Hivi tafsiri ya 'Breaking news' ni 'Habari mpasuko'?

Hivi tafsiri ya 'Breaking news' ni 'Habari mpasuko'?

Breaking news ina dimension 2:
- ni habari mpya na haijaongelewa kwa hivo habari moto moto au habari pya, habari inayoingia ni sawa
- ni habari haikusemwa kwenye taarifa ya habari ya mwisho na haiwezi subiri taarifa ya habari inayo kuja au itakua yakwanza kwenye taarifa ya habari hiyo, na inavuruga mpango wa kawaida wa matangazo: hapo ndipo inakua "breaking" yeneywe.
Tafsiri yake kwa kiswahili inatakiwa ireflect hizo dimension zote mbili.
Mi naona maybe Habari ya dharura... but hata mimi sijawa convinced...
 
kuna media moja hupenda kusema "Habari zilizotufikia hivi punde" binafsi ningesema habari zilizotufikia ghafla!

Nikweli kabisa ila tupate maneno mafupi yenye kuashiria maana hiyo ili iwe rahisi kuwekwa katika TV.
 
Breaking news ina dimension 2:
- ni habari mpya na haijaongelewa kwa hivo habari moto moto au habari pya, habari inayoingia ni sawa
- ni habari haikusemwa kwenye taarifa ya habari ya mwisho na haiwezi subiri taarifa ya habari inayo kuja au itakua yakwanza kwenye taarifa ya habari hiyo, na inavuruga mpango wa kawaida wa matangazo: hapo ndipo inakua "breaking" yeneywe.
Tafsiri yake kwa kiswahili inatakiwa ireflect hizo dimension zote mbili.
Mi naona maybe Habari ya dharura... but hata mimi sijawa convinced...

Ni 'habari zinazoingia sasa hivi'. Kwangu hiyo imetulia zaidi.
 
Breaking news ina dimension 2:
- ni habari mpya na haijaongelewa kwa hivo habari moto moto au habari pya, habari inayoingia ni sawa
- ni habari haikusemwa kwenye taarifa ya habari ya mwisho na haiwezi subiri taarifa ya habari inayo kuja au itakua yakwanza kwenye taarifa ya habari hiyo, na inavuruga mpango wa kawaida wa matangazo: hapo ndipo inakua "breaking" yeneywe.
Tafsiri yake kwa kiswahili inatakiwa ireflect hizo dimension zote mbili.
Mi naona maybe Habari ya dharura... but hata mimi sijawa convinced...

Kwakweli maelezo yako yameniongezea ufahamu nakushukuru sana!
 
hii mada ni nzuri, ukijadili zingatia kuwa habari husika haijatokea studio, habari hiyo si ngeni ilipotukia (eneo la tukio) nina wasiwasi huenda tumepata hasara kwa kuyakimbia mashairi, kama ilivyo kwa ,hatimaye, kuwa mwisho wa siku, na breaking news ni HABARI ZIMETINGA!
 
Wala siyo marefu kama unavyodhania. Ni maneno manne tu.
Ni kweli uko sahihi kwa kuanzia itafaa ila kitaaluma inatakiwa kuwe na istillah. Ambayo ufafanuzi wake utakuwa maneno hayo manne.!
 
Hehehee! Ni habari zilizo katika katika! Hihiii!:flypig:

Nimekuwa nikifuatilia matangazo ya TBC1 wamekuwa wapenzi sana wa wa kutumia neno habari mpasuko. Sijui wamepata wapi kiswahili hiki? Nionavyo kuna makosa. Ilipaswa watumie 'Habari motomoto'. Hawapaswi kutumia tafsiri sisi kwa neno hilo.
 
Breakin News ni Habari Punde::: kwanini wasi,tumie marine hassani anaonekana ni mtaalamu mzuri wa kiswahili na kingereza
 
Breakin News ni Habari Punde::: kwanini wasi,tumie marine hassani anaonekana ni mtaalamu mzuri wa kiswahili na kingereza

Nimeridhika na pendekezo la kuita 'habari punde'. Ila kumtumia MARINE HASSAN hapana, tena yeye naona ndiye anaye waharibu kabisa wenzake. Anaingiza maneno sijui anayapata wapi. Mfano. Utamsikia akisema waziri alikuwa 'akihudumu' katika.. Anajifanya kuchanganya kiswahili cha lafudhi ya kenya. Yeye anafahamu viswahili nasio kiswahili. Wakati mwingine napata kichefuchefu. Na ninamkumbuka mwl wangu Prof. Kahigi.
 
Kiswahili ni chakwetu ila kinakua taabu kukifafanu
 
Mantiki nzima ya breaking news imepotea kabisa hata kwenye vyombo vya habari vya kimataifa. Kuna kipindi hata BBC walilalamikiwa kwa kuweka breaking news which were not even news in the first place. Wakati mwingine nafikiria Channel ilisahau kuweka something they wanted to in their broadcast. So they dress it up and call it "Breaking News" to get more attention for it. Kwa nini wasiseme tuu: Habari zilizotufikia hivi punde?. Habari mpasuko? No way.
 
Me naona wangetumia neno hili habari za kushitukiza.
 
Back
Top Bottom