Hivi umewahi kuhisi kuna upendeleo wa baadhi ya watoto kwenye familia yenu?

Nimeona nami nichangie kitu hapa
Mimi ni first born kwenye familia yetu yenye watoto wa tatu na kitu cha kipekee mimi ndio mtoto pekee wa kiume
Wadogo zangu wamekuwa na-jelaous na mimi ni kutokana na mama kunipenda zaid ya wao hii inatokana na kuwa tukipitia through a lot kwenye makuzi yangu
Tulinusurika kifo wakati nilipo zaliwa tulipata ajari ya gar na mama wakati tukitoka sehemu nilipo zaliwa tukielekea nyumban
Pili life halikuwa zuri wakati ninakuwa so ilinibidi ni msaidie bi mkubwa kwenye shughuli zake za mama lishe
Ila kwa hawa madogo now wanaishi kwenye comfort zone na kitabia wakotofauti sana na mimi kidogo huyo wa mwisho
Kitabia mimi ni mpole sio mgomvi na wala sijawahi kumbishia bi mkubwa, kwa now inafika kipindi nikiwa narud home kwa likizo utasikia madogo wanasema mtoto wa mwisho huyo karud
Hayo ndo machache kwa ufupi
 
Tunawapenda watoto wote ila ni ngumu kumpenda mmoja zaidi ya wengine ambaye hata wengine wanajua wakihitaji kitu fulani kutoka kwa mzazi anayempenda wanamtumia kama chambo ili kufanikiwa.

Watoto wa mwisho wanapendwa na wazazi wote na nguvu zote za ulezi wa kudekeza huelekezwa kwake.

Kama watoto wote ni wa kike au wote ni wa kiume Mtoto anayependwa na mama hawezi pendwa na baba hali kadharika kwa mama pia. Na hilo halikwepi.

Na kama ni mchanganyiko basi Mtoto wa kike anaegemea kwa baba na wanatengeneza bond ya kudumu mpaka mama anaweza ona wivu vivyo hivyo Mtoto wa kiume huegemea kwa mama na kuwa Mtoto wa mama.

Lakini jambo ambalo hatulijui ni kuwa upendo wetu mkubwa kwa watoto ndio hugeuka kuwa chuki na uhasama baina yetu.

Fikiria baba mwenye mtoto wa kiume ambaye anampenda mnoo na anataka afanikiwe katika maisha yake kama kiongozi wa familia ajaye. Hawezi kumuacha awe mzembmzembe na asiyetegemeka. Atata ahakikishe anakuwa mwanaume kweli atakayelinda familia yake kiuchumi, kifkra, nguvu na mengineyo. Tegemea mtoto huyo akifanya uzembe tu kwa upendo wa baba atakula fimbo au adhabu nyingine. Lakini wakati huohuo mama atambembeleza na kumpakulia tuwali kidogo jikoni na tumchuzi twa nyama. Automatically mtoto ataona baba hampendi na mama ndio anampenda. Na ndio haya matoto ya mama yaliyopo siku hizi.


Lakini pia mama kwa upendo anataka binti yake akue na kuwa mwanamke bora . Mama hatataka mzaha. Akifanya makosa au uzembe katika maswala ya nyumbani na jikoni basi atakula sana ubapa wa mwiko na kurushiwa masufuria. Akikimbilia sebuleni anapokewa na baba na kukumbatiwa. Na ikiwezekana anafoka kwa mama apunguze adhabu anasahau ya kwake na mtoto wa kiume. Ona bond inavyotengenezwa hapa na nyingine kubomolewa. Na ndio maana watoto wa kike huwaambii kitu kuhusu baba zao labda awe mwehu.


Upendo ndio umetengeneza matabaka ya upendo katika familia na si chuki. Na siku zote wapokeaji wa adhabu hawaamini kama wanapendwa kwa kupewa adhabu ni mpaka wakikua ndio hutambua kuwa wazazi waliwajenga ama kuwaharibu katika malezi.

Mimi tumekubaliana na mwenzangu nikiwa natoa adhabu kwa mtoto au yeye ndio anatoa basi tukielewa tatizo tuunge mkono na hakuna kubembeleza mmojawapo ili wajue wote wawili hatujafurahishwa na alichofanya. Lakini upendeleo hauwezi kuisha kabisa.
 
Wabongo hatupendi kufata ethics na nidhamu majority ni sadist ndio maana wanakuwa Happy wengine wakitukanwa na kuzalilishwa loh.
[emoji23][emoji23][emoji23] Pm nafungua baadae
Baadaye saa ngapi my dear?
 
Mimi nimezaliwa wa kwanza nilipendelewa/nilidekezwa sana nikiwa mdogo lakin ikafika hatua sikupendelewa tena na upendo ukapunguzwa kabisa na nikawa mimi ndo mtoto wa kufanya kazi ngum za nyumbani, kuchimba shimo la takataka, yanaweza yakaletwa matofali/mchanga mzee akaniambia mimi ndo nihamishe kutoka sehem moja kusogeza sehem fulan na wala haina sababu ya kuyasogeza ila ni bas tu Ni vile aliamua niwe na kula kwa jasho nikiwa hapohapo nyumban had nikahisi nachukiwa kumbee laa mzee aliamua kunikomaza kiume makusudi tu maana dunia siyo nyepesinyepesi.

Mtoto ambae hajadekezwa huwa inamjenga sana kuwa mpambanaji na hata akiwa na biashara au kupata kaz n lazma aheshim alicho nacho, ila walio dekezwa anaweza akaacha kaz kisa amefokewa tu na kusahau malengo yake kwa kukatishwa tamaa na vikwazo vidogo maana uvumilivu unakuaga 0
 
Wala hujanikwaza rafiki.
Amen. Napokea baraka kwa niaba yake.
 
Upendo wa mzazi kwa watoto hauwez kuwa sawa hii hata nyumban nimeiona mama alikuwa anampenda sanaa kaka yangu ninaemfata kw akuzaliwa kuliko watoto wengine sababu sijui ninn maana huyo braza alikuwa mtukutu sanaaa ila baba alikuwa ananipenda sanaa mm sababu naamin nikiwa mm nilikuwa mtoto mtulivu sanaa sio mzururaji nina heshima napia nilikuwa nabidii katka masomo kuliko watoto wote
 
well well said mkuu
 
Ka-ugonjwa ka upendeleo Namge..??
yeah kuna mtoto mmoja kati yetu..mzee anampenda mpka ameshindwa kuficha..huwa anasema waziwazi kbsaaa..
Afu ndo kivuruge hatari..bhasi huwa tunacheka tu..tunaagiza bia tunakunywa siku zinaenda.
 
Hahaa hakuna feeling tamu kama kujua you are loved! That is awesome. Mimi mama ananipenda ila Sasa changamoto siwezi kurudisha that same love. Niliondoka home nikiwa 14 years kule nilikoenda aliyenilea akanionesha upendo. Nimejikuta nimeuhamisha wote yani. Nimejitahidi kuurudisha ila wapi. Mpaka mama anajua nampenda mlezi kumzidi. Sometimes naumia ila kuna vitu vipo out of our control.
 
Kuna kutokupendwa na kubaguliwa hayo yote nimeyapitia.. sikuwa napendwa na nilibaguliwa hali ilipelekea nikakosa hata elimu kwani mimi na dada yangu tulimaliza shule ya msingi pamoja na tukafeli wote . Yeye akapelekwa shule ya kulipia mie nikaachwa nyumbani na sikuwahi kuuliza maana nilijua niko fungu gani. Yaani si kwa baba yangu wala kwa mama yangu.

Cha ajabu walianza kuonyesha upendo naweza sema ni wakinafki mara baada ya kusikia nafanya kazi. Walikuwa hawajali wala hawakuniuliza nafanya nn waliona tu natoka na kurudi basi wakasikia kwa watu kuwa nina kazi na walizidisha kuonyesha upendo nilipowaambia kuna mtu analeta barua na nikaolewa. Na mimi sasahivi ninikukumbuka yale mambo siwatafuti hata miezi sita .. nikikumbuka ni wazazi wangu napiga kiwasalimia tena tupo mji mmoja nauli hazidi 3000 kwenda na kurudi hata watoto wangu sijawahi wapelekea nikienda ni mimi tu na mtoto wa kwanza yupo darasa la kwanza na wao hawaniulizi pia... aiisseee nna mengi.. najisikia vibaya nikikumbuka.. ila wanangu nawapenda sawaaa kabisaaaa
 
Pole sana dear,
Hii imeniuma jamani..!!
Mungu akutie nguvu, wasamehe na uachilie ili uishi tu kwa amani,
 
This is really bad...I was not their best either..LAKINI side effects zipo mpaka now.
vuta subira..bora mmoja asome vizuri primary school.. secondary asome kawaida na tution nzuri..afu mwingine secondary peleka private
 
Pole sana dear,
Hii imeniuma jamani..!!
Mungu akutie nguvu, wasamehe na uachilie ili uishi tu kwa amani,
Ahsante hii imenifunza na kunikomaza. Na nitawasuprise pale nitakapomaliza elimu ya juu miaka kadhaa mbele. Yani naomba wawe hai waone. Na bado mimi ndiye msaada mkubwa kwao.[emoji848]
 
Wa kwako haamini Kama ni wako kweli
 
upendo wa mzazi kwa mtoto huwaga hauji automatically Bali kuna sababu lakini Mara nyingi hujenga chuki kwa mtoto anayependwa zaidi mfano Mimi kwetu ni first born na tumezaliwa watatu ,mama yangu ananipenda Sana kuzidi wenzangu Ila ni kwa sababu kwenye malezi sikuwahigi kumsumbuaga kama walivokuwa wanamsumbua wadogo zangu kwa hiyo imesababisha mimi kuchukiwa na kuonekana nakuwa favoured sana.
 

Upendo haulazimishwi lakini unaweza kujitahidi kubalance matendo yako. Mama yako pengine ana majuto ya kutokukaa na wewe muda mrefu Ila mawazo ya wewe kumpenda mtu aliyeliziba pengo lake lazma imfanye ajisikie vibaya na kumuumiza sana. Najua si rahisi lakini inawezekana kiasi mkuu ili umpunguzie maumivu maana mwisho wa siku na yeye anakupenda sana
 
Pole mkuu lakini chuki uliyoibeba lazma ikuathiri kwa kiasi flani, kama itawezekana wekeza nuvu kwa wanao na uiachilie
 
Unakuta labda mtu ni rebel kwenye familia, wazazi kila wakitaka kumnyoosha yeye anakuwa anahisi hawampendi. Halafu kuna yule ambaye wanahisi anafuata njia sahihi so wanakuwa wanampongeza huyu rebel anajihisi kama anatengea.
Na the more rebelious kid unavyozidi jaribu kumnyoosha the more anavyokuchukia na kuzidi kiwa rebelious.
Mara nyingi kunakuwaga kuna shida sema unakuta mzazi haijui. Uwa mtoto kuwa rebelious anakuwa kama vile ana fight back anafanya yale anayojua kuwa hampendi makusudi tu kama kuwakomoa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…