Hivi tofauti kati ya utu na ubinadamu ni ipi?

Mtu ni binadamu aliechangamka!.

Hata ukiwa unasimuliwa kitu cha kutisha ukiambiwa Kuna binadamu hapo kwenye kona hata hushituki! Ila ambiwa Kuna mtu hapo kwenye kona! Kwanza moyo utaanza kwenda mbio! Utahisi na huyo mtu atakuwa kichwa chenye mapembe!.. ogopa sana huu usemi Moyo wa mtu ni kichaka!. 😂
 
Ubinadam ndio utu.... Ubinadam ni hali ya kumtendea mtu Sawa Sawa yaliyo mema nayakupendeza mfano kakosea, ni Kawaida ya binadam kukosea hivyo utafuta Madhaifu yake kwa kuangalia mapungufu kama binadam.... Utu ni ustaharabu.... Kutenda mema,, [emoji1787][emoji1787]

Ina changanya but utu ndio ubinadam

Utu una tokana na neno mtu na ubinadam una tokana na neno binadam [emoji1787][emoji1787]
 
Hapo inatakiwa ujue tofauti ya mtu na binadamu halafu ndo utajua tofauti ya utu na ubinadamu.

Kabda ya uzao wa Adam walikuwepo watu, na majitu hao watu na majitu wana utu.

Adam kaumbwa katika bustani ya Eden muda huo watu na majitu yalikuwepo kitaa.
Uzao wa Adam ndo binadamu, Hawa binadamu wanna ubinadamu.
 
Chanzo cha maneno haya ni;
Mtu » utu
Binadamu » ubinadamu
Yote yana maana moja kumaanisha USTAARABU NA HEKIMA kwasababu asiri ya mtu au binadamu ni MUNGU aliyetuumba na hekima na ustaarabu.
 
😂😂😂 sawa na kuambiwa bia na Serenge large vina utofauti gani😂 kuna vitu vingine muwe serious kidogo leo ni wikiendi mamaeeeee wakuu nimelewa sielew kitu ngati mnigana mbwelahi kunyumba
 
Chanzo cha maneno haya ni;
Mtu » utu
Binadamu » ubinadamu
Yote yana maana moja kumaanisha USTAARABU NA HEKIMA kwasababu asiri ya mtu au binadamu ni MUNGU aliyetuumba na hekima na ustaarabu.
Siyo kweli

Binadam linatokana na Bin-Adam yaani mtoto wa Adam kulingana na maandiko ya kimapokeo kutoka mataifa ya magharibi na Mtu linatokana na U-mntu yaani mtoto wa Mntu kulingana na asili ya Kibantu ya watu wa Afrika
 
Siyo kweli

Binadam linatokana na Bin-Adam yaani mtoto wa Adam kulingana na maandiko ya kimapokeo kutoka mataifa ya magharibi na Mtu linatokana na U-mntu yaani mtoto wa Mntu kulingana na asili ya Kibantu ya watu wa Afrika
Ndugu zangu Kadri mnavyozidi kunielezea ndio mnazidi kunichanganya😄
 
Utu ni hali ya kuwa na uungwana na matendo mema dhidi ya binadamu wenzako. Ubinaadamu ni hali ya ukiumbe yaani nafsi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…