Naona watanzania kwasasa wengi wao wamekuwa na hulka ya kupiga picha na hela trna hela za kutosha. Je tabia hii wewe unaichukuliaje, ujanja au ushamba?
View attachment 2771898
Ukiona MTU anatumia nguvu Nyingi, kuiaminisha dunia yupo vzr, kifedha, ujue huyo ana msongo wa mawazo,na Hana ka kitu, ni choka mbaya, anafanya hayo kujipa aueni ya fedha,
Ukifika pale Tigo,makao makuu, wale staff walioajiliwa na Tigo kama Tigo, au huawei, hawanaga swaga Nyingi, wengi ni humble Sana, wanamkwanja mrefu, hawana haja ya kupiga makelele kila MTU ajue,utajua tu kwa yanayoendelea kwenye maisha Yao,
Sasa omba ukutane na wale freelancers wauza vocha, kwanza swaga Nyingi, na kutumia nguvu Nyingi, watu wajue kuwa wao ni wafanyakazi wa Tigo, au wale wadada wa call centre ukikuta wamepiga T-shirt zao za Tigo, wana mbwembwe Sana, ukimuuliza, anasema ni mfanya kazi wa Tigo, kumbe ni wakandarasi, tu wanapokea 400K gross!
Kwenye pesa hqkuna kelele, wenye hela hawana kelele, Umeishawahi kuona V8 cruzer imepasuliwa exhaust inapiga kelele kama vi arteza, au Subaru?!
Kwa wenye pesa no kelele, cheki Masaki, upanga dar, area d, Kisasa Dodoma, au, shangani mtwara, sasa nenda Chaduru, au Tandale, kila Kona ni makelele.