Jamani kuna jambo linahitaji majibu ya wazi.
Mwaka jana TCRA waliifungia JamiiForums kwa takriban siku 90, wakisema ni adhabu. Sawa, adhabu ikaisha. Lakini mpaka leo, ili kuingia kwenye hii platform bado watu wengi wanalazimika kutumia VPN.
Swali langu ni hili: kama adhabu iliisha rasmi, kwanini access bado iwe ngumu kiasi hiki? Hii inamaanisha nini kwa uhuru wa kupata taarifa na kutoa maoni?
Inafika mahali wananchi tunajiuliza hivi mamlaka hizi zinajitazama kama nani ndani ya nchi? Kwa sababu kinachoonekana hapa sio tena udhibiti wa kawaida, bali ni kama kunyima watu haki yao ya msingi ya mawasiliano.
Teknolojia haiwezi kuzuiliwa kwa nguvu. Watu wataendelea kutafuta njia mbadala, kama hizi VPN mnazozifanya kuwa lazima. Lakini je, hii ndiyo taswira tunayojenga kama taifa kwenye ulimwengu wa kidijitali?
Ni muda wa uwazi na maelezo ya moja kwa moja. Wananchi wanahitaji kuelewa kinachoendelea, sio kulazimishwa kupita njia za pembeni ili tu wapate taarifa.
#UhuruWaHabari #DigitalFreedom #JamiiForums