Hivi Ulengaji shabaha (sniping) ni kipaji au unapitia mafunzo maalumu?

Hivi Ulengaji shabaha (sniping) ni kipaji au unapitia mafunzo maalumu?

kanonb

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2016
Posts
391
Reaction score
328
Habari wanajamvi poleni na misongo ya mawazo (tozo) na mengine mengi.

Tafadhali naomba wajuvi wa mambo naomba kuuliza swali hivi hawa watu walenga shabaha (snipers ) wanapatikanaje jeshini ni mafunzo tuu au na kipaji cha mtu kinachangia?

Je, training zao zipo kama za askari wa kawaida au kuna la ziada na katika kikosi kimoja cha askari huwa wanakaa wangapi (katika mission)?
 
Mkiwa jeshini, kwa ajili ya mafunzo (military course) achana na hii kwa mujibu wa sheria, pamoja na mafunzo mengi mtakayopitia baadae mtaanza mafunzo ya kutumia silaha, kwa maana ya kuifahamu silaha kuanzia kuifungua, kuisafisha, kuifunga tena na kisha kuitumia.

Kwenye mafunzo ya kuitumia (range) kuruta (wanafunzi wa kijeshi) wote mtapewa silaha na idadi sawa ya risasi then tunaelekea uwanja wa range ambako tutakuwa na kazi ya kuilenga ile bull (target) kwa idadi ya risasi 5 kwa kila kuruta, hapo sasa ndo tunaanza kuwapata mananga na walioiva (hapo mnakuwa mshapewa maelekezo jinsi ya kulenga.) Sasa usnipa unaanzia hapo, i.e kipaji +maelekezo mliyopewa.

Kwenye risasi 5, kuna mmoja hatagusa kabisa bull, kuna mwingine atapiga tu body, kuna mwingine atapiga bull risas moja na kuna mtu atapiga 4 ..hapo sasa ndo mchujo ushaanza ndugu yangu kuelekea usnaipani,

Nimejaribu kueleza kwa kifupi!
 
Ili uwe sniper inabd uende kwenye sniper school,, ni kozi kama kozi zingine and sniper sio for shooting only,, mara nyg wanafanya kaz deep within enemy lines na kufanya reconnaissance, na sabotage na kaz zingne kama hzo,, so sio only for shooting,,
 
Mkiwa jeshini, kwa ajili ya mafunzo (military course) achana na hii kwa mujibu wa sheria, pamoja na mafunzo mengi mtakayopitia baadae mtaanza mafunzo ya kutumia silaha, kwa maana ya kuifahamu silaha kuanzia kuifungua, kuisafisha, kuifunga tena na kisha kuitumia. Kwenye mafunzo ya kuitumia (range) kuruta (wanafunzi wa kijeshi) wote mtapewa silaha na idadi sawa ya risasi then tunaelekea uwanja wa range ambako tutakuwa na kazi ya kuilenga ile bull (target) kwa idadi ya risasi 5 kwa kila kuruta, hapo sasa ndo tunaanza kuwapata mananga na walioiva (hapo mnakuwa mshapewa maelekezo jinsi ya kulenga.) Sasa usnipa unaanzia hapo, i.e kipaji +maelekezo mliyopewa...
Kwenye risasi 5, kuna mmoja hatagusa kabisa bull, kuna mwingine atapiga tu body, kuna mwingine atapiga bull risas moja na kuna mtu atapiga 4 ..hapo sasa ndo mchujo ushaanza ndugu yangu kuelekea usnaipani,

Nimejaribu kueleza kwa kifupi!
Tofautusha marksmanship na sniping,, hyo ya range ni marksmanship,, skill ya muhimu kwa kila mwanajeshi,, sniper z more than sniping
 
Tofautusha marksmanship na sniping,, hyo ya range ni marksmanship,, skill ya muhimu kwa kila mwanajeshi,, sniper z more than sniping
Ila ndo tunaanzia huko mkuu, huwezi kutafuta watu tu frm no where ukasema twendeni mkajifunze, katika ku-make hii skill muhimu kwa kila mwanajeshi ndo tunawatambua sasa wanaoweza kwenda snipping officially
 
Mfano ni Kwenye mafunzo mnaweza mkapewa risas 10 mnawekewa Target mbele hata umbali wa mita 100 baada ya kupewa mafunzo ya utumiaji sahihi wa silaha
katika kulenga hizo 10 wapo wataokosa zote wapo watakao piga Target kwa risas 5 , 2, 1 na ile target inakua na michoro sahihi ambayo inatoa point kwa kila sehem inayo pigwa mfano wa hii Target hapa chin ukipiga kwenye sehem nyeusi ni point 10 na unavyozid kupiga nje point zinapungua kuna 9,8,7,6
Hivyo majaribio ya Mara kwa Mara wapo watakao kua na uwezo wa kutandika risasi nyingi kwenye hii point nyeusi ambapo anakua anajikusanyia point nyingi zaid ya wenzake hao ndo wanaenda kuendelezwa na kupewa mafunzo zaid ndo ma-sniper wanavyoanza kuchujwa.
Target-6-Basic-791x1024.jpg
 
Habari wanajamvi poleni na misongo ya mawazo (tozo) na mengine mengi.

Tafadhali naomba wajuvi wa mambo naomba kuuliza swali hivi hawa watu walenga shabaha (snipers ) wanapatikanaje jeshini ni mafunzo tuu au na kipaji cha mtu kinachangia?

Je, training zao zipo kama za askari wa kawaida au kuna la ziada na katika kikosi kimoja cha askari huwa wanakaa wangapi (katika mission)?
Hamza alijifunza kupitia mitandao, tumia simu yako.
 
Habari wanajamvi poleni na misongo ya mawazo (tozo) na mengine mengi.

Tafadhali naomba wajuvi wa mambo naomba kuuliza swali hivi hawa watu walenga shabaha (snipers ) wanapatikanaje jeshini ni mafunzo tuu au na kipaji cha mtu kinachangia?

Je, training zao zipo kama za askari wa kawaida au kuna la ziada na katika kikosi kimoja cha askari huwa wanakaa wangapi (katika mission)?
Pamoja na kipaji na interest kuna mafunzo rasmi na maalum
 
Nasikia yule jamaa wa 2017 kule dodoma jiji aliye mnani nani alikuwa ni sniper sasa mbona alishindwa kazi na alitumwa na yule aliye kuwa nani. 🙅🤒🤒
 
Asante wakuu kwa maelezo yenu Mujarabu kabisaa naomba kujibiwa na swali la pili huwa ni wangapi katika kikosi cha askari wanapokuwa kwenye mission
 
Mfano ni Kwenye mafunzo mnaweza mkapewa risas 10 mnawekewa Target mbele hata umbali wa mita 100 baada ya kupewa mafunzo ya utumiaji sahihi wa silaha
katika kulenga hizo 10 wapo wataokosa zote wapo watakao piga Target kwa risas 5 , 2, 1 na ile target inakua na michoro sahihi ambayo inatoa point kwa kila sehem inayo pigwa mfano wa hii Target hapa chin ukipiga kwenye sehem nyeusi ni point 10 na unavyozid kupiga nje point zinapungua kuna 9,8,7,6
Hivyo majaribio ya Mara kwa Mara wapo watakao kua na uwezo wa kutandika risasi nyingi kwenye hii point nyeusi ambapo anakua anajikusanyia point nyingi zaid ya wenzake hao ndo wanaenda kuendelezwa na kupewa mafunzo zaid ndo ma-sniper wanavyoanza kuchujwa.View attachment 1930252
Naomba nisaidie nakala ya hiki kitabu
 
Nasikia yule jamaa wa 2017 kule dodoma jiji aliye mnani nani alikuwa ni sniper sasa mbona alishindwa kazi na alitumwa na yule aliye kuwa nani. [emoji135][emoji855][emoji855]
Yule alie mnanii nanii siyo sniper sniper anapiga risas moja tu akikosa Target anaweza kurudia ya pili lakin akikosa mission inakua imefeli na anaondoka eneo la tukio kwa haraka sana Sasa yule alie mnanii nanii alipiga risasi zaid ya 16 inaonekana ilitumika bunduki ya kivita na siyo silaha maalum kwaajili ya sniper
 
Back
Top Bottom