Hivi tukiacha blaahblaah na porojo za kufarijiana kiimani, tukifa tunaenda wapi?⚰️⚰️

Hivi tukiacha blaahblaah na porojo za kufarijiana kiimani, tukifa tunaenda wapi?⚰️⚰️

Hivi tukiacha blaahblaah na porojo za kufarijiana kiimani, tukifa tunaenda wapi?

Eti wakuu?
safi sana. Haya maswali ni ya msingi sana. Hongera sana ndugu.

"Maswali makubwa maishani" ni yale maswali ya msingi ambayo yamewasumbua wanadamu kwa karne nyingi. Wanachunguza asili ya uwepo, maadili, na hali ya mwanadamu. Baadhi ya maswali makubwa ya kawaida ni pamoja na:
*Mimi ni nani? Swali hili linachunguza utambulisho wetu, madhumuni yetu, na nafasi yetu duniani.
*Kwa nini niko hapa? Swali hili linatafuta kuelewa maana na madhumuni ya maisha.
* Maana ya maisha ni nini? Swali hili linahusiana kwa karibu na la awali, lakini linazingatia umuhimu mkubwa wa kuwepo.
* Je, kuna Mungu au nguvu za juu zaidi? Swali hili linachunguza asili ya ulimwengu na kama kuna nguvu ya kimungu inayouongoza.
* Nini kinatokea baada ya kifo? Swali hili linaangazia asili ya kifo na nini kinaweza kuwa nyuma yake.
* Ni nini asili ya ukweli? Swali hili linachunguza asili ya msingi ya ulimwengu na mtazamo wetu juu yake.
* Ni nini asili ya fahamu? Swali hili linatafuta kuelewa asili ya akili zetu na jinsi tunavyopitia ulimwengu.
* Ni ipi njia sahihi ya kuishi? Swali hili linachunguza maadili, maadili, na njia bora ya kuishi maisha yenye kuridhisha.
* Ni nini asili ya wema na uovu? Swali hili linaangazia asili ya kimsingi ya maadili na kutofautisha kati ya mema na mabaya.
* Je, mustakabali wa ubinadamu ni upi? Swali hili linachunguza uwezo wa binadamu na changamoto tunazokabiliana nazo kama spishi.
Haya ni baadhi tu ya maswali mengi makubwa ambayo yamefikiriwa na wanafalsafa, wanatheolojia, na wanasayansi katika historia yote. Ingawa kunaweza kusiwe na majibu ya uhakika kwa maswali haya yote, kuyachunguza kunaweza kutusaidia kupata ufahamu wa kina zaidi wetu na ulimwengu unaotuzunguka.
 
Hivi mkuu kwanini sisi huwa tuna vichwa vigumu hivi? Mleta mada kaweka wazi " Ukiachana na masuala ya imani"
Kwani ulishaona Mtz mwenye kichwa chepesi?Ingekuwa wapo wenye vichwa vyepesi tungekuwa mbali mnooo
 
  • Kicheko
Reactions: Tsh
Kuwaza kwamba ukifa kuna sehemu unaenda nazo ni blah! blah! Tu
 
Hili swali aliwahi kuulizwa Yesu mara kadhaa, na mara ya mwisho aliulizwa akiwa msalabani na mharifu akiwa pale msalabani, na Yesu akamjibu pale pale.

Na kwa sisi wenye akili pana, tuna uhakika na jibu la Yesu kwa 100%. Kwanini? Yesu mbali na kulijibu kwa maneno tu (ambayo mtu mwingine yoyote angeweza kufanya) Yesu kipekee kabisa akalijibu kwa vitendo. Mwamba alisema atasubiriwa na kufa msalabani (na kweli akafa), akasema atafufuka(na kweli akafufuka) na mwisho akasema anapaa kwenda mbinguni (na kweli akapaa zake) huku akiahidi kurudi tena!

Jibu lake kuhusu kufa lilikuwa ni hili.
Heri wafu wafaao katika Bwana (Yesu) maana WATAPUMZIKA.
Mjinga huyu, anauliza swali halafu anaweka mipaka ya majibu ati POROJO ZA KIIMANI. Biblia inasema kuwa Yesu ni kila kitu. Asante mkuu kwa jibu la uhakika.
 
Wanao kufa mazima ni watu waishio chini ya kivuli cha uovu, wanao ishi kwa kumtumainia mwenyezi Mungu wanalo tumaini la kuishi hata wakifa,

Hapa hakuna maisha ya baadae ya watenda maovu, maisha ya baadae ni ya watu waishio katika nuru , yaani walio kubaliwa na Mungu tu.

Wengine safari yenu inaishia kaburini.

Labda mjifariji na maneno ya kama hakuna mungu, na ukifa umekufa na blah blah zingine za watu wanao ipenda dunia hata kufikia kukataa kufa.
 
Hivi tukiacha blaahblaah na porojo za kufarijiana kiimani, tukifa tunaenda wapi?

Eti wakuu?
Wakati upo tumboni mwa mama yako, ulikuwa unajua upo wapi na unaenda wapi?
Ikiwa hujaambiwa kama ulikuwa ndani ya tumbo la mama usingeweza kusadiki, habari za baada ya kifo utazipata katika maandiko ya dini na si kwengineko ambapo wewe umeshayafungia mlango na kuita blaahblaah na pororjo za kufarijiana kiimani, hutopata jibu mpaka ufe ndiyo utakapokuwa na uhakika wa wapi umekwenda. Usisikie la kuambiwa mpaka uone mwenyewe. Subiri ufe wangu ndiyo utaona wapi unakwenda.
 
Hili swali aliwahi kuulizwa Yesu mara kadhaa, na mara ya mwisho aliulizwa akiwa msalabani na mharifu akiwa pale msalabani, na Yesu akamjibu pale pale.

Na kwa sisi wenye akili pana, tuna uhakika na jibu la Yesu kwa 100%. Kwanini? Yesu mbali na kulijibu kwa maneno tu (ambayo mtu mwingine yoyote angeweza kufanya) Yesu kipekee kabisa akalijibu kwa vitendo. Mwamba alisema atasubiriwa na kufa msalabani (na kweli akafa), akasema atafufuka(na kweli akafufuka) na mwisho akasema anapaa kwenda mbinguni (na kweli akapaa zake) huku akiahidi kurudi tena!

Jibu lake kuhusu kufa lilikuwa ni hili.
Heri wafu wafaao katika Bwana (Yesu) maana WATAPUMZIKA.
Na Mlivyo Na Fikra Sahihi Mnasubiri Arudi Awachukue Nyie Wake Mlio Wema Mpae Mbinguni Mkaketi Mkono Wa Kuume Kwa Baba Pamoja Nae Huku Mkisifu Na Kuimba....Ngoja Tuwaache Nyie Msubirio Sisi Twatangulia
 
Hivi tukiacha blaahblaah na porojo za kufarijiana kiimani, tukifa tunaenda wapi?

Eti wakuu?
Hatuendi mahali Kwa sababu "kwenda" kuna maanisha "movement" ambayo ni chacteristic of living things. Hivyo, a dead thing cannot move.
 
Back
Top Bottom