Hivi uchoyo/ubinafsi unafaida gani katika maisha yako ya duniani hapa

Hauna faida yeyote basi tu ni roho ya mtu ilivyo mbaya au utakuta mwanamke kaolewa ndugu wa mume wakija mwendo wa maharage tu na dagaa mpaka waondoke
Mtu akitaka kunifukuza kwa maharage na dagaa anajisumbua.....hizo ni mboga favorites zangu....vyovyote utakavyopika bora usiniwekee mchanga tu...[emoji2][emoji2][emoji2]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wengi wa watu wa namna hii mwisho wao huwa msongo wa mawazo na magonjwa ya moyo. Roho mbaya ni sumu inayoanza na mhusika mwenyewe siku zote.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna mamaangu mkubwa huwa akiniona nilipo sasa kimaisha haamini kiasi kwamba analiaga tu, alinisumbua sana kipindi cha ukuaji wangu!
 
Nadhani we ni mmojawapo mwenye tabia ya kipuuzi ukidhani ni sifa. Ishi na watu vizuri wewe...
Kila mtu apambane na hali yake, sifugi watu nafuga mifugo au ndege kwa faida, unataka kustarehe kwa jasho langu? Utajifunza lini kutafuta maisha? Kama unataka vya bure zipo sehemu mahsusi, unakula unaliwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndy madhara ya kukaa na KAKA...PAMBANA NA HALI YAKO....sidhani km hivyo Vitu vyote ANAFICHIWA MTOTO MDOGO...ni MIJITU NA MIDEVU YAO.....akikaa kwnye TV kuanzia alfajiri hadi SAA NNE za USIKU...ukiweka JUICE AU MATUNDA kwa Fridge WATU wanashindana KUMENYA MACHUNGWA TU na kutupa MAGANDA YA NDIZI...kwann SHEMEJI asifiche VITU?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zaidi ya mara moja nmeshashuhudia mpita njia anapewa maji ya bomba makusudi. Ilihali ya kuchemshwa yapo, ila ukionekana umempa tu ni msala!
kwel mkuu watu wa aina hyo wapo sana

Sent from my Android phone
 
NA WATU WANYE ROHO MBAYA/UCHOYO/UBINAFSI, AFYA ZAO HUWA MGOGORO.. HAWANAWIRI, WANAKONDA MPAKA UNASHANGAA

NAMSHUKURU MUNGU KWA KIASI KIKUBWA SINA HZO MAMBO NA NINAOMBA MKE NTAKAYEMWOA AWE NA ROHO NZURI
Wala usidhani ni waliokonda pekee ndo wenye hizo roho...wengine wanene haswaaa...afya nzuri...na bado wachoyoooooo! Wana gubuuu....wana wasimanga watu waliomo majumbani mwao!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kukaa kwa mashemeji au mawifi hakujawahi kumwacha mtu salama...
Maisha ni magum sawa ila mtu ukijitegemea kwa kujituma kufanya kaz hata ya kubeba zege ni salama zaid kuliko kukaa na kumtegemea ndugu...Maisha ya manyanyaso kutoka kwa ndugu ndiyo yaliyosababisha niweke degree yangu pembeni na kuanza kubeba zege ambapo nlipata mtaji kupitia kaz hyo na kufanya mambo mengine....
 



Tupatie mrejesho je huyo MTU anaendeleaje ?

Uchoyo ni kitu kibaya.
 
Kazi mnayo
 
Imagine mtu anaitwa Angel halafu anakuwa mchoyo.??
Sasa si ungeitwa devil tujue moja.!!
 

TAFUTA VITU VYAKO ACHANA NA VITU VYA WATU
 
Umeongea ukweli na haya matukio kwa watu ambao wamepitia Maisha ya hama hama na kuishi na ndugu au watu baki ni lazima utakuta wamekutana nayo.

Kimsingi hizi tabia watu wengi hujifunzia tokea utotoni na wachache sana hujifunzia ukubwani.

Ni matokeo ya kuwa na fikra za hofu ya kupoteza. Imagine mtu anawaza utakula matunda as if yalinunuliwa ili yatazamwe. Kama watu wanakula sana vilivyomo kwenye friji, dawa sio kulifunga maana ndio utawapa hamu zaidi, dawa ni kununua matunda mengi zaidi ili kila mtu atosheke.

Mara nyingi watu wa namna hii walilelewa na wazazi au walezi ambao waliwafunza kuwa maisha ni kujitetea pekee yako na kutojali wengine nyakati za uhaba na matokeo yake wamejijengea tabia za kupenda kujitetea wenyewe na kutojali wenzao.

Kuna shangazi yangu huyo, miaka hii ameshazeeka, hakuna mtu anaeenda kwake kwanza nyumba nzuri kubwa inavyumba vya kulala vitano ila hakunaga wageni wala watu wanaotaka kwenda ishi nae sababu ya tabia kama hizi ulizoweka hapa.

Enzi zake alikuwa anafanya kazi kwenye NGO's za kishua na alikuwa na mtonyo ila huwezi amini alikuwa na roho ya kukunja mbaya. Ukihadithiwa matukio yake utasema wanamtungia nenda kakae kwake wiki tu utaona. Hivi vitu umesema hapa nimehisi pengine ulishawahi kuishi kwake.
 
Roho kushikana na vitu.
 
Mbona unani attack, aliekwambia sina vyangu ni nani mkuu?
Watu wa hivi inabidi uwavumilie sana. Hii ndio sampuli ya watu ambao hata wakienda msalani hawa mwagi maji choo kinakuwa na hali ya kukwaza watakaotumia baadae so msamehe bure tu. Wewe unaelezea tatizo yeye anakuja kukulaumu kama ng'ombe anayetafuta majani haaachi kuwapigia kelele wapita njia. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Bwege kabisa huyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…