Swali zuri lingekuwa wananchi vijijini wanapata milo mingapi kwa siku na milo hiyo inacomprise nini?
Why discuss macdonald, kfc, steers, mary brown wakati idadi kubwa ya watu wanaishi kwa asali na ubuyu ( wenye bahati ) miaka zaidi ya 40 baada ya uhuru na kuahidiwa maisha bora kwa kila mtanzania.
...hivi tuna matatizo ya ukomo wa kufikiri?
Cha msingi watanzania tunakula vyakula salama ukilinganisha na hizo processed food wanazokula wenzetu, ukikuta chakula cha standard yetu kina lebo 'Organic' na bei juu.
Kama unataka macdonald ukiwa bongo umeipata - kanunue mkate na mayonnaise kibandani mtaani kwenu, tafuta kipande cha nyama upendayo choma chemsha juu yako, kata pande la nyanya na kitunguu, usisahau pande la kabichi weka hivyo vyote katikati ya mapande mawili ya mkate tafuta mkeka na kokakola jichane.
...mawazo yale yale ya Ubepari ni adui wa haki!
MacDonald=Unhealthy food. Hatuitaki Tanzania.
...kwani unalazimishwa ule?
Kwanza hatutaki zije, haina maana kufagilia ajira zinazohatarisha maisha ya watu. Junk food should be discouraged with all efforts. Let our people eat their natural/organic food. Can't you see problems of obesity escalating in those western countries? The main reason,among others,is junk food! Usifagilie kila kitu cha huko majuu my buddy.
...yale yale,...! target ni kina nani kaka?
Ukitaka unaweza kuongea nao uanzishe. Target yako itakuwa middle class people. Pia unaweza kutumia akili yako na kuanzisha franchise yako binafsi. Huhitaji jina la Macs. Tena kwa nchi kama tz ambapo wao hawajapata market share...inakuwa fresh kabisa.
...angalau wewe umeangalia nje ya boksi!
kwa hiyo nyie mnaoipinga in maana ikija itaathiri afya za watanzania wote au itasababisha msiwe na maisha bora mnayoyangojea kama nchi ya ahadi?????
..hebu waulize...
Hivi Mcdonalds kuna ugali nyama choma jamani. Achilia mbali kiti moto. Kama hamna, basi haina haja hapa bongo.
...hii ndio athari ya kila kizuri tunasema cha kizungu.
Bandugu mna bore!...
Hivi mnadhani kilio cha serikali watalii/expatriates waje kwa wingi Tanzania maana yake watakula kwa mama Ntilie? au mnataka wale huo ugali na nyama choma mnazozifagilia hapa?
Hamjaweza fikiri MacDonalds watawezesha ajira ngapi hapa nchini? kuanzia wafugaji, wafanyakazi, suppliers, nk? Leo hii hamuoni faida ya Mahoteli ya kitalii, Supermarkets chache tulizonazo, au Mlimani City kwa mfano mdogo?
Hatuwezi kuishi kwa kutarajia mama ntilie atakidhi mahitaji ya
watu wote wanaoishi Mijini.
Kwa taarifa yenu, watalii wengi kwenye vigezo vya health & safety hupendelea kula kwenye known/tried and tested franchise kama hizo tajwa hapo awali, ikiwemo KFC, Burger King, Nandos etc, sio kwa mama Ntilie!
Msidhani kuwa kuiga mifumo ya kimagharibi ni dhambi ati tu kwakuwa Mwl Nyerere alisema wao ni makabaila na wanyonyaji! Tumejiingiza kwenye mfumo wa soko huria, lazima twende na matakwa yake.