Hivi unakubaliana na kauli kwamba Mwendokasi wanajiendesha kwa hasara?

kimsboy

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
9,846
Reaction score
20,319
Kauli ya kamati ya bunge imeniacha hoi na mshangao sana kwamba eti kampuni ya mwendokasi inajiendesha kwa hasara

Hili nalipinga kwa nguvu zote, kwa jinsi wanavyojaza abiria na wateja wake ni wengi hakuna muda unakuta mwendokasi haijajaa sasa hizo kauli za kwamba wanajiendesha kwa hasara zinatoka wapi?
 
Jiandaeni kwa kupandishiwa nauli ,hizi ni za chini ya kapeti nauli itskuwa kati ya tsh 800 na tsh1000 wanafunzi sh400
 
[emoji23][emoji23][emoji23] Kwahiyo Atcl inavyopata hasara haina wateja? Kwahiyo Tanesco pia haina wateja? Kijana uwe ugoogle hata mara moja moja kwa mwezi uondoe hizi aibu ndogo ndogo.

Hata Dawasco utakuta ina hasara
Waswahili Sisi bado Sana kwenye management
 
Halafu mjue nyie watu wazima mnatupeleka shimoni mmekalia majungu tu na uzembe tu pumba#"&u zenu
 
tatizo hela zinatembea kwenye mikono ya watu, serikali waweke njia za electronic kwenye ulipaji nauli kuanzia kwenye mwendo kasi, vivuko na usafiri wowote wa serikali. mambo ya kutoa hela kama upo dukani kwa mangi ndo yanakwamisha mahesabu.
 
Na namna wanavyowaacha abiria vituoni na kupitisha magari matupu kutoka Kimara hadi Jangwani, ni lazima kweli hasara iwepo.
 
[emoji23][emoji23][emoji23] Kwahiyo Atcl inavyopata hasara haina wateja? Kwahiyo Tanesco pia haina wateja? Kijana uwe ugoogle hata mara moja moja kwa mwezi uondoe hizi aibu ndogo ndogo.
Wateja ndo input namba moja kwenye biashara , kama una wateja halafu unapata hasara maana yake ni kuwa una mfumo dhaifu.
Hao Tanesco , Atcl wote hawakustahili kupata hasara kama wangekuwa na mfumo madhubuti
Miaka flani kivuko cha kigamboni kulikuwa kinapata hasara pamoja na nyomi lote lile!
 
[emoji23][emoji23][emoji23] Kwahiyo Atcl inavyopata hasara haina wateja? Kwahiyo Tanesco pia haina wateja? Kijana uwe ugoogle hata mara moja moja kwa mwezi uondoe hizi aibu ndogo ndogo.

Hebu tupe mapato ya mwendokasi tokea ilipoanzishwa, pamoja na mchanganuo wa matumizi tulinganishe na thamani ya huo mradi ndio upatikiwe majibu ya hayo maswali yako!
Halafu hivi Tanesco nayo inajiendesha kwa hasara...!?
 
Popote mswahili alipo anawaza kuiba tu, check hata kwenye migodi waswahili huko wanashirikiana na wawekezaji kukadiria kiduchu thamani ya madini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…