Kaka! ! You have nailed it kiasi ambacho hata zuzu atakuelewa, kweli kuna watu wanapendelea kudhihaki western media kwa sababu wanazo zijua wenyewe, ni kweli wakati mwingine media hizo huwa zinaripoti kwa maslahi yao, lakini si muda wote,
Mwaka 1996 Cnn walikua wa kwanza kutoa na kurusha live habari ya Mv Bukoba walikuwa na maslah gani katika ajali ile ?mwaka jana tulishuhudia live coverage ya shujaa mandela, kutoka Bbc, Cnn etc,.
Binafsi napenda sana habari, nina karibia news source za karibi kila pande.ya huu ulimwengu ,Kuanzia hizo western, aljazeera, iran na russia tv, katika suala hili la ebola sijaona likizungumziwa kama janga la sehemu moja, hizo media za afrika.magharibi naangalia pia zinachofanya ni kulalamika tu,
Hapo kwenye stastitics na utafiti ndio kabisa tumeshindwa, kama kweli walitengeneza Aids na Ebola, kulikuwa na haja gani wao mosi kutuambia, pili kufanya jitihada za ku contain kwa Arvs and the like, au labda sifahamu nijuzwe kuna taasisi au shirika lolote la afrika lililobadilisha chochote kuhusiana na magonjwa hayo,? Tumefikia wapi na tafiti zetu? Ina maana magharibi wana hila hadi.kwenye utashi wetu wenyewe. Mikoa iliyoongoza kwa maambukizi ya ukimwi kagera na sasa iringa, kwa kiasi.kikubwa ilichangiwa na wanaume kutofanyiwa tohara , leo hii kuna kampeni ya tohara ya bure tena kwa watu wazima, tulikuwa na ujanja wa kulitambua hilo kwa tafiti zetu? ,vipi kama tusingeambiwa?
Hizo hizo.media zinazobezwa, leo hii ndo zinakuja na fact kuwa hata huko marekani , kuna maambukizi ya ebola, na kweli tunashuhudia juhudi zinafanywa ili kuncontain maambukizi kwa kupeleka madaktari, na kuzuia connection zote za usafiri kwenda west africa ili lisije kuwa janga la dunia, kama kweli wa magharibi wana hila hapa ndo ulikuwa wakati muafaka wa kukaa kimya , wakituangalia tunavyopukutika na ebola.