Hivi unajua kuwa Rais Magufuli huwa ni mtu wa kufika bei haraka sana?

Hivi unajua kuwa Rais Magufuli huwa ni mtu wa kufika bei haraka sana?

G Sam

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
11,795
Reaction score
36,704
Kiukweli Rais Magufuli ni Rais wetu ndiyo ila ana udhaifu mmoja mkubwa sana. Ni mtu wa kufika bei haraka kama utamfanyia vitu viwili tu
1. Mpe sifa na ukuu
2. Mpe fedha

1. Sifa na Ukuu
Ukitaka kuamini rejea majina yote yaliyokatwa kwenye ubunge utagundua ni wengi ambao walikuwa "nyutro" na yeye hataki kabisa mwanaccm uwe "nyutro" Unatakiwa kusifia miradi kuipamba na kumpamba na yeye. Fanya kuitembelea na kusema "Haijawahi tokea" Ukifanya hayo wewe kwake utakuwa mchapa kazi na muadilifu.

Rais Magufuli hataki kabisa mwanaccm anayeipa Chadema kipaumbele chochote kile. Huo ni utakuwa ugomvi mkubwa sana kati yenu. Pia kushirikiana na upinzani wa kweli jihesabie huna lako ndani ya utawala wake. Hapendi kabisa kabisa kukosolewa kwa jambo lolote lile hata kama amefanya makosa makubwa.

2. Mpe hela
Huwezi kuamini kuwa sasa rafiki mkubwa wa Rais Magufuli ni kama kina Rostm Azizi maana wanatoa mpunga unaomzidishia sifa. Vimilioni 20 vya harambee mbona safi tu.

Mtu kama Mwanyika leo ni super pamoja na kuharibu kule ACACIA. Jiulize kwanini kina Harbinder na Rugemarila bado wapo mahabusu! Ni kwasababu wamegoma!

Kwa kutambua hayo wengi wa watanzania wasaka tonge wameamua kucheza ngoma yake kwa kishindo kweli kweli. Yani hawa watafanya lolote jambo ilimradi waneemeke kwani wamesha mjulia mkuu wao na habadiliki hivyo ni rahisi sana kuishi naye.

Huwezi kuamini, kama wewe ni msaka tonge basi hakuna kiongozi rahisi kuwahi kutokea kuishi naye kama Rais Magufuli.
 
Jamani mkishiba ugali na maharage uliotafutwa na shemeji zenu msiwe mnakuja kuja. Mbia huku tafadhali!
 
Mithili maji yanavyopenya kwenye sponji na ndivyo ujumbe wako ulivypenya kwenye mioyo ya wasomaji wako na kueleweka barabara hakika umefunua siri kubwa ya supreme leader wetu
 
Rostam kuchangia sh 20m ujenzi wa Kanisa imekuuma sana bwashee?

Ni Rostam huyu huyu aliwanunulia vyombo vya muziki kwaya ya KKKT kinondoni labda utakuwa umesahau bwashee!
 
Kimei alimjengea tawi ka CRDB Chato akaahidiwa CHEO.

Leo kapitishwa kugombea VUNJO, walioshinda KURA ya maoni wamepigwa chini.


Mbatia na Mrema wametumikaa ila leo ni kama wamegeukwa.


Graduates wenzangu tuchukue vitamvulisho vya machinga tuchape kazi kweriiii kweriiiiii
 
Rostam kuchangia sh 20m ujenzi wa Kanisa imekuuma sana bwashee?

Ni Rostam huyu huyu aliwanunulia vyombo vya muziki kwaya ya KKKT kinondoni labda utakuwa umesahau bwashee!
Kisha Rostam akawapa ccm ya Magufuli Channel ten na magazeti yake.
 
Back
Top Bottom