jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 26,540
- 25,834
Hakuna ubishi kwamba kilimo ndo kimekuwa nguzo kuu ya uchumi wa Tanzania, ambapo kilimo kinachangia 24.5% kwenye GDP.
Kilimo kinachangia asilimia 85 kwenye total export, na pia nusu ya waajiriwa wote wanatokea kwenye sekta ya kilimo, kwa mujibu wa data zilizopo mitandaoni. Lakini kwenye uchumi wetu kwa ujumla, sekta nyingine zaidi ya Kilimo, kuna utalii, uvuvi, madini, misitu, nyuki, nishati na “uzalishaji”
“The main sectors are agriculture, tourism, fishing, forestry and beekeeping, mining, manufacturing and the energy industries. Agriculture – plays an important economic role as it employs 75% of the population.“
Sasa kilimo ndicho kina ajiri asilimia 75 za wananchi wa Tanzania! Sasa ukitizama kwa makini, utaona kwamba ilikuwa ni ujinga kuiogopa corona na kudai tuombe Mungu ataizuia. Tukaikuza na kuijengea mazingira rafiki ya kusambaa zaidi makanisani na misikitini kwa kuagiza mikusanyiko ya kuomba dhidi ya gonjwa linalosambaa kutokana na mikusanyiko!, na wakati tulikuwa na nafasi kubwa na nzuri kabisa ya kujifunza kutoka kwa wenzetu. Lakini badala ya utaalam, zikaingizwa siasa.
Jiji la Dar siyo siri ndo kitovu cha gonjwa hili. Lakini sababu zilizotolewa kuhusu katazo la lockdown, hazikuwa na mantiki, kwasababu kwanza hatukuwa na ulazima wa total lockdown!
Pili, kusema eti “Kwani watu wa Dar hawataki viazi”, ama watu wa mikoani “hawataki vitenge”, siyo kauli zenye kuonyesha weledi kwenye janga linalotukabili.
Kuhakikisha sekta ya usafirishaji, haswa kutoka na kuingia Dar ikiwemo mizigo na abiria, inakuwa monitered ili kupunguza maambukizi, kama wanavyofanya wenzetu (Uganda, Zambia, Rwanda etc), kwenye borders zao wakati wanapokea mizigo kutoka kwetu pamoja na raia. Sisi tuliacha kila kitu wazi. Hata mipaka haikufungwa, bali ilijifunga yenyewe tu kutokana na majirani kufunga mipaka yao. Kwenye anga ni hivyo hivyo.
Pia, kama tunategemea Kilimo, kwetu sisi ilikuwa rahisi sana kuhakikisha kuwa sekta hiyo haswa upande wa usafirishaji, inakuwa monitored na hatua zote stahiki zinachukuliwa ikiwa ni pamoja na kuwapima madereva, pamoja na wafanyakazi wote walioko kwenye sekta ya kilimo na usafirishaji wa bidhaa zake. Kuhakikisha maelekezo ya wataalam wa afya yanafuatwa.
Chloride inasaidia kwasababu yenyewe haina tofauti na bleach. Lakini ilizuiliwa na mwanzoni niliona baadhi ya viongozi kaka Mama Mughirwa wakifanya jitihada ambazo zilitakiwa kuendelezwa siyo tu kwenye mabasi, bali hata vyombo vya usafiri vinavyoingia na kutoka Dar.
Lakini sababu inayotolewa kuwa watu watakufa njaa haina mashiko. Madhumuni haswa ya lockdowns, ni kuhakikisha ni ya muda mfupi(mara nyingi siku 14), kwenye eneo athirika (tulikuwa na nafasi hii kuliko wenzetu). Lakini tulizembea mwanzoni tukidhani ni gonjwa la wazungu tu hilo. Au “kakolona!” Au “tumafua tu!”
Lengo la lockdown, pale inapowahiwa mwanzoni kabisa, ni kwamba inakuwa ni eneo dogo. Mfano Dar ni kubwa. Lakini wagonjwa hawakusambaa jiji zima kwa wakati mmoja. Wagonjwa waliopatikana mwanzoni kabisa, kungewekwa lockdown ya eneo hilo husika kwa siku 14, huku kukiwa na juhudi za usiku na mchana za tressing pamoja na isolation, yani kuwatafuta watu walio kutakana na waathirika hao. Ni rahisi kuwapata mapema kabla hawajausambaza kwenye kipindi ambacho hawaruhusiwi kutembea. Maana kwa kipindi hicho cha siku 14, wale walioambukizwa, wengi wao dalili tayari zinakuwa wazi.
Na hivyo kwa kipindi hicho, kazi ya tressing ama utafutaji na ufuatiliaji wa wale waliokutana na waathirika inakuwa siyo kubwa na kwasababu wako ndani, wanakuwa hawasambazi, na baada ya kupatikana, wanahudumiwa na baada ya hapo lockdown ya eneo husika inaondolewa kwa tahadhari. Kwasasa tumeshachelewa kwa kiasi kikubwa. Lakini ni muhimu hatua zikachukuliwa, kabla janga halijatapakaa huko vijijini ambapo ndipo kwenye ugali wa nchi!
Nasema “kwenye ugali wa nchi”...Sasa je? kama uchumi wetu unaendeshwa na mkulima, kwanini hatuchukui hatua stahiki kumlinda? Wakulima wanawalisha wale wanaobwatuka huko mjini! Lakini hawajui madhara yake ya ubwatukaji huo. Mwishowe, ugonjwa ukifika vijijini uchumi unaanguka chali! Ama viongozi wanadhani Dar inaendeshwa na nani kiuchumi? Eti watu kurandaranda Dar ndo nguzo ya uchumi?
Taifa la Marekani lina “mixed economy”, ila linategemea viwanda sana kwenye livelihood yake. Mfano viwanda vya vyakula, vimekuwa na maambukizi sana. Kiwanda kikubwa kabisa cha nyama kinachoitwa Tyson’s, kimeanza kufilisika kwasababu hiyo. Hawakuweka wala kuchukuwa hatua na tahadhari. Wengi wanaofanya kazi humo ni immigrants na minorities, wengi wameambukizwa na kupelekea viwanda kufungwa na hivyo kusababisha upatikanaji hafifu wa chakula kwenye supermarkets.
“Supply and demand are the forces that drive the U.S. economy. Supply includes labor, represented by employment, and natural resources, such as oil, land, and water. Oil prices drive 70% of the cost of gas. Demand, or personal consumption drives almost 70% of the economy.”
Kwajinsi uchumi wa marekani ulivyo, ni wazi kwamba unaendeshwa na labors. Watu wasiolipwa mishahara ya maana. Watu ambao ni kama wanalitumikia tabaka moja ambalo kwasasa linahisi kuanza kuikosa ile privilege waliyokuwa nayo ya kutumikiwa.
Watu wa chini na tabaka la chini ndiyo nguzo ya uchumi wa marekani. Hata nchi ama uchumi ukifunguliwa, wao ndiyo wako kwenye hatari zaidi ya maambukizi.
Ni tabaka dogo lenye wafuasi wasiojitambuwa ndiyo wenye kuona kwamba hatua zilizochukuliwa, na zinazoendelea kuchukuliwa, hazikusaidia na wala hazitasaidia kupunguza idadi ya vifo na pengine uchumi kuanguka moja kwa moja.
Without lockdown across the world coronavirus would have killed 40 million, experts say
Kama ilivyo kwa hawa oligarchies wa marekani pamoja na minions wao, kuna uwezekano kuwa kama kuna kitu kitatupa shida na sisi kama Taifa ni matabaka. Kuna wakusanyaji, wapangaji na watumiaji wa kodi zetu (wakati mwingine kibabe). Hawa wamekuwa na tabia ya kutokujali maisha ya watu wala kuona kwamba yana umuhimu! Wao starehe yao imo kwenye kodi wanazokusanya, na vitu wanavyoviona bila kujali gharama zake. Kama vile ambavyo kuna hao wazungu wanaokaa mezani kula “fillet mignon”, bila kujuwa zinafika mezani kwa style gani. Hao ni wale wasiotambuwa kuwa privileges zao zinatokana na sacrifices za kila aina kutoka kwenye matabaka ya chini, na hivyo hawaoni umuhimu wao!
Sasa hatua ambazo ilikuwa tuzichukuwe sisi dhidi ya jiji letu la Dar, ndizo hatua wanazozichukuwa majirani zetu dhidi ya Taifa letu. Sasa maamuzi yaliyofanywa ni sahihi? Charity begins at home!
Kama uchumi wetu unaendeshwa na mkulima, hizo nyingine zilikuwa blah blah na kupanic kwa kukosa plan.