Forbes1990,
Mkuu Mwizi ni Mwizi halafu haya maisha huweza m'badilisha hata mchungaji/shekhe wa leo ukamkuta kesho ni tapeli/kibaka wa kutupwa hadi ukawa unajiuliza kulikoni.
Hayo magari mkuu wakiiba wanaenda yakata kata kila kitu kinauzwa kivyake,hivi dereva wa uber aliechafukwa apate connection ya kwenda kuuza Unga south,kaambiwa mtaji ni 2M tu ya kibongo (fanya uje mwanangu hela ipo huku)
uunafkiri ataogopa kuiba hilo gari asepe? ataiba vizuri tu kwanza kashapga hesabu kwenda south anaenda kwa njia za panya hatumii airport wala bus official (utamkamatia wpi)
Kule anaenda kufanya biashara haramu ambayo haina tofauti na biashara aloifanya huku kupata mtaji wa biashara ya south,kwa ufupi mwizi ni mwizi tu na akiamua kaamua hata umchukue makalio print,umchukue picha kila kona ya mwili wake,Ukiona Haibi sio kwamba kaogopa ZILE TAARIFA ZAKE alizochukuliwa,ila anakuwa tu kawaza familia yake/ndugu/nk nk.
Ndio mana kuna kampuni kama huna Familia (hupewi ajira) wanajua kabisa wewe anytime unaweza badilika maana huna cha kupoteza,hivyo huyu jamaa yeye anahofia wizi ila hajaamua kuwaza kuna hata matapeli wa LIVE uso kwa uso.
Mtu anakufata anakupanga live mnaangalia uso kwa uso unampa hela kisha analala mbele,hivi huyu tapeli haogopi kuja kudakwa siku 1 kwasababu kashaonekana? Biashara ni Majaribu mkuu.