Hivi tukiacha blaahblaah na porojo za kufarijiana kiimani, tukifa tunaenda wapi?⚰️⚰️

Kwahiyo kwenye mfuko wa uzazi kabla ya kuzaliwa ulikuwa mfu?
 
Tutaishi milele baada ya kukufa,maisha yasio ya mihanjo na iwapo tuu,tuliishi kwa kumwabudu na kumheshimu Mungu.
 
Sasa kwanini wasituamshe,kwani wameambiwa aliyelala anafurahia lift?
Huamshwi kwa sababu uwezi kuamka Tena tumesha waamsha Sana na hawakuamka mwisho wa siku wakatoa harufu ya kukera.
 
Dunia ina umri wa miaka mamilioni kadhaa. Achana nayo hayo tuanze walipoanza kuhesabu mpaka leo tuko mwaka 2024, tukichukua waliozaliwa kuanzia mwaka 0 mpaka 1800 kamili inawezekana wote hawapo duniani na wamekufa. Mi nadhani tukifa ndiyo kama alivyosema mdau mmoja huko juu kwamba kumbukumbu zinabaki kwa ndugu zako na watu wanaokufahamu na baada ya muda fulani hautakumbukwa popote kwa chochote. Tutendeni mema tu ili kuziridhisha nafsi ila hatuna cha kukitegemea baadaye. Ukifa ndo mwisho wako huo.
 
Hivi tukiacha blaahblaah na porojo za kufarijiana kiimani, tukifa tunaenda wapi?

Eti wakuu?
Hili swali aliwahi kuulizwa Yesu mara kadhaa, na mara ya mwisho aliulizwa akiwa msalabani na mharifu akiwa pale msalabani, na Yesu akamjibu pale pale.

Na kwa sisi wenye akili pana, tuna uhakika na jibu la Yesu kwa 100%. Kwanini? Yesu mbali na kulijibu kwa maneno tu (ambayo mtu mwingine yoyote angeweza kufanya) Yesu kipekee kabisa akalijibu kwa vitendo. Mwamba alisema atasubiriwa na kufa msalabani (na kweli akafa), akasema atafufuka(na kweli akafufuka) na mwisho akasema anapaa kwenda mbinguni (na kweli akapaa zake) huku akiahidi kurudi tena!

Jibu lake kuhusu kufa lilikuwa ni hili.
Heri wafu wafaao katika Bwana (Yesu) maana WATAPUMZIKA.
 
Unazaliwa bara lingine na jinsia tofauti.
Mi nakumbuka kabla sijafa na kuzaliwa bara jeusi, nilikuwa askari mwanamke mtiifu wa Adolf Hittler.

Ilikuwa tarehe 6June 1944 (D-Day), wakati majeshi wa Marekani wanatuvamia kupitia Omaha bay. Ambapo ilipewa code "Operation Overlord".
Ni story ndefu......
 
Labda Unarudi ulipokuwa kabla ya kuzaliwa 🐼
Hili jibu ambayo kidogo huenda,labda linaweza kukupa picha iwapo utajiuliza kabla hujazaliwa ulikuwa wapi?
 
Naweka kambi !

Ina maana watakatifu kina Ritha na wengineo hawapo ?

Au ni kila mtu ana maarifa yake juu ya anachokiamini
 
Tupa hapa hiyo story ndefu maisha ndio haya haya
 
Hivi tukiacha blaahblaah na porojo za kufarijiana kiimani, tukifa tunaenda wapi?

Eti wakuu?
Motoni milele vs uzima wa milele. Kuna njia mbili kubwa. 1.Njia pana, na mlango ni mpana waiendeayo ni wengi ndio hiyo iendayo motoni. 2.Njia nyembamba, na imesonga kwa kuwa imesonga waionayo ni wachache sana ndio njia iendayo uzimani. Yu karibu malangoni.
 
Motoni milele vs uzima wa milele. Kuna njia mbili kubwa. 1.Njia pana, na waiendeayo ni wengi ndio hiyo iendayo motoni. 2.Njia nyembamba, imesonga kwa kuwa imesonga waionayo ni wachache sana ndio njia iendayo uzimani. Yu karibu malangoni.
Hivi mkuu kwanini sisi huwa tuna vichwa vigumu hivi? Mleta mada kaweka wazi " Ukiachana na masuala ya imani"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…