Wakulonga
JF-Expert Member
- Oct 29, 2012
- 762
- 771
Mimi nilikuwa ni miongoni mwa watu waliokuwa wanafuatilia kwa makini sana sakata la Ebola tanzania. Hawa mabeberu waliuaminisha ulimwengu kuwa tz kuna Ebola na kushindana katika kutoa matamko kwa raia wao. Mimi nijuavyo Ebola kama pembe la ng’ombe halifichiki cha kushangaza mpaka leo sijackia sehemu fulani ebola inaendelea kuua watu. Hivi kweli Ebola iliwapo nchini au ndo mbinu za mabeberu na vibaraka wao kutaka kuichafua nchi kwa maslahi yao. Mbona hata hao vibaraka wao nao wapo kimya hawatoi takwimu ya watu waliokufa kwa ebola mpaka sasa ni wangapi. Ama kweli ukitaka kumuua mbwa kwanza mpe jina baya kisha muuwe hamna atakaye kuuliza. Jamani mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. UNCLE CHAPA KAZI mabeberu na vibaraka wao kina Lisu washaanza kukuelewa.Watulie dawa iwaingie maana dawa hii haichagui mweusi au mweupe.