Pre GE2025 Hivi Tundu Lissu ni mtu wa aina gani?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

kyagata

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2016
Posts
10,406
Reaction score
19,892
Huyu mtu bwana hana shukrani,

Yeye mwenyewe kwa kinywa chake aliwahi kukiri kuwa yeye na Magufuli waliwahi kuwa marafiki wazuri tu siku za huko nyuma na kuna majina yao ya utani nimeyasahau walikua wanaitana.

Mara ghafla Magufuli alivyokua Rais Lissu akaanza uchokozi wa kumtukana Magufuli bila sababu za msingi.

Kilichotokea mimi na wewe msomaji tunakijua ila aliyemfanyia hayo madhira Lissu sio Magufuli kama ambavyo Lissu amekua akimaintain mpaka leo.

Then Mbowe na Viongozi wenzake wa CHADEMA kwa moyo mkunjufu na wa upendo walifanya kila liwezekanalo kuhakikisha Lissu anapata matibabu kwa haraka na kwa gharama yoyote ili kuokoa maisha yake.

Lakini leo Lissu huyu huyu anatumika kumchafua mheshimiwa Mbowe.

Daktari Samia alipoteza muda wake kwenda kumjulia hali Lissu pale Nairobi hospital, lakini leo Mama yetu huyu kipenzi nae anaoga matusi kila siku kutoka kwa huyu mtu.

Hivi huyu Lissu ni mtu wa aina gani asiye na shukrani kwa watu wanaomsaidia?
 
shinikizo la mabwenyenye ya magharibi yaliyomfanya awe kibaraka wao, ndiyo hasa limemfanya awe na tamaa, mdomo na makelele kama alivyo.

wamemwambia lazima awe mwenyekiti wa chama cha siasa, ili wakimtumia kitu pesa kupitia NGOs zao humu nchini, mlungula umfikie yeye mwenyewe kama mwenyekiti wa chama na sio mtu mwingine.

ndio maana ana mawenge,
leo anatangaza kugombea umakamu mwenyekiti, kesho anabadili anataka kugombea uenyekiti Taifa
 
Huyu mtu tumkatae
 
Huyu mtu tumkatae
ni wazi hafai kabisa pale chadema na kwingineko nchini,

nadhani wajumbe wa mkutano mkuu wa chadema taifa, wamejipanga vizuri sana, watamkataa na watamziba mdomo na makelele yake kwa uhuru, haki na uwazi Jan.22,2025, ili iwe fundisho kwa wenye tabia za midomo kama hizo
 
Lisu ndo m/kiti wa chama
 
Unashindwa kutofautisha urafiki, staha, fadhila na HAKI.... LISSU ANAJUA HAKI ZAKE , HAOMBI FADHILA
 
Huyu mtu tumkatae
Mkuu kuna shida gani akilini mwako?
1. Lissu na Magufuli hawakuwa na ugomvi bali Lissu alikuwa na ugomvi na urais wa Magufuli..Urais ni taasisi siyo kama unavyowaza wewe.
2. Lissu na Samia hawana ugomvi ila anaugomvi na urais wa Samia, Urais ni taasisi.
3. Lissu hana ugomvi na Mbowe na viongozi wengine wa CHADEMA, bali Lissu anagombea cheo cha uenyekiti wa CHADEMA kama ilivyo kwenye katiba ya CHADEMA.
Hivyo punguza ujuaji ya kuona mtu akitoa maoni au kutafuta nafasi iliyotangazwa kumchukulia kuwa anaugomvi binafsi.
 
Ni mtu ambaye hana unafiki kama mlivyo watanzania wengi. Kisa mimi na wewe ni marafiki nikikosea badala ya kusema ukweli husemi kisa tu ni rafiki yako au niliwahi kukupa 500 ukiwa na kiu.
Watanzania mnataka watu wasema kweli au wanafiki wanaolindana kisa urafiki, undugu, uchama?
 
Shida lissu mpenda haki sana na hii nchi waliopo juu hawataki mambo ya haki
 
Nyuzi joto/boiling point ikiongezeka zaidi, inapelekea maharage yachezecheze zaidi(mayowe makelele zaidi n.k) mwishowe yanaiva......
 
Kuna tofauti kati ya mambo binafsi na mambo ya kazini/ ya uongozi wa nchi.

Tundu Lissu anaelewa tofauti hiyo.

Wewe huelewi.
 
Aliyempiga risasi Lissu atakuwa anafahamika na hayati Magufuli.
 
Kilichotokea mimi na wewe msomaji tunakijua ila aliyemfanyia hayo madhira Lissu sio Magufuli kama ambavyo Lissu amekua akimaintain mpaka leo.
Kama sio magufuli ni Nani?

Unataka tuamini unachosema, wewe ni nani?.

Ujinga tu.
 
Acha chuki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…