Hivi tafsiri ya 'Breaking news' ni 'Habari mpasuko'?

Hivi tafsiri ya 'Breaking news' ni 'Habari mpasuko'?

Hii pia nimeipenda...
Habari ilio ingia ghafla ni sawa sababu ina onesha emergency na uncontrolable nature ya habari. Ila habari zimeingia sasa hivi hazina ile dynamics....
Better yet: Habari ya ghafla or Habari ghafla ila sijui kama semantic iko sawa hapo kwa kiswahili...
 
breaking news maana yake ni habari mshitukizo, maana yake haikutarajiwa ila imeibuka katika hali ya kutokutarajiwa.
 
breaking news Kwa kiarabu الأخبار العاجلة
kwa kiswahili kuvunjika kwa Habari

Kwa Lugha ya kifaransa les dernières nouvelles

kwa lugha ya ki taliano : ultime notizie

Kwa Lugha ya Kispanyola noticias de última hora

Kwa Lugha ya kihindi खबर

Kwa Lugha ya KiJerumani. breaking news
 
Habari ilio ingia ghafla ni sawa sababu ina onesha emergency na uncontrolable nature ya habari. Ila habari zimeingia sasa hivi hazina ile dynamics....
Better yet: Habari ya ghafla or Habari ghafla ila sijui kama semantic iko sawa hapo kwa kiswahili...
Nadhani 'Habari ghafla' au ' Habari mshtukizo' yangefaa zaidi kuliko habari mpasuko.
 
breaking news Kwa kiarabu ??????? ???????
kwa kiswahili kuvunjika kwa Habari

Kwa Lugha ya kifaransa les dernières nouvelles

kwa lugha ya ki taliano : ultime notizie

Kwa Lugha ya Kispanyola noticias de última hora

Kwa Lugha ya kihindi ???

Kwa Lugha ya KiJerumani. breaking news
Mzizimkavu nakushukuru kwa kutuonesha mitindo mbalimbali ya kuashiria 'breakingnews'
 
breaking news maana yake ni habari mshitukizo, maana yake haikutarajiwa ila imeibuka katika hali ya kutokutarajiwa.

Nakubaliana na wewe! TBC Wangehitaji wangepata maoni mazuri kama haya. Kweli kwenye wengi pana mengi.
 
Acha direct translation, nakushauri uangalie dictionery badala ya kutusumbua
 
umoto moto wake ni nini, tetea hoja yako..kwanini moto moto??

Breaking new huwa ni sensitive news ambazo ndio zinatoka hewani na zinagusa hisia za walio wengi-(mawazo ya kwangu). Hivyo nadhani motomoto linaweza kufikiriwa!!! Naona mwandishi hayuko mbali sana na maana ya breaking news.
 
Acha direct translation, nakushauri uangalie dictionery badala ya kutusumbua
Ndugu yangu nadhani kama kidogo hujanielewa. Wanaotumia direct translation [tafsiri sisi] ndio hao wanaoita habari mpasuko. Sisi sasa wacha tujadiliane, tutapokea mawazo mazuri ambayo yatatusaidia kuelewa usahihi wa jambo hilo. Kukusaidia tu maana ya kitu kupata kwake wkt mwingne inatakiwa uhusishe na mazingira na mahusiano. Ingekuwa rahisi hvy husingesikia habari mpasuko.
 
Breaking new huwa ni sensitive news ambazo ndio zinatoka hewani na zinagusa hisia za walio wengi-(mawazo ya kwangu). Hivyo nadhani motomoto linaweza kufikiriwa!!! Naona mwandishi hayuko mbali sana na maana ya breaking news.
Nakushukuru kwa ufafanuzi mzuri. Nafikiria angalau mpaka hapo tumepata picha fulani. Nawashukuru wote kwa michango yenu mizuri kabisa. MUNGU AWABARIKI.
 
leo wkt wa kipindi cha jambo tbc marine hassan amesema
'mda umekwenda matiti'
akiwa na maana mda umekwisha na akasisitiza kuwa hakukosea wala kumaanisha ya akina mama, bali ni kiswahili sanifu na kinachokubalika
 
Ili liendelee kuwa na MNOGO wake si vibaya tukilikopa
hili neno na kulihalalisha kuwa la kiswahili kwani binafsi naona
ni "Habari kali zilizotufikia hivi punde" Tukitafsiri sana ndio
yale yale ya Kompyuta kwa kiswahili nani anafahamu? na kama
anafahamu nani anatumia?
 
leo wkt wa kipindi cha jambo tbc marine hassan amesema
'mda umekwenda matiti'
akiwa na maana mda umekwisha na akasisitiza kuwa hakukosea wala kumaanisha ya akina mama, bali ni kiswahili sanifu na kinachokubalika

Mkuu naona ni bora watumie Kiswahili kinachoeleweka na watu wa kawaida. Muda umekwenda matiti inawezekana ni Kiswahili safi lakini ni watazamaji wangapi watajua maana yake? Unakuta badala ya kujadili yaliyojiri kwenye taarifa ya habari, watazamaji wanajadili maana ya lugha iliyotumika. Sio sahihi. Nimeona hata kwenye local TV zinazotumia lugha ya Kingereza wanatumia Kiingereza kigumu kupita hata CNN au BBC. Haileti maana. Vyombo vya viangalie zaidi jinsi ya kufikisha ujumbe kwa walengwa badala ya lugha.
 
Back
Top Bottom