Hivi Tanzania kuna sehemu hawajui Kiswahili?

Hivi Tanzania kuna sehemu hawajui Kiswahili?

Kuna watu wanaishi nyuma ya ule mlima?
Utatokea nchi hiihii ya tz... Moro hiyohiyo...Ila kuna jamaa alituambia eti kuna upande wa mlima ukivuka upande wa pili unatokea mjini halafu distance yake ni fupi sema kikwazo ni mlima tu... Ndo tulitaka tujue kama ni kweli au cheche coz ukiwa town unauona mlima vzr tu.
 
Hakuna
tapatalk_1581350246957.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndiyo mkuu hata Nigeria [emoji1184] kuna sehem za nchi yao watu hawajui kiingereza
 
Nop sikuvuka kiongozi...Tulikuwa wengi nia yetu ilikuwa kufika kilele cha mt.uluguru... Lakini tulipokaribia juu wengine wakaanza kuchoka na kuanguka anguka.. Walioshindwa safari tuliwaacha nyuma ila ilifika kipindi tukabaki wachache na muda uliyoyoma hivyo tukageuza kuwarudia wenzetu... Tukapita mashambani kwa waluguru ndo wakatupa hayo makaroti,ndizi wengine wakapewa hadi cabbage...Tukanywa maji tukaenda kilimahewa kushangaa shangaa baadaye tukarudi shule.
Kwa kalembawani hukooo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mongwe kule kipindi nasoma mzumbe sekondari niliendapo mara moja moja... Watu wanajua kiswahili na vigodoro wanacheza waluguru hao.

Nakumbuka nilitoa mia mbili nikapewa karoti nyingi kwelikweli na ndizi nikapiga deshi lunch... Waluguru noma.
Mpaka sasa..siku hizi sema mambo yamekaza sio nyingi kaama miaka ile.
 
Miaka mitatu iliopita tulienda (kifamilia) kijiji cha lusangi wilaya ya kondoa, tulienda kwenye nyumba ambayo mwenyewe tulimfaham, tunakaribia kufika palikuwa na wadada wawili wamekaa nje ya nyumba hiyo, ghafla wakasimama wakakimbilia ndani!

Tunapiga hodi hawaitikii wapo ndani!
Walibakia kutuchungulia tu na kurudi ndani, hawaongei!

Mpaka mwenyeji aliporudi ndo tukajua kuwa hawajui kishwahili.

Na kwamba walitokea kijiji kingine cha janjaluse.

Na pia nimepita hii njia ya pori kwa pori ambayo unapita kongwa, baadhi ya vijiji vya mpwapwa kabla hujatokea kilosa.

Kuna watu hawajui kabisa kishwahili kule!

Ndo mara ya kwanza naona ktk nyumba ya familia ndani kuna kondoo wanakaa pamoja na nguruwe, kuku, mbuzi.

Na wote hao ikifika asubui wanafunguliwa wanazurura kooote kutafuta chakula.
Kumkuta nguruwe jalalani kwako ni sawa na kumkuta mbwa!

Lakini pia kuna maeneo watu wakiona gari wanakimbia!

Nimeendesha gari nikiwa ktk mradi wa utafiti wa maeneo yenye madini.

Kilindi tanga nako kuna wanguu hawajui kiswahili na maeneo menginewe!

Sent using Redmi Y2
 
Back
Top Bottom