Ndugu yangu, usifikiri ni utani, ni kweli Yesu yuaja upesi (Ufu 22:10-12)
Kwa ujasiri kabisa unafurahia kutupa habari za matendo ya uzinzi na uasherati? Kweli?
Au wewe mwenzetu una mbingu yako? Maisha haya yana mwisho kaka, na baada ya maisha haya kuna hukumu. Itakusaidia nini kufurahia tendo hilo kwa dakika chache halafu siku ya mwisho uangamie katika moto wa milele?
1 Kor 6:9
"Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti."
Haya, sijui utajitetea nini siku ya mwisho, mimi nimeishakuambia.