Trainee
JF-Expert Member
- Sep 22, 2018
- 3,118
- 4,238
Tunaona mara kwa mara operations za kuwaua baadhi ya viumbe hasa wanyama kwa sababu fulani fulani.
Sikatai uhai wa binadamu ni muhimu na unatangulizwa mbele (unapewa kipaumbele) dhidi ya uhai wa viumbe wengine
Lakini nashangaa na ninaona kama muda mwingine hatua inayochukuliwa ni ya juu mno dhidi ya viumbe hao
Sambamba na hilo najiuliza ni kwa nini hatua hizo zinachukuliwa kwa wanyama wa aina fulani tu huku wengine wakilelewa vizuri?
Inawezekana nimeandika bila kufunguka sasa ngoja ninyooke moja kwa moja ili nieleweke vizuri na kila msomaji
Fisi wawili wakipandwa na kichaa wakashambulia watu wawili watatu kijiji fulani tunaona maafisa wanyamapori wanaanza msako wa fisi
Msako unakuwa babkubwa na siyo kuwakusanya ili kuwapeleka maporini laa, bali kuwakusanya wakiwa mizoga yaani ni operation ya kuwaua
Tukio kama hilo hilo likitokea kwa tembo na faru utasikia au kuwaona maafisa wanyamapori wakifanya oparetion vile vile
Tofauti na ile ya fisi, operation hii utasikia wanawatawanya au kuwafukuzia tembo kuelekea kwenye maeneo yao ya hifadhi
Sasa huwa najiuliza sana kwanini simba, fisi, chui nk operation zao ni kuwaua lakini tembo, faru, nyati nk operation zao ni kuwafukuza tu?
Tena hii tabia imeambukizwa mpaka huku chini kwa sisi tusio na maafisa wanyamapori yaani ni kuua tu viumbe wa watu
Wataalamu wa wanyama najua mpo humu hebu nipeni elimu juu ya hili maana binafsi naona kama wanyama wengine wanaonewa sana