza Ndugai yeye na genge lake la kina Polepole.

Mama awe mkali kidogo atoe kafara watu wawili watatu kwa kuwafukuza uanachama wale wanaojiona MaConky kwenye chama na serikali ili adabu na nidhamu vichukue mkondo wake.
 
Job anakiona kibanzi jichoni mwa ndugu yake, lakini papo hapo haioni boriti iliyoko jichoni mwake. Yeye ndani ya mhimili wa Bunge lake analo boriti lakini anakiona kibanzi katika mhimili mwingine.

Nahisi amewekwa nje ya "inner circle" vile kama ilivyokuwa wakati wa mwendazake. Hiki anachokipitia hivi sasa na kukionyesha ni dalili za sonono na jakamoyo.

Atambue tu SSH ni kiongozi wa taasisi nyeti ya urais na pia ni Mwenyekiti Taifa wa chama chake. Akileta za kuleta hatakuwa akipambana naye bali Vita ataipata kutoka kwa wasaidizi wake.

CCM wana msemo wao kuwa atulie na aheshimu kiti. Akishindwa kupambana naye, ajisalimishe na kujiunga naye. Tunajua maumivu yake yanatokana na jiji la Dodoma kutokupewa hadhi yake, kizungumkuti cha bandari ya Bagamoyo, sura fulani asizozikubali kupewa uwaziri na pia chuki zake binafsi kwa mtu anayemwona kuwa ni dhaifu na asiyetosha katika nafasi aliyopewa.

Bosi ni bosi, na yupo hapo pengine mpaka 2030. Kumng'oa 2025 ni jambo gumu sana, ingawaje kwa CCM hii dhaifu inawezekana na kuwafanya wasambalatike na kugawana fito.

Mwl. Nyerere aliwahi kusema, upinzani wa kweli utatokea hapa nchini, pale CCM itakapo gawanyika mapande mawili. Naiona CCM ya SSH na ile ya JPM zikisigishana.
 
CCM wenye walikosea kuiita hii awamu ya sita…wakati ni transition tu. Uongozi ukianza lazima uwe na vision halafu kinachofuata ni utekelezaji. Sasa mtu unaachiwa shamba la mihogo uliambiwa nguruwe wafungwe kwanza mpaka tuvune maana ni kikwazo kwa maendeleo ya shamba.

Wewe unakuja kuachia nguruwe sijui ukifikiria wewe ni mjanja zaidi au ni mwema au labda mihogo unaijua sana kuliko mwenye maono ya shamba lake au labda bwana shamba katili nguruwe wana haki ya kuwa huru mihogo itapatikana kweli. Lazima watu wavurugane na shamba halitakuwa salama..maana halina mwenyewe.
 
Akili kama hizi ndio zinafaanya hii nchi ijae wanasiasa wanafiki..

#MaendeleoHayanaChama
 
Huyu alitaka Katiba ifanyiwe marekebisho ili Dikteta atawale milele Bogus kabisa.
Nina imani na naamini kuwa iko siku Ndugai atatoka hadharani na kumuomba Msamaha Tundu Lisu kwa uovu aliomtendea; kumnyima matibabu live bila chenga wakati ni stahiki yake, kuongopea dunia hajui alipo wakati anaona na kusikia kila siku akifanyiwa operations kutokana na majeraha ya risasi alizopigwa maeneo ya bunge mchana kweupe, kumvua ubunge kwa hila bila kumlipa stahiki zake pamoja na kumdhihaki kwa madhila aliyopitia.

Nasema na narudia tena iko siku ataomba msamaha hadharani na kama hatafanya hivyo hiyo dhambi haitamtoka kamwe.
 
Maslai ya mswahili yanapokoma akili urudi toka likizo.
Yule aliyepita aliwatuza Sana waimba kwaya.
Ilikuhitaji dakika 5 kuimba kwaya kesho asubui umeletewa v8 na barua ya uteuzi.
Chawa wameyakosa haya ndo chanzo cha makelele,mara wahuni,mara kukopa,mara sijui amaleki,nk.
 
Job ishu ya Dodoma kufifia na aliwekeza pesa zake zote Dodoma huku akijua arudi tena kutafuna kodi zetu 2025 imemchanganya Sana maana wanasiasa wetu hawana ujanja wa kuishi nje ya kupewa,hata kama wanamiliki mabus au malori wape miaka 3 baada kuwa bench Hakuna bus wala roli utaliona barabarani wanaendesha biashara kwa kodi zetu,rejea mabus mbwembe ya Buffalo, scandinavian,nk pale kodi zetu zilipofika ukomo wa kuingia kwenye makoti yao na biashara zilikufa.
Usiendeshe biashara kwa pesa ya ofisi.
 
Huruma ya mzazi ndo imemponza,sisi wapiga kelele tulimuonya mapema mwanzo tukimtakia mema,wasio watoto wako fukuza nadhani ameelewa sasa.
 
Afanye hivo mapema kabla hajavuliwa uanachama,kwamaana hata eleweka.
 
Unadhani kuwatoa kafara 2 au 3 nirahisi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…