Hivi suala la kugawa vishkwambi linahitaji sherehe kweli?

Eti na helikopta juu,hii haikubariki ni matumizi mabaya ya pesa za Umma..

Watu ambao hawajajiajiri hao hawaoni uchungu na pesa zetu na Hawa ndio wanadiscourage watu kulipa Kodi.

Planning kwa watumishi wa umma kwenye nchi zetu ni hafifu sana kwa mfano madarasa ya milioni 75 ambayo ni matatu yanaenda kuzinduliwa na msafara wa milionj 25 kosa hiyo itumike kuongeza darasa jingine
 
Halafu viongozi wanaonaga wananchi kama wajinga utakuta mradi mmoja mfano daraja kwanza viongozi wote wanalitembelea, wanaweka jiwe la msingi, halafu wanazindua ujenzi, halafu wanakuja kulifungua na bado watatembelea hapo hapo miaka nenda rudi na inakua kama habari vile,
 
KAMA NI KWELI BAS HII NCHI INAZIDI KUPUNGUKIWA IDADI YA WATU WENYE AKILI TIMAMU
 
Mimi naona hamna tatizo kwasababu hana kazi lazima atafute kitu cha kumkeep busy. Ni kama tu polisi wa Norway wakipigiwa simu mlevi kaanguka wanakuja faster kumhudumia angalau siku iyo wawe busy.
Umenikumbusha. Niliwahi kuona huko kwa wenzetu mtu anapiga simu 911 eti paka wake kapanda juu ya paa na kakataa kushuka na kweli rescue team ilikuja kumshusha paka!!!! Nikasema we have a very very very long way to go!!!!
 
Mkuu, siyo kupenda sherehe. Hii ni sehemu ya propaganda za CCM. Serikali zote zenye malengo wa kijamaa huwa zinaendeshwa kwa design hii ya propaganda, propaganda...... Same as China, Russia, North Korea, Venezuela na Cuba.
 
Swali la kujiuliza ni je, Samia haoni haya matumizi mabaya yanayofanywa na hao aliowateua??

Au yeye akishateua basi..inakuwa sawa na kwenda haja na kusahau.
Huyu mama ameshaorojeka kabisa kiuongozi.
Acha kashfa kwa cheo cha urais, hayo unayoyaona wanafanya watendaji ndio tabia halisi za jamii yetu ya Kitanzania.... kupenda raha na starehe
 
Anayepangiwa bajeti ya mabilioni ya kuendeshesha sherehe/matukio za/ya kitaifa/kiserikali ndiye huyo anayepanga tukio gani lifanyike kama sherehe na ndiye huyo anayeenda kukabidhi hivyo vishikwambi!!
Hii nchi tuna tatizo mahali pengi ila kuanzia ni top 3 wote kutoka/kutolewa.
 
Mdororo wa Brain power πŸ˜… hatar sn !!
 

Hizi siasa za kiki muasisi wake ni Magufuli. Kila jambo alikuwa anaenda hewani na sifa kibao. Matokeo yake CCM wakajiaminisha kuwa hizo kiki ndio kukubalika. Serikali ya sasa nayo imeeiga ujinga ule ule kwenye hiyo dhana potofu ya kukubalika kwa promo za kijinga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…