Hivi unakubaliana na kauli kwamba Mwendokasi wanajiendesha kwa hasara?

Hivi unakubaliana na kauli kwamba Mwendokasi wanajiendesha kwa hasara?

Hebu tupe mapato ya mwendokasi tokea ilipoanzishwa, pamoja na mchanganuo wa matumizi tulinganishe na thamani ya huo mradi ndio upatikiwe majibu ya hayo maswali yako!
Halafu hivi Tanesco nayo inajiendesha kwa hasara...!?

Ndio maana nasema kama mtu huwezi kugoogle tu kuna shida. Tanesco hawajawahi kupata faida. Ulivyo kiazi unaanza kufikilia ni kiasi gani nyumba zilivyo nyingi zinatumia umeme na kununua kila siku.

Kama hata kugoogle ni shida msiwe mnaleta ujuaji.
 
Hizo ni kauli za wezi kuhadaa imma Ili waendelee kuiba. Gari zinajaa hadi unabanwa na mlango. Kama daladala tu zinapata faida sembuse wao.

Ni vigumu kupata hasara kwenye genge lakini TTCL na Tanesco hawawezi pata faida kamwe. Achana na habari za kujaa watu sio hoja kwenye kampuni au taasisi.
 
Mwendo kasi ingefanya kazi kama inavyotakiwa ingepunguza idadi ya magari barabarani pia ingeleta ajira kwa vijana wengi, kuanzia udereva mpaka kusafisha mabasi.
 
Ndio maana nasema kama mtu huwezi kugoogle tu kuna shida. Tanesco hawajawahi kupata faida. Ulivyo kiazi unaanza kufikilia ni kiasi gani nyumba zilivyo nyingi zinatumia umeme na kununua kila siku.

Kama hata kugoogle ni shida msiwe mnaleta ujuaji.
Kiazi bila shaka utakuwa ni wewe! Tena kilaza, binafsi hata kuandika hujui unajidai mjanja wa kugoogle?
Wewe shupalia tu kwamba hao Tanesco wanapata hasara kwa kufanya reference za huko miaka ya nyuma ukidhani huo ndio uhalisia!
Kama wewe ujanja wako upo kwenye kugoogle, hebu fanya hivyo halafu ulete takwimu kwamba kwa mwaka uliopita hadi kufikia Dec 2021 mwendokasi waliingiza Tsh ngapi na hadi kufikia hapo walikuwa wamepata hasara au faida ya kiasi gani, kisha fanya hivyo kwa Tanesco pia.
 
Usafiri ni mmoja ya huduma muhimu serikari inatakiwa kuwafanyia wananchi,( maji, umeme nk) hivyo hata kama wanapata hasara, lazima watafute njia nyingine, ili waendelee kutoa huduma.
 
Hizi zinazokuja mwenge kupitia shekilango hizo kweli ni hasara tu
 
Naona mods wamefyeka baadhi ya comments humu maana uzi pages zimepungua.
 
Zile tiket za mwendokasi ni rahisi kuiba mapato.
Yule mkata tiket Kwa kushirikiana na wenzake wanaweza kutengeneza tiket zao na kuziuza,zile tiket hazikaguliwi,ukishanunua Kwa muuza tiket hakuna mtu anayekagua zaidi ya kuzichana kidogo na kumpa mteja.Mashine zote za kukagulia tiket ni mbovu.
Sishangai kusikia wamepata hasara.
Kinachotakiwa zitumike kadi na machine za kukagulia ziwe nzima.
 
Hapo watachukuwa wenye nchi na kufanya mradi binafsi wa pamoja... ..

Nchi Ina wenyewe hii.. ..
 
Kiazi bila shaka utakuwa ni wewe! Tena kilaza, binafsi hata kuandika hujui unajidai mjanja wa kugoogle?
Wewe shupalia tu kwamba hao Tanesco wanapata hasara kwa kufanya reference za huko miaka ya nyuma ukidhani huo ndio uhalisia!
Kama wewe ujanja wako upo kwenye kugoogle, hebu fanya hivyo halafu ulete takwimu kwamba kwa mwaka uliopita hadi kufikia Dec 2021 mwendokasi waliingiza Tsh ngapi na hadi kufikia hapo walikuwa wamepata hasara au faida ya kiasi gani, kisha fanya hivyo kwa Tanesco pia.

Dah yaani nimeleta hapo bado umeshindwa kubonyeza [emoji23][emoji23][emoji24]
 
Waliondoa card ili mapato halisi iwe Siri Yao,
Sasa wametuwekea komedi ya scanner, na wanachana ticket,
Hapo lazima kuna fungu linaenda ofisi za chama Fulani,
Ndiyo maana hawaguswiii na hawaguswiii!
Nchii hii Bora kimondo kije kiporomokee hapa tuumbwe upya!
 
Kwa nini wasiweke mfumo wa railway kwenye barabara ya mwendokasi ili kupunguza gharama za uendeshaji?
 
Kauli ya kamati ya bunge imeniacha hoi na mshangao sana kwamba eti kampuni ya mwendokasi inajiendesha kwa hasara

Hili nalipinga kwa nguvu zote, kwa jinsi wanavyojaza abiria na wateja wake ni wengi hakuna muda unakuta mwendokasi haijajaa sasa hizo kauli za kwamba wanajiendesha kwa hasara zinatoka wapi?
Ikiendeshwa kwa faida nauli mtaimudu?
 
Back
Top Bottom