Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Tunavyofahamu ni kuwa chombo cha habari cha TBC ni cha Watanzania wote na kinagharamiwa uendeshaji wake na kodi za wananchi wote, wana CCM na wana Chadema.
Kwa hiyo ni wajibu wa Mkurugenzi wa TBC, Ayoub Rioba, kuangalia ni kitu gani kina umuhimu mkubwa kwa Taifa na kukionyesha mubashara bila upendeleo wowote.
Vile vile Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya mwaka 1977, ibara ya 3(1( ) inatamka wazi kuwa "Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, itakuwa nchi ya kidemokrasia na ni ya mfumo wa vyama vingi" mwisho wa kunukuu.
Ndipo hapo ninapomuuliza Mkurugenzi wa TBC, ni kwanini waliamua kuonyesha tukio dogo la ufunguzi wa mahakama ya wilaya ya Chato na kuacha kuonyesha mubashara, tukio lenye umuhimu mkubwa kwa Taifa hili la mkutano mkuu wa chama kikuu cha upinzani nchini cha Chadema?
Tunajua pia TBC sio chombo cha habari cha CCM, na ni cha Taifa zima, kwa hiyo kufanya upendeleo kwa matukio yoyote ya ki-CCM ni makosa makubwa
Naomba mwenye kuelewa umuhimu wa TBC kuonyesha kila tukio analofanya Rais kwenye nchi hii lionyeshwe mubashara, na kutoweza kuonyesha matukio mengine yenye umuhumu mkubwa sana kwa Taifa hili aweze kunijibu.