Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu Yiyu Sheping hebu rudi utujuze zaidi nimekua interesting sana na hizi habari,shusha vitu angalau nasi tupate mawili matatu.
Halipo, Tanzania hakuna wasomi.Mimi nadhani linaweza kuwepo na hata kama halipo bado mambo haya huwa ni top secret,kwani kwa dunia ya leo jinsi ilivyo ungekuta tumesha shambuliwa.
Yaani acha tu Mkuu, ni hovyo kabisa!Huku bado tcra wameshindwa hata kuzima simu feki achilia mbali kutengeneza websites za serikali!! Poor ccm
Huko ndo kujilinda sasa, sitashangaa Majeshi yetu yanatumia Windows 7 kwa mambo yake ya msingi.aisee wale jamaa inabidi tu tukubali wana akili za ajabu...........kwanza kule kwao wanatumia internet yao wenyew ambayo aiko connected na hii tunayotumia wengne kwahio hamna uwezekano kabisa wa kuwashambulia kimtandao wao wanashambulia tu wengine
Kama ni kweli basi tunaweza sema hii inchi ina matatizo mengi mazito tena ya kiroho.Mi naona uwezo tunao, hakuna linaloshindikana na watanzania tunauwezo mkubwa tu kiakili ila tukitqka kuwa fiti ni lazima mambo flani yabadilike, mifumo flani ibadilike na Serikali iamue kuwekeza kweli kweli ktk sayansi kuanzia ngazi ya awali na kuendelea. Siyo kwa ajili ya kupata watu wa cyber tu hatakupata wataalamu wengine ktk fani tofauti..
Hapa kwetu unakuta mtu anaunda kitu but anaweza pigwa marufuku na asiendelezwe wakati nchi za wenzetu mtu akionesha uwezo flani atasaidiwa kwa hali na mali...kwa mfano kuna mtu alitengeneza Helkopta mbeya naamin mlisikia kilichofata...nimewahi kukaa na mzee mmoja genius sana waisrael wenyewe walipobahatika kukaanaye walikubali (Mungu amrehemu huyu mzee kafariki mwaka jana) alikuwa anafanyakazi jeshini (engineer ) inasemekana aliwahi kutengeneza helkopta miaka ya 80, Alikuwa anauwezo kutengeneza bunduki, Aliwahi kutengeneza kinu cha kupukuchulia mahindi, ametengeneza madhine ya kutotolesha vifaranga nk...Je unaweza kuhisi mtu huyu alikuwa muhimu kwa kiwango gani endapo angewezeshwa na kutumika ktk Taifa.!?
Nachotaka kusema ni kwamba kilakitu kinawezekana ila uwekezaji lazima ufanyike na mifumo flani inayokwamisha watu kuonesha uwezo wao na kutokuwaendeleza, mifumo hii ibadilike
Aha ha ha ha ha ha ha ha!Wanajua kufwatilia chadema anafanya nini wapi wana mkutano baaasi!! Mengine hayawahusu na si kazi yao
Ebhana weeee, nipe elimu hapo kaka.zamani nchi ikishinda kwenye dog fight inaattain air superiority. kwenye cyber war unaweza tawala anga kwa kutumia kompyuta tu. ni vita mbaya kuliko tunavyodhani. mbaya zaidi hakuna rules of engagement. wamarekani walijiandaa na operation Nitro Zeus. ingetokea Israel wameivamia Iran. Marekani angeingilia kwa kuzima kila kitu.
Kama hauwezi kufikiri tofauti huwezi kuwa na jipya na utaendelea kuitumia vilivyotupwa na wenzio wanaofikira mpya kila uchao.Nilikuwa naangalia Documentary moja inaitwa Zero Days. inaelezea namna Marekani na washirika wake waliweza kushambulia mitambo ya nyuklia ya Iran kwa kutuma kirusi cha kompyuta (STUXnet). kirusi hicho kilisababisha mitambo ya Iran iwe inalipuka.
wairan wakajifunza kitu na kuamua kuunda jeshi lao la mtandaoni. moja ya kazi ilizofanya ni kushambulia mitandao ya benki za Marekani na mifumo ya umeme. Pia waliishambulia Uturuki na kuzima umeme nusu ya nchi kwa saa 12.
hii ni vita mbaya sana. inaweza zima umeme, mawasiliano ya simu, mitambo na ndege za kijeshi, mifumo ya maji safi na salama, traffic control, mifumo ya benki na fedha. kifupi nchi inaweza rudi stone age ndani ya dakika. Assume tushambuliwe kwenye mifumo yetu ya simu-pesa?
je Tanzania tuna jeshi la mtandaoni?
Mkuu kwa aina ya Elimu tegemezi tuliyo nayo na aina ya Wasomi niwaona kwa kada mbalimbali Viongozi wetu wa serikali ni ngumu kufikiri tunaweza fika hukoMkuu Tanzania watu wenye uwezo huo wapo wengi tu na tunaweza kua na jeshi imara sana la aina hiyo..
aisee ndio maana nchi zetu hizi ni ngum sana kujilinda hasa kwe cyber worldHuko ndo kujilinda sasa, sitashangaa Majeshi yetu yanatumia Windows 7 kwa mambo yake ya msingi.
Israel ilikuwa inatishia kutumia nguvu za kijeshi ili kuizuia Iran kutengeneza bomu la nyuklia. Marekani akaona Israel peke yake hawezi pambana na Iran hivyo atalazimika kumsaidia. Pia akaona kuwa itakuwa ngumu kwake kuvamia nchi ya tatu ya kiislamu, itamuharibia kidiplomasia. ndiyo wakaja na mpango Nitro Zeus.Ebhana weeee, nipe elimu hapo kaka.