Hivi uchoyo/ubinafsi unafaida gani katika maisha yako ya duniani hapa

Haaaaaaaaaaaaaaaa umenikumbusha jirani yangu mmoja hapa... Amekuja kuwekeza samaki kwangu..


Ana wageni masela wenzake. Mboga naona ni dagaa maharage tangu wafike dah Nimeshangaa sana


Mahondaw wa Smart911
Super dear... Actually huyo jirani yako ana roho ya ki-maskini...

Au wanasema..

Maskini akipata...
 
Hatari Sana. Mama wa nyumba anaweka vitu vya kupika chumbani kwake, sasa uone anavyomgombeza dada wa kazi kwa matumizi Mabaya! Mama anawaka vitu vidogo hadi kero. Kwakweli hii tabia inaudhi
Sasa hio ni akili gani, kama friji ipo mtu anaweka vitu rum vikaozea huko dah..Au mtu akienda kazini anaficha jiko ili mliobaki msipike.Uchoyo sio kitu chema jamani!!!
 
Ndio wabongo walivyo, ila wengi wenye tabia hii ni malimbukeni wa maisha, wale watu wamepata maisha mazuri ghafla bila kutegemea. Naamini kama umekulia kwenye maisha huwezi kuwa mjinga mjinga hivi huku ukinyanyasa watu na roho za kimaskini.
 
Hauna faida yeyote basi tu ni roho ya mtu ilivyo mbaya au utakuta mwanamke kaolewa ndugu wa mume wakija mwendo wa maharage tu na dagaa mpaka waondoke
Hio kitu nmeshuhudia katika ukuaji wangu kwa aunt yangu flanii..kina bamdogo wamekula sana arage na kabichi wakati kuna ma kilo ya nyama frijini
 
MI nadhani watu wengi wa hivyo ni wale waliopata Mali kwa shida sana hvyo wanapenda na ww usote, hivi huoni hata mashuleni ukikuta teacher mnoko sana ukifuatilia utangundua alisoma kwa shida na tabu sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkuu hama tu kwa shemeji ukajitegemee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hawa wat wapo hta maji ya kunywa unanyimwa.uchoyo haufai wakuu

Sent using Jamii Forums mobile app from my Android phone
 
hahahaha na watu wa kanda maalumu mkiendaga kusalimia hamfikirii kurud kwenu mapema haahah! kama nakuona kakangu! ila ni roho ya ajabu alafu inakera sana jaman!
Hahahaha dadake Mbitiyaza siyo hivyo, bali nilikuwa niko chuo hapa hapa Dar na mjomba yuko hapa hapa Dar, sasa ikifika muda wa kufunga chuo wakati mwingine nilikuwa naona tabu sana kutoka Dar hadi mkoani, hivyo naamua kubaki hapa hapa mjini kuokoa gharama ya nauli ya safari na mahitaji mengineyo yahusuyo safari, uzuri ni kwamba siyo muda wote nilikuwa namaliza muda wangu kwake wa mapumziko
 
hahahaha na watu wa kanda maalumu mkiendaga kusalimia hamfikirii kurud kwenu mapema haahah! kama nakuona kakangu! ila ni roho ya ajabu alafu inakera sana jaman!
Dadake kwa uroho mbaya kwa vitu vidogo vidogo tu mko vizuri aisee!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…