Mheshimiwa Job Ndugai, umekuwa ukihaha sana kwa siku za hivi karibuni kikosoa serikali kwa Mambo menngi. Kimsingi serikali sio Mungu na huwa inakosea sana. Japo pia makosa mengi ya serikali zetu yalitokana na udhaifu na Unafiki wa Bunge ambalo wewe umekuwa sehemu ya uongozi wake kwa muda mrefu.
Ndio maana uliwahi hata kujishangaa mwenyewe ulipong'aka na kuhoji Bungeni kuwa "HIVI KWELI SHERIA HII TULIIPITISHA SISI HUMU BUNGENI"?
Lakini usisahau kuwa wale waliokuwa mstari wa mbele kuikosoa na kuikumbusha serikali wajibu wake walichukiwa na kupigwa vita na cha ajabu na wewe Ndg Ndugai ukaungana kuwapiga vita kwa namna namna.
Leo unahitahidi kuwa Kiongozi wa mhimili na Kiongozi wa Upinzani Bungeni kwa dhambi uliyoiunga mkono na kuishiriki kwa gharama zote na rasilimali za Bunge.
Wewe sio mwana CCM kuliko Hayati Mwalimu Nyerere, Lakini Mwalimu Nyerere aliona wazi bila Upinzani Nchi hii ingeenda kusiko, akasimama kidete kuunga mfumo wa vyama vyingi Nchini.
Kila serikali huja na maono yake pamojana kubeba mizigo na madudu ya watangulizi wake. Muache Mheshimiwa Samia atekeleze aliyokusudia na wakati ndio utamhukumu sio Bunge dhaifu.