Haya maisha haya, unakutana na mambo mengi sana ya kukuumiza moyo na kukufurahisha yes dunia imeumbwa hivyo.
je wewe umeweza kusamehe kila jambo lililokutokea au linalokutokea katika maisha yako? mimi nimeshindwa, kuna watu bwana nilikua nao very close, katika maisha yetu mimi ndie nilikua nakwenda kuwatembelea.
Nikisikia wanaumwa nishafunga safari, nikijua tu nina muda sijaonana nao najikuta nishafunga safari, ikumbukwe hapo ninapokaa ni karibu na barabara kuu, yani huwez kua una safari ya mjini au kurud bila kupita ninapokaa lakini hakujatokea hata mmoja kuja kunitembelea na ukiona umetembelewa ujue mtu alikua anakuja eneo la jiran ulilopo ndio mtu anapita.
Kisa kinakuja hapa kuna mambo flan flani niliyataka yafanyike kwao, hawa ni ndugu zangu upande wa baba, bas pia wakanipigisha danadana lisifanyike na maneno ya kejeli nikaona isiwe kesi jambo likafanyikia nyumban kwa wazazi wangu, since then nimekua na hasira nao kiasi nashindwa kumove on.
Yaani hata ile kwenda kuwatembelea sifanyi tena na mimi naweza kuwa nnashida na maeneo waliyopo nahata nisiende na naweza kupanga kabisa ngoja niende moyo wangu ukawa mzito mpaka naghairisha kuna mmoja nilikutana naye ananiuliza mbona huji siku hizi nilimjibu tu nimechoka kufatafata watu ambo sioni umuhim wao kwangu nikampa ukweli wa moyo lakini bado nafsi yangu kama ina kinyongo dhidi yao nifanyeje iniepuke hii hali?