Hivi Ulengaji shabaha (sniping) ni kipaji au unapitia mafunzo maalumu?

Hivi Ulengaji shabaha (sniping) ni kipaji au unapitia mafunzo maalumu?

Nasikia yule jamaa wa 2017 kule dodoma jiji aliye mnani nani alikuwa ni sniper sasa mbona alishindwa kazi na alitumwa na yule aliye kuwa nani. 🙅🤒🤒
Kushindwa kwa sniper kunatokana na kazi kuwa haramu, wao hufunzwa kwa ajili ya kazi halali tu.
 
Habari wanajamvi poleni na misongo ya mawazo (tozo) na mengine mengi.

Tafadhali naomba wajuvi wa mambo naomba kuuliza swali hivi hawa watu walenga shabaha (snipers ) wanapatikanaje jeshini ni mafunzo tuu au na kipaji cha mtu kinachangia?

Je, training zao zipo kama za askari wa kawaida au kuna la ziada na katika kikosi kimoja cha askari huwa wanakaa wangapi (katika mission)?
Kuna wenye vipaji vyao wanabahatikaga kuingia huko na kuna vile vile kuna wenye vipaji vyao ambao wapo tuu hawajulikani pia ila kwa wale waliotreiniwa huwa na mafunzo zaidi yaani step by step .
Picha inawekwa full risasi 5 unaambiwa lenga sehem fulan 5 sehem fulani 5 sehem fulan 5 sehem fulan wakati huo hiyo sehemu ambayo ushalenga hiyo picha inabadilishwa kulinga na unapolenga.
Kwa mfano kama ni kiuno baada ya 5 hizo kinaondolewa(kufutwa pale kwenye target)kama ni shingo hivyo hovyo kama ni kichwa tena jichoni au ile sehemu ya paji la uso (ile sehemu wanaosali sana inaota sijida) givyo hivyo hadi hatua ya mwisho amboayo sasa point unawekewa nukta (yenye muonekano kwa mbali )naa...
Naomba niishie hapo kwa leo.
 
Mkiwa jeshini, kwa ajili ya mafunzo (military course) achana na hii kwa mujibu wa sheria, pamoja na mafunzo mengi mtakayopitia baadae mtaanza mafunzo ya kutumia silaha, kwa maana ya kuifahamu silaha kuanzia kuifungua, kuisafisha, kuifunga tena na kisha kuitumia.

Kwenye mafunzo ya kuitumia (range) kuruta (wanafunzi wa kijeshi) wote mtapewa silaha na idadi sawa ya risasi then tunaelekea uwanja wa range ambako tutakuwa na kazi ya kuilenga ile bull (target) kwa idadi ya risasi 5 kwa kila kuruta, hapo sasa ndo tunaanza kuwapata mananga na walioiva (hapo mnakuwa mshapewa maelekezo jinsi ya kulenga.) Sasa usnipa unaanzia hapo, i.e kipaji +maelekezo mliyopewa.

Kwenye risasi 5, kuna mmoja hatagusa kabisa bull, kuna mwingine atapiga tu body, kuna mwingine atapiga bull risas moja na kuna mtu atapiga 4 ..hapo sasa ndo mchujo ushaanza ndugu yangu kuelekea usnaipani,

Nimejaribu kueleza kwa kifupi!
Safii baba umeiva
 
Habari wanajamvi poleni na misongo ya mawazo (tozo) na mengine mengi.

Tafadhali naomba wajuvi wa mambo naomba kuuliza swali hivi hawa watu walenga shabaha (snipers ) wanapatikanaje jeshini ni mafunzo tuu au na kipaji cha mtu kinachangia?

Je, training zao zipo kama za askari wa kawaida au kuna la ziada na katika kikosi kimoja cha askari huwa wanakaa wangapi (katika mission)?
Ni kipaji tu hicho brother!
angalia hapa
 
Udunguaji ili uwe bora ni lazima uende kozi maalum,japo wapo wenye shabaha kiasili lakini bado ili uwe mdunguaji mzuri itakubidi uende kozi..
Utaenda kozi kwa kuwa utatakiwa kujua matumizi sahihi ya silaha ya kudungulia,ujue mahesabu,ujue kujificha usionekane,pia uwe na mbio na mambo mengine muhimu..
 
Nina swali la kizushi, je ni kweli risasi ya SMG ikipigwa inasafiri km 3? Yaani mita 3000?

Msaaada tafadhali.
Sub Machine Gun haina uwezo huo wa kusafiri 3000m,mita 400 inaweza kutembea au ikitembea zaidi ya hapo haiwi na madhara kwa tageti..
 
Ni kipaji tu angalia hapa
 

Attachments

  • VID-20210415-WA0000.mp4
    6.4 MB
  • VID-20210415-WA0006.mp4
    2.1 MB
Yule alie mnanii nanii siyo sniper sniper anapiga risas moja tu akikosa Target anaweza kurudia ya pili lakin akikosa mission inakua imefeli na anaondoka eneo la tukio kwa haraka sana Sasa yule alie mnanii nanii alipiga risasi zaid ya 16 inaonekana ilitumika bunduki ya kivita na siyo silaha maalum kwaajili ya sniper
Daaah noma sana aiseee 🙌🙌🙌🙌
 
Pale kibaha kuna majamaa yanashinda asubuhi to jioni kazi yao ni moja tu,hayo mambo ya kulenga shabaha.
 
Back
Top Bottom