Hivi uchumi wa Tanzania unaendeshwa na nani?

Hivi uchumi wa Tanzania unaendeshwa na nani?

Mwanzoni kabisa niliandika humu na kuonya kuhusu hilo la kutengwa. Sasa bado kwenye utalii. Ubishi mwingine haufai.
Kweli kabisa itachukua muda sana watalii kuja kwani watakuwa na maswali wa sintofahamu kuhusiana na mazingira mapya ya Corona.
 
Kweli kabisa itachukua muda sana watalii kuja kwani watakuwa na maswali wa sintofahamu kuhusiana na mazingira mapya ya Corona
Watasubiri hadi herd immunity imalize kazi yake. Na hapo inategemea na watu kujitoa muhanga na kuchapa kazi. Hilo likichukuwa muda sana uchumi utaharibika zaidi.
 
Kweli kabisa itachukua muda sana watalii kuja kwani watakuwa na maswali wa sintofahamu kuhusiana na mazingira mapya ya Corona

Corona imeletwa na hao hao watalii sasa sisi Watanzania kwa nini tuwe na wasi wasi. Swala ni kujikinga tu, kuna maradhi mengi tu watu wanakufa kila siku. Pengine ni vyema tungepata statistics za kila mtu anayekufa anakufa kwa ugonjwa gani then tufanye comparison.
 
Asante sana kwa hoja mujarab, japo uchumi wa Tanzania unakuwa kwa asilimia 7% GDP na unategemea kilimo na unaendeshwa na wakulima, lakini mchango wa sekta ya kilimo katika ukuaji huo wa uchumi ni chini ya asilimia 2% ya GDP, hii maanale asilimia 80% ya Watanzania wanaotegemea kilimo ndio wanagawana umasikini wa less than 2% ya GDP, halafu alisimia 20 ya waliobaki ndio wanafaidi huo ukuaji wa asilimia 5%, tungefanya lockdown, ambao wange suffers most ni wale masikini asilimia 80%, wanaochangia 2% ya uchumi wetu, huku wale matajiri wa 5% ndio wana uchumi wa kuwawezesha kuhimili lockdown.

Hivyo rais Magufuli kugomea lockdown downtown amefanya the right thing.

Japo watu wanakufa kwa Corona,wote wanaokufa ni watu wa lile kundi la matajiri.

Uchumi wa Magufuli: Sekta Binafsi ina-Suffer. Yalianza Maduka, Yakafuata Mashirika, Sasa ni Zamu ya Media Ina-suffer! - JamiiForums
P
Naunga mkono hoja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maghufuli hayuko sahihi kwasababu zifuatazo...

1. hatukuwa na zuiyo lolote mipakani na wageni walikuwa wanaingia kama kawaida. Kiukweli lockdown inatakiwa iwe ya muda mfupi na haraka sana mara baada ya mgonjwa ama wagonjwa wa awali kugundulika. Na ndiyo maana inatakiwa kuwa siku 14 kwasababu kupindi hicho ndo ambacho mtu mwathirika anaweza kuona dalili za covid-19. Na kwasababu ndani ya siku hizo 14 hakuna wenye kutembea tembea, ina maambukizi yanakuwa yamesitishwa. Sasa hapo ndo usiku na mchana kuwatafuta wale wote walokutana na waathirika hao. Kwahizo siku 14 wengi tayari watakuwa wameshaanza kuwa na dalili. Wale wasiokuwa nazo lazima wapimwe incase ni asymptomatic.

2. Uchumi wetu unategemea kilimo, tunamlinda mkulima kuanzia Dar kwasababu ndo anayetulisha. Huo uchumi unaoutaja ni wakifisadi kama ni kweli kilimo kinachangia asilimia mbili tu ya GDP. Taarifa hii umeitoa wapi?

Nadhani wengi wenu mko kwenye hoja za kisiasa zaidi ndo maana mnazungumza “blanket statements” mfano “Maghufuli kugomea lockdown amefanya the right thing”

Ugonjwa ukisambaa vijijini Dar mtakula wapi?
Usihangaike na mayala anatafuta uteuzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Corona imeletwa na hao hao watalii sasa sisi Watanzania kwa nini tuwe na wasi wasi. Swala ni kujikinga tu, kuna maradhi mengi tu watu wanakufa kila siku. Pengine ni vyema tungepata statistics za kila mtu anayekufa anakufa kwa ugonjwa gani then tufanye comparison.
Hayo magonjwa mengine sio hatari kama Corona ambalo mpaka sasa hakuna kinga ,dwa wala chanjo. Usiwe mjinga wewe ugonjwa umekatwa na mtalii ,mtanzania au myama lazima tahadhari zichukuliwe na mipango dhabiti na endelevu iwekwe wazi ili kila mtu ajikinge,ajiangalie baadaye tuendelee na kazi zetu kama kawaida.

Statistics za magonjwa mengine zipo kwenye system ya serikali inaitwa MTUA 1 utapata za Ukimwi na related diseases nk takwimu zote za magonjwa mengine zipo .

Ndio maana ulienda hospitali kwa daktari au basi kwenye hospital yoyote kuna likitabu likubwa kila mwezi kila taarifa za.mgonjwa na magonjwa zipo kwenye database ya serikali.Ukitaka kujua ni wangapi wamepimwa malaria,wakutwa positive ,wamekufa nk
 
Hayo magonjwa mengine sio hatari kama Corona ambalo mpaka sasa hakuna kinga ,dwa wala chanjo. Usiwe mjinga wewe ugonjwa umekatwa na mtalii ,mtanzania au myama lazima tahadhari zichukuliwe na mipango dhabiti na endelevu iwekwe wazi ili kila mtu ajikinge,ajiangalie baadaye tuendelee na kazi zetu kama kawaida.Statistics za magonjwa mengine zipo kwenye system ya serikali inaitwa MTUA 1 utapata za Ukimwi na related diseases nk takwimu zote za magonjwa mengine zipo .Ndio maana ulienda hospitali kwa daktari au basi kwenye hospital yoyote kuna likitabu likubwa kila mwezi kila taarifa za.mgonjwa na magonjwa zipo kwenye database ya serikali.Ukitaka kujua ni wangapi wamepimwa malaria,wakutwa positive ,wamekufa nk

Just to put it clearly, ugonjwa wowote ni hatari na unaua. Covid-19 uzuri wake njia za kujikinga zipo, kama unafuata njia za kujikinga hakuna tatizo, hizo stats nimeziongelea ukilinganisha na idadi ya Watanzania waliokufa hadi hivi sasa hata hypothetically ukaweka 10,000 bado sana ukilinganisha na idadi ya Watanzania wanaokufa kwa magonjwa mengine. Sijasema hatua tusizichukue kujilinda lakini hakuna sababu yoyote ya kuweka taharuki kwa jamii.

USA mbona wanaanza kuondoa lockdown wakati bado hakuna dawa? We must be realistic with our situation bila kufuata ulimbukeni. FYI Germany figures zao zimeanza kupanda baada ya kuondoa hiyo lockdown waliyokuwa wameweka. Wakimaliza ujinga wao sisi watatukuta pale pale.
 
Kama hatua za kuzuia maambukizi yasiendelee kwa kasi, mwishowe unategemea iweje?

Manacheza sadakalawe na maisha ya watu! Yani mwenye kupata apate na mwenye kukosa akose?

Kwa taarifa yako, unafiki uatawamaliza, hata Trump anataka watu watoke ndani lakini wamegoma! Lockdowns zinaondolewa lakini watu wamegoma, pamoja na kusema kuwa watanyimwa unemployment kama wakikataa kwenda kazini kwasababu ya corona.

Watu wanataka solutions na siyo blah blah.
 
Corona imeletwa na hao hao watalii sasa sisi Watanzania kwa nini tuwe na wasi wasi. Swala ni kujikinga tu, kuna maradhi mengi tu watu wanakufa kila siku. Pengine ni vyema tungepata statistics za kila mtu anayekufa anakufa kwa ugonjwa gani then tufanye comparison.
“Corona imeletwa na watalii” ni kauli mbovu kabisa!

Ililetwa lini? Mgonjwa wa kwanza alipatikana wapi? Hatua gani zilichukuliwa?
 
Hayo magonjwa mengine sio hatari kama Corona ambalo mpaka sasa hakuna kinga ,dwa wala chanjo. Usiwe mjinga wewe ugonjwa umekatwa na mtalii ,mtanzania au myama lazima tahadhari zichukuliwe na mipango dhabiti na endelevu iwekwe wazi ili kila mtu ajikinge,ajiangalie baadaye tuendelee na kazi zetu kama kawaida.

Statistics za magonjwa mengine zipo kwenye system ya serikali inaitwa MTUA 1 utapata za Ukimwi na related diseases nk takwimu zote za magonjwa mengine zipo .

Ndio maana ulienda hospitali kwa daktari au basi kwenye hospital yoyote kuna likitabu likubwa kila mwezi kila taarifa za.mgonjwa na magonjwa zipo kwenye database ya serikali.Ukitaka kujua ni wangapi wamepimwa malaria,wakutwa positive ,wamekufa nk
Kwasababu ni “novel virus”, pale New York sasa hivi kuna ugonjwa unawapata watoto ambao unahusishwa na corona, hivyo hili siyo gonjwa la kuliachia lisambae kwa kasi hii na huku solution haipo karibu.
 
Koyu keza mbochi ndio Mabeberu wanachojua kwa sasa.
 
Mliposema “Kwani watu wa mikoani hawahitaji vitenge”, hamkufikiria namna ya kuwalinda wakati mnawapelekea hivyo vitenge? Hamkufikiria kuwalinda wakati mnaenda kununua vyakula? Wakikumbwa na gonjwa mtakula wapi?

Au uweke wazi kuwa uchumi unaendeshwa na nani. Kwasababu hata hii issue ya sukari inaonyesha tuna uchumi hohehahe!
Uchumi unaendeshwa na siasa.Ishu ya sukari ni much know za wanasiasa bei upangwa na demand na supply, wao walikuwa usingizini hawakuona upungufu ili waweke stock ya kutosha demand.
 
Kwasababu ni “novel virus”, pale New York sasa hivi kuna ugonjwa unawapata watoto ambao unahusishwa na corona, hivyo hili siyo gonjwa la kuliachia lisambae kwa kasi hii na huku solution haipo karibu.
Kosa la China ni kutoweka uwazi yaani walifucha taarifa, ungedhibitiwa mapema usingesambaa duniani.
 
Hakuna ubishi kwamba kilimo ndo kimekuwa nguzo kuu ya uchumi wa Tanzania, ambapo kilimo kinachangia 24.5% kwenye GDP.

Kilimo kinachangia asilimia 85 kwenye total export, na pia nusu ya waajiriwa wote wanatokea kwenye sekta ya kilimo, kwa mujibu wa data zilizopo mitandaoni. Lakini kwenye uchumi wetu kwa ujumla, sekta nyingine zaidi ya Kilimo, kuna utalii, uvuvi, madini, misitu, nyuki, nishati na “uzalishaji”

“The main sectors are agriculture, tourism, fishing, forestry and beekeeping, mining, manufacturing and the energy industries. Agriculture – plays an important economic role as it employs 75% of the population.“

Sasa kilimo ndicho kina ajiri asilimia 75 za wananchi wa Tanzania! Sasa ukitizama kwa makini, utaona kwamba ilikuwa ni ujinga kuiogopa corona na kudai tuombe Mungu ataizuia. Tukaikuza na kuijengea mazingira rafiki ya kusambaa zaidi makanisani na misikitini kwa kuagiza mikusanyiko ya kuomba dhidi ya gonjwa linalosambaa kutokana na mikusanyiko!, na wakati tulikuwa na nafasi kubwa na nzuri kabisa ya kujifunza kutoka kwa wenzetu. Lakini badala ya utaalam, zikaingizwa siasa.

Jiji la Dar siyo siri ndo kitovu cha gonjwa hili. Lakini sababu zilizotolewa kuhusu katazo la lockdown, hazikuwa na mantiki, kwasababu kwanza hatukuwa na ulazima wa total lockdown!

Pili, kusema eti “Kwani watu wa Dar hawataki viazi”, ama watu wa mikoani “hawataki vitenge”, siyo kauli zenye kuonyesha weledi kwenye janga linalotukabili.

Kuhakikisha sekta ya usafirishaji, haswa kutoka na kuingia Dar ikiwemo mizigo na abiria, inakuwa monitered ili kupunguza maambukizi, kama wanavyofanya wenzetu (Uganda, Zambia, Rwanda etc), kwenye borders zao wakati wanapokea mizigo kutoka kwetu pamoja na raia. Sisi tuliacha kila kitu wazi. Hata mipaka haikufungwa, bali ilijifunga yenyewe tu kutokana na majirani kufunga mipaka yao. Kwenye anga ni hivyo hivyo.

Pia, kama tunategemea Kilimo, kwetu sisi ilikuwa rahisi sana kuhakikisha kuwa sekta hiyo haswa upande wa usafirishaji, inakuwa monitored na hatua zote stahiki zinachukuliwa ikiwa ni pamoja na kuwapima madereva, pamoja na wafanyakazi wote walioko kwenye sekta ya kilimo na usafirishaji wa bidhaa zake. Kuhakikisha maelekezo ya wataalam wa afya yanafuatwa.

Chloride
inasaidia kwasababu yenyewe haina tofauti na bleach. Lakini ilizuiliwa na mwanzoni niliona baadhi ya viongozi kaka Mama Mughirwa wakifanya jitihada ambazo zilitakiwa kuendelezwa siyo tu kwenye mabasi, bali hata vyombo vya usafiri vinavyoingia na kutoka Dar.

Lakini sababu inayotolewa kuwa watu watakufa njaa haina mashiko. Madhumuni haswa ya lockdowns, ni kuhakikisha ni ya muda mfupi(mara nyingi siku 14), kwenye eneo athirika (tulikuwa na nafasi hii kuliko wenzetu). Lakini tulizembea mwanzoni tukidhani ni gonjwa la wazungu tu hilo. Au “kakolona!” Au “tumafua tu!”

Lengo la lockdown, pale inapowahiwa mwanzoni kabisa, ni kwamba inakuwa ni eneo dogo. Mfano Dar ni kubwa. Lakini wagonjwa hawakusambaa jiji zima kwa wakati mmoja. Wagonjwa waliopatikana mwanzoni kabisa, kungewekwa lockdown ya eneo hilo husika kwa siku 14, huku kukiwa na juhudi za usiku na mchana za tressing pamoja na isolation, yani kuwatafuta watu walio kutakana na waathirika hao. Ni rahisi kuwapata mapema kabla hawajausambaza kwenye kipindi ambacho hawaruhusiwi kutembea. Maana kwa kipindi hicho cha siku 14, wale walioambukizwa, wengi wao dalili tayari zinakuwa wazi.

Na hivyo kwa kipindi hicho, kazi ya tressing ama utafutaji na ufuatiliaji wa wale waliokutana na waathirika inakuwa siyo kubwa na kwasababu wako ndani, wanakuwa hawasambazi, na baada ya kupatikana, wanahudumiwa na baada ya hapo lockdown ya eneo husika inaondolewa kwa tahadhari. Kwasasa tumeshachelewa kwa kiasi kikubwa. Lakini ni muhimu hatua zikachukuliwa, kabla janga halijatapakaa huko vijijini ambapo ndipo kwenye ugali wa nchi!

Nasema “kwenye ugali wa nchi”...Sasa je? kama uchumi wetu unaendeshwa na mkulima, kwanini hatuchukui hatua stahiki kumlinda? Wakulima wanawalisha wale wanaobwatuka huko mjini! Lakini hawajui madhara yake ya ubwatukaji huo. Mwishowe, ugonjwa ukifika vijijini uchumi unaanguka chali! Ama viongozi wanadhani Dar inaendeshwa na nani kiuchumi? Eti watu kurandaranda Dar ndo nguzo ya uchumi?

Taifa la Marekani lina “mixed economy”, ila linategemea viwanda sana kwenye livelihood yake. Mfano viwanda vya vyakula, vimekuwa na maambukizi sana. Kiwanda kikubwa kabisa cha nyama kinachoitwa Tyson’s, kimeanza kufilisika kwasababu hiyo. Hawakuweka wala kuchukuwa hatua na tahadhari. Wengi wanaofanya kazi humo ni immigrants na minorities, wengi wameambukizwa na kupelekea viwanda kufungwa na hivyo kusababisha upatikanaji hafifu wa chakula kwenye supermarkets.

“Supply and demand are the forces that drive the U.S. economy. Supply includes labor, represented by employment, and natural resources, such as oil, land, and water. Oil prices drive 70% of the cost of gas. Demand, or personal consumption drives almost 70% of the economy.”

Kwajinsi uchumi wa marekani ulivyo, ni wazi kwamba unaendeshwa na labors. Watu wasiolipwa mishahara ya maana. Watu ambao ni kama wanalitumikia tabaka moja ambalo kwasasa linahisi kuanza kuikosa ile privilege waliyokuwa nayo ya kutumikiwa.

Watu wa chini na tabaka la chini ndiyo nguzo ya uchumi wa marekani. Hata nchi ama uchumi ukifunguliwa, wao ndiyo wako kwenye hatari zaidi ya maambukizi.

Ni tabaka dogo lenye wafuasi wasiojitambuwa ndiyo wenye kuona kwamba hatua zilizochukuliwa, na zinazoendelea kuchukuliwa, hazikusaidia na wala hazitasaidia kupunguza idadi ya vifo na pengine uchumi kuanguka moja kwa moja.

Without lockdown across the world coronavirus would have killed 40 million, experts say

Kama ilivyo kwa hawa oligarchies wa marekani pamoja na minions wao, kuna uwezekano kuwa kama kuna kitu kitatupa shida na sisi kama Taifa ni matabaka. Kuna wakusanyaji, wapangaji na watumiaji wa kodi zetu (wakati mwingine kibabe). Hawa wamekuwa na tabia ya kutokujali maisha ya watu wala kuona kwamba yana umuhimu! Wao starehe yao imo kwenye kodi wanazokusanya, na vitu wanavyoviona bila kujali gharama zake. Kama vile ambavyo kuna hao wazungu wanaokaa mezani kula “fillet mignon”, bila kujuwa zinafika mezani kwa style gani. Hao ni wale wasiotambuwa kuwa privileges zao zinatokana na sacrifices za kila aina kutoka kwenye matabaka ya chini, na hivyo hawaoni umuhimu wao!

Sasa hatua ambazo ilikuwa tuzichukuwe sisi dhidi ya jiji letu la Dar, ndizo hatua wanazozichukuwa majirani zetu dhidi ya Taifa letu. Sasa maamuzi yaliyofanywa ni sahihi? Charity begins at home!

Kama uchumi wetu unaendeshwa na mkulima, hizo nyingine zilikuwa blah blah na kupanic kwa kukosa plan.
Wananchi wanaanza kugundua ukweli kuhusu rais, pia majirani zetu walishagundua mapema zaidi. Ulimwengu mzima umeona namna tunavyocheza na kifo. Watz tafadhali tuache kukaa pembeni na kuangalia, tuchukue hatua, tuachane na ccm.
 
Mjinga mmoja anayepoteza muda wake kukamata wanaomsema vibaya mtandaoni..smh
 
Wananchi wanaanza kugundua ukweli kuhusu rais, pia majirani zetu walishagundua mapema zaidi. Ulimwengu mzima umeona namna tunavyocheza na kifo. Watz tafadhali tuache kukaa pembeni na kuangalia, tuchukue hatua, tuachane na ccm.
Well said👏🏽
 
Back
Top Bottom