Hivi Sungura anataga Mayai au Anazaa? Nimeulizwa na binti aliyetoka kufanya Usaili wa ualimu hivi karibuni

🤓🤓😂😂

Inategemea na sungura yupi.
Kwenye Fasihi Sungura anaweza kutaga na kuzaa papo hapo
Hizo ni hadithi mkuu. Halafu sungura sio mnyama mgeni kabisa maana karibia Kila kabila Lina hadithi zake tangu utotoni hadithi za sungura na fisi au na kobe tumesimuliwa sana
 
Umeamua kuwavua nguo walimu sasa
Hapan mkuu huenda wapo wengi wa namna hii hivyo ni vyema sisi tukaangalia namna ya watoto wetu waweze kujifunza kwa vitendo kama nilivyo eleza.

Umewahi kuulizwa yesu alikuwa mwanamke au mwanaume? Jibu ni hujawahi maana viongozi wa dini wanapewa kipindi Kila ijumaa ama jtano
 
Huyo asifaulu hiyo interview atafanya vijana wetu wa kayumba kuwa vilaza walioshindikana.
Kabisa. Pia Kuna shida kwenye elimu yetu.Mwalimu anayefundisha biology hajawahi hata kuona viumbe anao wafundisha nayeye kakaririshwa vilevile
 
Kwanza kabisa kwa maelezo uliyoyatolea sijaona haja ya kuhusanisha kulaumu mfumo wa elimu bali ni ujinga wa mtu binafsi kuuliza kama mnyama anataga.
Pili wewe kwakuwa unajua kuwa sungura hatagi hakukupi nafasi ya kupata darasa la kufundisha kuhusu ufugaji wa sungura isitoshe umewapata siku chache kama ulivyosema. Lakini point ya kusema wafugaji (ambao siyo wewe) wapewe vipindi chuoni naafikiana na wewe,kuna wafugaji wanafuga kisasa kwa models ambazo hazifundishwi kwa vyuo vyetu ambapo wahitimu wanaotoka chuoni wakipata nafasi kwenye hizo farms wanaanza kufundishwa upya. Vyuo vinaweza shirikiana na hawa kwa kuwapa vipindi ili kupanua wigo wa ufahamu wa mambo mengi na mara nyingi huwa ni technlojia ya ulimwengu wote kwa ujumla na kuwawezesha wahitimu kuwa na wigo mpana wa ajira
 
Sahihi mkuu ndio maana nimesema ni kitu kidogo sana........ mkuu kwa mfugaji yeyote wa muda mrefu anakuwa anajua vitu vingi sana kiuhalisia na tofauti na muhitimu wa kitengo husika.

Hivyo ukubali ukatae wanafunzi wakipelekwa shamba wakiwa na mkufuzi wao pamoja na mkulima/mfugaji watapata elimu na majibu ya maswali Yao.

Hata kama hujui kma sungura anazaa au anataga ukifika shambani utaambiwa hawa sungura Wana mimba na wapo karibu kuzaa....na badae mtaonyeshwa watoto wa sungura hivyo utaelewa vizuri.

Sikupingi nakubaliana nawewe.
 
Hukuwa na sababu ya kuandika hayo yote. Nyie mngemjibu tu kuwa "Sungura anazaa".
Kutokujua hilo haimanisi hana elimu na kwamba hafai kuwa mwalimu.
Yapo mambo mengi sana watu hawayajui ila siju ikiwapasa kuyajua huyajua kuanzia hapo na wanaweza hata kuwaelekeza wengine.
 
Nilishakutana na vituko kàma hivi toka mwalimu graduate, nilishangaa sana. Ikabidi niulize rafiki zake kama ni kweli ana degree ya ualimu.
Kuna majanga ya kutisha kwenye mfumo wa elimu nchini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…